Wizi mkubwa unafanywa hivi manunuzi ya magari ya Serikali, pikipiki, ambulance nk, vifaa vya kielectronic vya umma, na manunuzi yote ya Serikali

Ni kweli Kabisa.....Magufuli alikuwa anawashughulikia...Watu wakalalamika. Sasa hivi hawashughulikiwi....watu wanalalamika tena. Sasa nyinyi Wa-Tanzania mnataka nini?
yule marehemu alikuwa sahihi 100% sema kuna majitu jamii ile ya matapeli, dhulma, walevi na wapenda kuua watu kisa mali si wanaume wala wanawake wote wana tabia hizo ndo walikuwa wanamchukia ..
 
Naungana na wewe hao wana iibia nchi na wananchi
 
Bila sheria ya kumalizana kiuchumi hadi kizazi cha 3 wizi na ufisadi hautaisha serikalini. Hela nyingi inapotea mikononi mwa watu badala ilete maendeleo.
Na ninaona viongozi wakuu kama hawana mpango wa dhati kupambana na huu uhuni wana hamishana ofisi tuu
 
Mfumo wa manunuzi ukweli ni kuwa sirikali imeshindwa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, na hicho ni chanzo cha umaskini wetu na umaskini wa taifa letu.Yafaa tujifunze kwa wenzetu wao wameweza je na sisi tumeshindwa je🤔
Na wakisha ona wanataka hela basi ujue lazima wata pendekeza manunuzi ya vitu, mara utasiki paah! Utasikia serikali yaamua kuwanunulia walimu wote laptop, na wao huwa wajanja huwa wanagusa pale pale ambao wanajua kabisa wakipeleka pendekezo litakubaliwa na ndio hapo mpango huanza na usimamizi unapo kuwa wa hovyo.
 
Manunuzi ya kifisadi.
Sio muda utasikia serikali yatumia bilion 68 kununua pikipiki elfu kumi na mbili mia tatu (12300) kwa ajili ya watendaji wote wa vijiji nchi nzima

Halafu ukipiga hesabu bei ya pikipiki moja milion tatu lakini sita ukija tizama aina ya pikipiki ni TVS ambao kwa bei rejareja kariakoo na posta ni milion 2 laki 8 lakin serikali imenunua kwa milion 4 kila moja 🤣🤣🤣 na hapo ni bei ya jumla

Wakati kwa wingi huo wa pikipiki ni rahisi hata kupata kwa chini ya 2.6 mil

Lakin utashangaa pikipiki zimeagizwa moja iwa moja toka kiwandani lakini beinyake inazidi hata bei ya rejareja hapa hapa tanzania tena namtumbo huko 🤣🤣🤣 hii nchi hiii mama asiwachekee hawa wahuni wanao jinufaisha wao wakati kuna watoto wanakaa chini huko shuleni hawana hata dawati la elfu 70 tu.
 
Hamna dawa zaidi ya hio. Tukiweza kuzifanya nafasi za kisiasa zionekane kama ni ualimu tu basi tutafika mbali
 
Kwanini tunanunua TOYOTA TZ kwa bei kubwa wakati pesa ni yetu ns tunao uwezo wa kununua popote kwa toyota kwa bei nafuu,kenya hununua toyota japan kwa bei nafuu sisu TZ tunanunua jwa dealer kwa bei ya juu maradufu.

Kama unanunua gari brand new Toyota hauna namna utakwepa commission inayoenda Toyota Tanzania
 
CCM yapaswa kubadilishwa, imetawala nchi hii muda mrefu sana.

China imetumia miaka 40 kufika hapo ilipo kwa kubadilisha mawazo ya watu wake.

Leo hii China ni nchi yenye nguvu duniani.

Leo raisi wa Ufaransa na raisi wa EU wapo China kuwabembeleza waendeleze ushirikiano na taifa hilo kubwa.

China imetumia miaka 40 kuwaondoa wananchi wake kutoka katika lindi la umaskini wa kutupwa.

GDP ya China leo yasimama zaidi ya dola trilioni 12 nyuma ya USA ambayo ina GDP ya karibu dola trilioni 20.

Alipokufa Mao, China ilianza njia mpya ya kutafuta asali na maziwa wananchi wa vijijini waliruhusiwa kulima mashamba kwenye ardhi zao na kuhimizwa kuhifadhi chakula hivyo kuboresha hali za maisha.

Mwaka 1979 China ikafungua milango yake na Marekani ikawa ya kwanza kuja kuwekeza kwenye viwanda ambavyo vilijengwa kwa fedha za mikopo na pango kwa wawekezaji ikawa ndogo sana hivyo kufanya fedha za nje kumiminika kwa wingi nchini humo.

Tokea hapo leo hii China ni nchi tajiri yenye viwanda mamia kwa mamia

Sasa Tanzania tokea aondoke mwasisi wa taifa hili hayati Mwalimu Nyerere tunazidisha hali yetu ya wizi na ubadhilifu wa mali ya umma na fedha za walipa kodi.

Kibaya zaidi CCM chama cha mapinduzi kikawa ndo kinara wa ufisadi, na ukumbatiaji wa mafisadi kiasi cha kuambizana wengine wajivue magamba na vitu vingine vya ajabu.

Dawa pekee iliyopo mezani kwa sasa ni kubadili katiba yetu na kufuata baadhi ya sera nzuri za wachina, na zile sera kali kwa watu wasoitakia nchi hii maendeleo kwa kuiba fedha za walipa kodi, fedha za miradi zitokazo kwa wafadhili wa nje na fedha zingine kutoka vyanzo mbalimbali.
 
Uvccm na wafia CCM humu wamekimbia hawataki kbs kuona mamb ya CAG!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…