Wizi mkubwa unafanywa hivi manunuzi ya magari ya Serikali, pikipiki, ambulance nk, vifaa vya kielectronic vya umma, na manunuzi yote ya Serikali

Wizi mkubwa unafanywa hivi manunuzi ya magari ya Serikali, pikipiki, ambulance nk, vifaa vya kielectronic vya umma, na manunuzi yote ya Serikali

Ni kweli Kabisa.....Magufuli alikuwa anawashughulikia...Watu wakalalamika. Sasa hivi hawashughulikiwi....watu wanalalamika tena. Sasa nyinyi Wa-Tanzania mnataka nini?
yule marehemu alikuwa sahihi 100% sema kuna majitu jamii ile ya matapeli, dhulma, walevi na wapenda kuua watu kisa mali si wanaume wala wanawake wote wana tabia hizo ndo walikuwa wanamchukia ..
 
Sio kuibia Serikali bali kuibia nchi, ni lini serikali ilikuwa na pesa zake??!



Watendaji wa serikali ndio wezi sasa wewe unataka mwizi ajue/ajitambue yeye mwenyewe kwa wizi wake??!


Ila tunashukuru kwa kutufumbua macho.

Halafu wewe umejuaje kwamba kuna wizi wa aina hizo huko serikalini??!, wewe umesomea upelelelezi??!😀
Naungana na wewe hao wana iibia nchi na wananchi
 
Mfumo wa manunuzi ukweli ni kuwa sirikali imeshindwa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, na hicho ni chanzo cha umaskini wetu na umaskini wa taifa letu.Yafaa tujifunze kwa wenzetu wao wameweza je na sisi tumeshindwa je🤔
Na wakisha ona wanataka hela basi ujue lazima wata pendekeza manunuzi ya vitu, mara utasiki paah! Utasikia serikali yaamua kuwanunulia walimu wote laptop, na wao huwa wajanja huwa wanagusa pale pale ambao wanajua kabisa wakipeleka pendekezo litakubaliwa na ndio hapo mpango huanza na usimamizi unapo kuwa wa hovyo.
 
Manunuzi ya kifisadi.
Sio muda utasikia serikali yatumia bilion 68 kununua pikipiki elfu kumi na mbili mia tatu (12300) kwa ajili ya watendaji wote wa vijiji nchi nzima

Halafu ukipiga hesabu bei ya pikipiki moja milion tatu lakini sita ukija tizama aina ya pikipiki ni TVS ambao kwa bei rejareja kariakoo na posta ni milion 2 laki 8 lakin serikali imenunua kwa milion 4 kila moja 🤣🤣🤣 na hapo ni bei ya jumla

Wakati kwa wingi huo wa pikipiki ni rahisi hata kupata kwa chini ya 2.6 mil

Lakin utashangaa pikipiki zimeagizwa moja iwa moja toka kiwandani lakini beinyake inazidi hata bei ya rejareja hapa hapa tanzania tena namtumbo huko 🤣🤣🤣 hii nchi hiii mama asiwachekee hawa wahuni wanao jinufaisha wao wakati kuna watoto wanakaa chini huko shuleni hawana hata dawati la elfu 70 tu.
 
Ni lazima ifike hatua tukubali kuwa hii nchi na nyingi za Africa bado hazijawa tayari kutawaliwa kidemokrasia, hii nchi inataka sheria kandamizi kusha wawepo watu wa kuzisimamia haswa, ndani ya miaka 3 tu hela ya umma itaogopeka vibaya.

Katiba irekebishwe ili kusiwepo na kiongozi yoyote aliye na kinga, mihimili ipewe nguvu halisi ya kujitegemea.

Akigundulika yoyote kufanya ufisadi, kwanza anyang'angwe mali zake ZOTE, kisha kesi za ufisadi zisiwe na dhamana, ziendeshwe harakaharaka na kifungo kiwe miaka 30 au kunyongwa bila huruma.

Ukionyesha mfano kwa chambo kama watatu hivi, hakuna raia watakaokuwa wanakimbilia teuzi tena.

Bila kudhibiti rushwa tusitarajie maendeleo yoyote yale, hela zinapotea nyingi sana huko.
Hamna dawa zaidi ya hio. Tukiweza kuzifanya nafasi za kisiasa zionekane kama ni ualimu tu basi tutafika mbali
 
Kwanini tunanunua TOYOTA TZ kwa bei kubwa wakati pesa ni yetu ns tunao uwezo wa kununua popote kwa toyota kwa bei nafuu,kenya hununua toyota japan kwa bei nafuu sisu TZ tunanunua jwa dealer kwa bei ya juu maradufu.

Kama unanunua gari brand new Toyota hauna namna utakwepa commission inayoenda Toyota Tanzania
 
CCM yapaswa kubadilishwa, imetawala nchi hii muda mrefu sana.

China imetumia miaka 40 kufika hapo ilipo kwa kubadilisha mawazo ya watu wake.

Leo hii China ni nchi yenye nguvu duniani.

Leo raisi wa Ufaransa na raisi wa EU wapo China kuwabembeleza waendeleze ushirikiano na taifa hilo kubwa.

China imetumia miaka 40 kuwaondoa wananchi wake kutoka katika lindi la umaskini wa kutupwa.

GDP ya China leo yasimama zaidi ya dola trilioni 12 nyuma ya USA ambayo ina GDP ya karibu dola trilioni 20.

Alipokufa Mao, China ilianza njia mpya ya kutafuta asali na maziwa wananchi wa vijijini waliruhusiwa kulima mashamba kwenye ardhi zao na kuhimizwa kuhifadhi chakula hivyo kuboresha hali za maisha.

Mwaka 1979 China ikafungua milango yake na Marekani ikawa ya kwanza kuja kuwekeza kwenye viwanda ambavyo vilijengwa kwa fedha za mikopo na pango kwa wawekezaji ikawa ndogo sana hivyo kufanya fedha za nje kumiminika kwa wingi nchini humo.

Tokea hapo leo hii China ni nchi tajiri yenye viwanda mamia kwa mamia

Sasa Tanzania tokea aondoke mwasisi wa taifa hili hayati Mwalimu Nyerere tunazidisha hali yetu ya wizi na ubadhilifu wa mali ya umma na fedha za walipa kodi.

Kibaya zaidi CCM chama cha mapinduzi kikawa ndo kinara wa ufisadi, na ukumbatiaji wa mafisadi kiasi cha kuambizana wengine wajivue magamba na vitu vingine vya ajabu.

Dawa pekee iliyopo mezani kwa sasa ni kubadili katiba yetu na kufuata baadhi ya sera nzuri za wachina, na zile sera kali kwa watu wasoitakia nchi hii maendeleo kwa kuiba fedha za walipa kodi, fedha za miradi zitokazo kwa wafadhili wa nje na fedha zingine kutoka vyanzo mbalimbali.
 
Sijui ni kwanini Serikali kwenye suala la manunuzi ya mali zake huwa haipo makini kila manunuzi ya Serikali yanapofanyika kuna pesa ya wizi inapita huko na kuna njia mbalimbali zinazotumika hapa ili kuiibia Serikali

1. Kuagiza vitu kwa idadi kubwa tofauti na mahitaji halisi ya Serikali sasa hapa kuna mambo, kwanza vinaagizwa vitu vingi na ndani yake inaingizwa order yao binafsi (Mafisadi) kwa hiyo mfano mahitaji ni 200,000 basi vitaombwa 250,000, hivyo elfu hamsini watajua wao watakavyoupeleka mchakato kati ya wanunuzi na watu wa store na record za ledger book ila Serikali itatoa hela ya 250,000 maana yake hapo kuna vitakavyoingizwa kwenye ledger na kuonekana vimetoka au visiingizwe kabisa kwenye ledger book.

2. Kuongeza gharama za manunuzi mara mbili au zaid ya bei halisi kama kitu kinauzwa Tsh.200,000/ basi serikali itauziwa kati ya Tsh.300,000 hadi Tsh. 350,000/- au zaid

3. Kununua vitu ambavyo ni low quality wakati vinavyohitajika na pesa iliyotoka serikalini ni ya vifaa vyenye high quality ( hili lilijitokeza kwenye vishkwambi, mashine za kusajili wapiga kura, mifumo ya kimtandao ya serikali , servers nk ndio maana mifumo mingi ya Derikali haiishi kusumbua kila mara)

4. Kuchanganya bidhaa original na feki zake, hasa zile zinazohitajika kwa wingi mf. Vifaa vya afya , vifaa vya kielectronic ,vifaa vya miradi ,vifaa vya kazi maalumu nk.

Yaani hapa iko hivi mfano vinahitajika vifaa 200,000 ambavyo bei yake ni Tsh.600,000/- kila kimoja ambacho ni original na high quality, kitakachofanyika ni kununua vifaa 100,000 original kabisa ambavyo navyo unaweza kukuta bei iliongezwa , halafu hivyo 100,000 vilivyo baki vinatafutwa feki yake vifananavyo na vinavyoweza kufanya kazi ile ile ila sio kwa ubora lakini kwa bei ya chini labda Tsh 250,000/- na hapa huwa order inatolewa China maana ndio kuna local industries zenye ubingwa wa kutoa copy za vitu kwa bei ndogo ili pesa ya juu watu waibe

5. Kuleta vitu vilivyoagizwa kwa mafungu mafungu yani kama vilihitajika vifaa labda 200,000 vinaletwa kwanza 130,000 halafu wanasikilizia kwanza kama kutakuwa na kelele wakiona kimya ndio imetoka hiyo vilivyobaki haviji tena pamoja na kwamba Serikali inakuwa ilishatoa hela ya vyote 200,000 na baada ya hapo wanacheza na watu wa record kwenye ledger book idadi inajazwa lakini vitu havipo.

Zipo njia nyingi zaidi na sitaki kuamini kwamba serikali haijui
Uvccm na wafia CCM humu wamekimbia hawataki kbs kuona mamb ya CAG!!
 
Back
Top Bottom