Wizi mkubwa unafanywa hivi manunuzi ya magari ya Serikali, pikipiki, ambulance nk, vifaa vya kielectronic vya umma, na manunuzi yote ya Serikali

GSM na MO wanatumika kuwa brainwash Watanzania kupitia Simba na Yanga.Hakika Watanzania wako busy na Simba na Yanga huku Nchi inazama wao hawana habari.Yule Mwamba wa Msoga hakika akili Mingi.Siku tukiamka tutakuta jamaa wote wameamia state sisi tumeachiwa Waliotukopesha watutawale.Ehee Mungu tusaidie Watanzania tutoke kizani Nchi inatafunwa hii.
 
Sijui ni kwanini Serikali kwenye suala la manunuzi ya mali zake huwa haipo makini kila manunuzi ya Serikali yanapofanyika kuna pesa ya wizi inapita huko na kuna njia mbalimbali zinazotumika hapa ili kuiibia Serikali

1. Kuagiza vitu kwa idadi kubwa tofauti na mahitaji halisi ya Serikali sasa hapa kuna mambo, kwanza vinaagizwa vitu vingi na ndani yake inaingizwa order yao binafsi (Mafisadi) kwa hiyo mfano mahitaji ni 200,000 basi vitaombwa 250,000, hivyo elfu hamsini watajua wao watakavyoupeleka mchakato kati ya wanunuzi na watu wa store na record za ledger book ila Serikali itatoa hela ya 250,000 maana yake hapo kuna vitakavyoingizwa kwenye ledger na kuonekana vimetoka au visiingizwe kabisa kwenye ledger book.

2. Kuongeza gharama za manunuzi mara mbili au zaid ya bei halisi kama kitu kinauzwa Tsh.200,000/ basi serikali itauziwa kati ya Tsh.300,000 hadi Tsh. 350,000/- au zaid

3. Kununua vitu ambavyo ni low quality wakati vinavyohitajika na pesa iliyotoka serikalini ni ya vifaa vyenye high quality ( hili lilijitokeza kwenye vishkwambi, mashine za kusajili wapiga kura, mifumo ya kimtandao ya serikali , servers nk ndio maana mifumo mingi ya Derikali haiishi kusumbua kila mara)

4. Kuchanganya bidhaa original na feki zake, hasa zile zinazohitajika kwa wingi mf. Vifaa vya afya , vifaa vya kielectronic ,vifaa vya miradi ,vifaa vya kazi maalumu nk.

Yaani hapa iko hivi mfano vinahitajika vifaa 200,000 ambavyo bei yake ni Tsh.600,000/- kila kimoja ambacho ni original na high quality, kitakachofanyika ni kununua vifaa 100,000 original kabisa ambavyo navyo unaweza kukuta bei iliongezwa , halafu hivyo 100,000 vilivyo baki vinatafutwa feki yake vifananavyo na vinavyoweza kufanya kazi ile ile ila sio kwa ubora lakini kwa bei ya chini labda Tsh 250,000/- na hapa huwa order inatolewa China maana ndio kuna local industries zenye ubingwa wa kutoa copy za vitu kwa bei ndogo ili pesa ya juu watu waibe

5. Kuleta vitu vilivyoagizwa kwa mafungu mafungu yani kama vilihitajika vifaa labda 200,000 vinaletwa kwanza 130,000 halafu wanasikilizia kwanza kama kutakuwa na kelele wakiona kimya ndio imetoka hiyo vilivyobaki haviji tena pamoja na kwamba Serikali inakuwa ilishatoa hela ya vyote 200,000 na baada ya hapo wanacheza na watu wa record kwenye ledger book idadi inajazwa lakini vitu havipo.

Zipo njia nyingi zaidi na sitaki kuamini kwamba serikali haijui
Hiyo ya bidhaa fake inatumika sana. Niliwahi kuambiwa wakati fulani Serikali ilihitaji pump kubwa za kusukuma maji. Supplier alipewa order ya pumps 15, kila moja dola 35,000. Akaleta na sample, ikakubaliwa. Jamaa aliagiza pump 2 toka Ujerumani, zikawa 3 ukijumuisha na ile ya sample. Moja akaipeleka China kwaajili ya kutoa copy. Wakatoa fake 12 kwa dola 5,000 kila moja.

Zilipoanza kufanya kazi, zile 12 ikawa ni matengenezo kila wakati. Waliopewa zile original 3 wakawa wanasifiwa sana wale wasimamizi kuwa ni watunzaji wazuri, kumbe zilikuwa ni pump tofauti kabisa.

Bila ya wananchi kuinuka na kuupinga huu uovu wa Serikali kwa vitendo, Serikali itaendelra kuwa genge la majizi la kuiba pesa ya umma.

Serikali imejaa majizi na wala rushwa, kuanzia mawaziri mpaka watendaji wa chini (hata PM mwenyewe siyo msafi).
 
Nilipoona TU wakubwa wanahangaika na vihela vya brashi Kwa TRAFIKI nikajua kuwa Kuna rushwa kubwa sana zinafanyika.

Hivi Hela ya Dereva wa Daladala asiye hata na kosa Bali anashika TU kabahsha kake anampa TRAFIKI akanunue maji na Joto la DSM inaathiri Nini pesa za Wizara zilizotungwa na Bunge ?
Pesa inatoka kwenye mfuko wa kondakta unakwenda Kwa ndugu yake ambaye ni TRAFIKI sidhani kama inaweza kuzuia miradi ya maendeleo isikamilike Kwa wakati.
Hatutaki TRAFIKI waonee watu Wala kuwabambika makosa lakini ni kuwapumbaza watu kutumia gharama za serikali kuzunguka Tanzania nzima kuwatangaza TRAFIKI au Polisi kuwa ni Wala rushwa wakubwa ili Hali watu wanakaa kitako ofisini bila jasho wanaikwapua mabilioni ya pesa zilizotungwa kwenye miradi ya maendeleo na Bado watu hao au wakubwa hao Wana mishahara mikubwa na marupurupu Kibao.
Kwa Sasa wakuu wa Idara kila siku ni kiguu na njia safari na kujilipa posho ya safari huku stahiki na madeni ya watu wa chini yakiwa hayalipwi . Na mbaya zaidi Serikali ya hii haitumii muda Mwingi kusikiliza Kero za watumishi wa chini wanavyoonewa na wakubwa.

Mfano suala la Wakubwa wa Polisi kushirikiana kuiba fedha za rambimbirambi ni jambo ambalo lingeweza kudhibitiwa kama pangekuwa na Baraza au bodi nje ya Polisi ya kusikiliza malalamiko ya Polisi wa chini.
Iundwe bodi Toka Majeshi mengine na usalama wa Taifa kusikiliza Kero za watumishi wa chini . Kuna mwanya mkubwa sana wa kula pesa zinazowahusu watumishi wa chini.

Nimeona Kuna Wilaya Fulani nayo inataka kuwachangisha walimu michango ya RAMBIRAMBI Kwa kuwakata kwenye mishahara lakini nyuma yake ni kwamba wamegundua kuwa ni pesa ambazo ni rahisi kuziiba kimya kimya na watu maisha yakaendelea.

Mama Samia inabidi akubali kuwa kuwategemea makada na Chawa itampa ugumu sana kuzibiti wizi wa Mali za umma.
Leta Katiba mpya mapema kabisa. Au vinginevyo chagua Mawaziri na wakuu wa Idara Toka nje kabisa ya makada wezi wanaoshindana kulimbikiza Mali na wanaambizana kabisa ukipata nafasi itumie usije ukaihutia !! Hawana hofu mana wanalindana , wanajua muda wako ni miaka Kumi utastaafu na wao watakua wanamiliki mabilioni ya pesa ndani na nje ya nchi huku watanzania wengi wakiendelea kuteseka Kwa kukosa ajira, miundombini Duni, Kodi kubwa na Riba kubwa kwenye mabenki. Hakika Mama Utakua hujatenda haki mbele za Allah aliyekupa nafasi ya juuu kabisa Duniani. Sijui utajibu Nini mbele za Allah, kwamba ulitaka akupe Nini ili usimamishe Taifa lenye kutenda haki lakini pia Taifa linalowakataa na kuhukumu madhalimu Kwa udhalimu wao waliofanya juu ya ardhi huku wakimkufuru Allah Kwa ulevi,uzinzi, kiburi , starehe,udanganyifu, ushirikina , ufiraji na hata kumwaga damu za wale wanaowataja Kwa uwazi .

Mh. Rais umepewa mamlaka makubwa na Allah na Katiba kukupa sharia Kali za kuwafukuza na hata kuwafilisi Mali walizoiba ni vizuri ukasimama kidete kulinda Mali za umma mkubwa wa watu kuliko kuwaonea aibu watu wa Chache huku wengi wakiumia .
 
PPRA ijitathmini na sheria zake mbovu ili kupunguza kazi kwa CAG na PCCB otherwise watalipuliwa sana wana wa manunuzi, DEDs na maafisa mipango na hili lipo sana upuuzi sana
 
Sijui ni kwanini Serikali kwenye suala la manunuzi ya mali zake huwa haipo makini kila manunuzi ya Serikali yanapofanyika kuna pesa ya wizi inapita huko na kuna njia mbalimbali zinazotumika hapa ili kuiibia Serikali

1. Kuagiza vitu kwa idadi kubwa tofauti na mahitaji halisi ya Serikali sasa hapa kuna mambo, kwanza vinaagizwa vitu vingi na ndani yake inaingizwa order yao binafsi (Mafisadi) kwa hiyo mfano mahitaji ni 200,000 basi vitaombwa 250,000, hivyo elfu hamsini watajua wao watakavyoupeleka mchakato kati ya wanunuzi na watu wa store na record za ledger book ila Serikali itatoa hela ya 250,000 maana yake hapo kuna vitakavyoingizwa kwenye ledger na kuonekana vimetoka au visiingizwe kabisa kwenye ledger book.

2. Kuongeza gharama za manunuzi mara mbili au zaid ya bei halisi kama kitu kinauzwa Tsh.200,000/ basi serikali itauziwa kati ya Tsh.300,000 hadi Tsh. 350,000/- au zaid

3. Kununua vitu ambavyo ni low quality wakati vinavyohitajika na pesa iliyotoka serikalini ni ya vifaa vyenye high quality ( hili lilijitokeza kwenye vishkwambi, mashine za kusajili wapiga kura, mifumo ya kimtandao ya serikali , servers nk ndio maana mifumo mingi ya Derikali haiishi kusumbua kila mara)

4. Kuchanganya bidhaa original na feki zake, hasa zile zinazohitajika kwa wingi mf. Vifaa vya afya , vifaa vya kielectronic ,vifaa vya miradi ,vifaa vya kazi maalumu nk.

Yaani hapa iko hivi mfano vinahitajika vifaa 200,000 ambavyo bei yake ni Tsh.600,000/- kila kimoja ambacho ni original na high quality, kitakachofanyika ni kununua vifaa 100,000 original kabisa ambavyo navyo unaweza kukuta bei iliongezwa , halafu hivyo 100,000 vilivyo baki vinatafutwa feki yake vifananavyo na vinavyoweza kufanya kazi ile ile ila sio kwa ubora lakini kwa bei ya chini labda Tsh 250,000/- na hapa huwa order inatolewa China maana ndio kuna local industries zenye ubingwa wa kutoa copy za vitu kwa bei ndogo ili pesa ya juu watu waibe

5. Kuleta vitu vilivyoagizwa kwa mafungu mafungu yani kama vilihitajika vifaa labda 200,000 vinaletwa kwanza 130,000 halafu wanasikilizia kwanza kama kutakuwa na kelele wakiona kimya ndio imetoka hiyo vilivyobaki haviji tena pamoja na kwamba Serikali inakuwa ilishatoa hela ya vyote 200,000 na baada ya hapo wanacheza na watu wa record kwenye ledger book idadi inajazwa lakini vitu havipo.

Zipo njia nyingi zaidi na sitaki kuamini kwamba serikali haijui
Bosi walishawaambia kila mtu ale kwa urefu wa kamba, sasa matokeo ya urefu wa kamba ndio haya na hawatafanywa chochote, wananchi tuamke tusitegemee kuna mtu atakuja kutusaidia kupambana na hawa mabaradhuli wabadhirifu
 
Hiyo ya bidhaa fake inatumika sana. Niliwahi kuambiwa wakati fulani Serikali ilihitaji pump kubwa za kusukuma maji. Supplier alipewa order ya pumps 15, kila moja dola 35,000. Akaleta na sample, ikakubaliwa. Jamaa aliagiza pump 2 toka Ujerumani, zikawa 3 ukijumuisha na ile ya sample. Moja akaipeleka China kwaajili ya kutoa copy. Wakatoa fake 12 kwa dola 5,000 kila moja.

Zilipoanza kufanya kazi, zile 12 ikawa ni matengenezo kila wakati. Waliopewa zile original 3 wakawa wanasifiwa sana wale wasimamizi kuwa ni watunzaji wazuri, kumbe zilikuwa ni pump tofauti kabisa.

Bila ya wananchi kuinuka na kuupinga huu uovu wa Serikali kwa vitendo, Serikali itaendelra kuwa genge la majizi la kuiba pesa ya umma.

Serikali imejaa majizi na wala rushwa, kuanzia mawaziri mpaka watendaji wa chini (hata PM mwenyewe siyo msafi).
Yapo mengi sana haya yanafanywa nashangaa kuna watu wanajiita usalama wa taifa eti "ulipo tupo" , haya yanapo fanyika kama kweli wao wapelelezi kwa nyanja zote huwa wawayaoni? Kwanini wasi rescue kabla ? Ili kweli tuwaone ni wapigania usalama na mali za taifa!? Au nao ni usalama wa mali za mafisadi.
 
Back
Top Bottom