Wizi wa kura wa mwaka 2019 na 2020 umesabisha CCM kichukiwe sana

CCM sanduku lao la kura ni TISS na Polisi, bila hao, mapema tu asubuhi hawapo.
 
Wewe unaishi Dunia ya peke yako kama unadhani Magufuli alichaguliwa kwa kura za wananchi
 
Usijijaze UJINGA. Magufuli aliiba uchaguzi wa 2019 wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020 kwa kutumia NEC, TISS na Police.

Angalia hata Bunge aliloliacha, siyo Bunge bali kundi la watu fulani wanakaa Dodoma kula Kodi zetu
 
Wewe unaishi Dunia ya peke yako kama unadhani Magufuli alichaguliwa kwa kura za wananchi
Kuukataa huu upuuzi wako ndio kuishi dunia ya pekeangu?
Hiyo dunia ya pekeangu inawezaje kukuruhusu wewe kushiriki mjadala na mimi?
Kajipange uje na hoja zenye mantiki sio kutuandikia vijihadithi visivyo na kichwa wala miguu
 
Kuwatoa wafanyakazi wa "vyeti feki" huku yeye mwenyewe Magufuli akiwa na PhD feki na Makonda wakiwa na vyeti feki
  • Kutotoa nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi
  • Kupeleka miundombinu mikubwa kwao Chato
  • Kukataa wazi wazi kupeleka maendeleo kwenye majimbo yanayoshikiliwa na UPINZANI
[emoji1534][emoji1534][emoji1534][emoji1534][emoji1534]
 
Gerald .M Magembe Mara nyingine watendee haki wazazi wako wajisikie walizaa binadamu na siyo zombie.

Kweli unaamini Hai kulikuwa na uchaguzi?
 
TISS wa wenzetu wapo bize kuiba fursa za uchumi mataifa ya nje Ili kujenga kwao na sio bize kupanga wizi wa kura.
China ukiimport chochote toka nje ya nchi maadamu tu kinakwenda boost uchumi wao na kodi unasamehewa au punguziwa kabisa.
Ingefaa magari,mitambo na chochote kinachokuja kukuza uchumi wetu kiruhusiwe kuingia bila kodi.
Kodi itajilipa indirect kwenye profit ya mzunguko.
 
Ishu ya vyeti feki ilikuwa ni kumpooza machungu bashite kutokana na makombora ya rashid enzi za ndoa changa za maswaiba, ndumba zilipoexpire wakatosana.
 
Wabunge wote wa ccm Hakuna atakaerudi bungeni wengi awakupita bali waliletewa ubunge na magufuli
 
Usiishi kwa kukariri denooJ. Unakosoa panapoharibiwa na unapongeza palipofanywa vizuri
Labda wapo wengine wanaokuelewa niwaache wachangie mada ila mimi nakuona unajichanganya sana, hujui ila unajiamini kwenye ujinga wako.

Kwamba unamkosoa Mbowe kwa kudai Katiba Mpya wakati Samia kasema isubiri kwanza, halafu bado unalaumu faulo zilizofanyika wakati wa uchaguzi kwa kudai haukuwa huru na haki.

Unadhani ukikaa uwasubiri mpaka wawe tayari huo uchaguzi nao utakusubiri? hujawahi kusikia wakisema mwisho wa uchaguzi mmoja ndio mwanzo wa uchaguzi unaofuata?

Mimi kwa upande wangu sioni chochote unachosema kilifanywa vizuri, zaidi nakuona kama mtu usiejua unachopigania, na uko tayari kupangiwa na adui zako muda gani uanze vita inayowahusu.
 
Bado unaendelea kuonesha ulivyo ndumilakuwili, kwako suala la kudai haki linahitaji "timing" halafu unakuja hapa kulia lia CCM waliiba kura, nikisema nawe haya madai yako hayana maana coz umekosea "timing" nitakuwa nakosea?!
Mleta mada ni pumbavu tu tena chawa wa Samia!

Kwa akili yake anaamini ccm ya kabla ya Magufuli iliuwa inapendwa sana na wanachi.

Huyu takuwa kazaliwa miaka ya juzi juzi ty hapa.
. Hajui kama kuna kipindi ilikuwa ukipita na nguo ya ccm pale kariakoo unazomewa! Hajui!
 
Wenye akili hawakurupuki kama akina Mbowe, huhitaji muda watafakari kwanza. Kumbuka Mbowe alikuwapo kwenye Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014/15 na yeye anakumbukwa sana kwa kuwaongoza UKAWA kutoka ndani ya Bunge.

Akili iliyotumika kutomalizia Katiba haiwezi kutuongoza kudai Katiba. Hata yule mwanafalsafa Albert Einstein anasema; "Problems will never be solved by the same mind that created them"

Raia kakuambia nipe muda, kwa nini usiheshimu madaraka yake angalao kwa mwaka mmoja ndiyo uje uanze.

Wewe denooJ huwezi kunielewa kwa kuwa mimi siko CCM wala CDM, napiga kote kote. Wewe akili yako imefungamana na CHADEMA..Na tatizo lenu hakuna mtu mwenye kufikiri tena, akikosea yeye ndiyo imetoka hiyo.
 
Hata sasa hivi ukifanyika uchaguzi wa huru na haki CCM wanaondoka madarakani.
 
Hata wanaccm wenyewe hawakupenda kuaibika vile. Ushindi wa kulazimisha kwa Ugoko haunogi
 
CCM haijawahi kupendwa. Wakongwe anakumbuka kuwa 1995 Maalim alishinda uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Zanzibar. Chombo kimoja cha habari kikamtangaza mshindi. Matokeo yalipindiliwa na chombo hicho kikaadhibiwa kwa kutangaza ukweli.
 
mnafiki mkubwa
 
Unapiga vipi kote kote wakati unalalamika uchaguzi Tz hauko fair halafu at the same time yule anayepigania kuondoa hali hiyo unamuona anakosea kwasababu hakutii kauli ya anayewanyima haki yao?

Simply wewe ni goigoi usiejua unachopigania.

Siku zote niko upande wa haki bila kujali itikadi, muda, sura, etc ila wewe kutambua hili kwa huo upeo wako bado sana.
 
Point tatu za msingi
1. CCM hawajaanza kuiba kura 2019 wala 2020. Wizi wa kura upo kwenye DNA ya CCM. Waliiba kura 1995, 2000 (na kusababisha mauaji Zanzibar), 2005 (mtandao wa jk kazini), 2010 (kitengo wakalazimika kukanusha hadharani kuwa hawajaiba kura), 2015 (hapa kosa kubwa lilikuwa kwa upinzani kumsimamisha kada wa CCM Lowassa) na hiyo 2019 na 2020. Na wataiba kura tena 2025.
2. Mtu anapoibiwa halafu anaishia kulalamika tu kuwa ameibiwa, haina tofauti na anayekaa kimya baada ya kuibiwa. Wapinzani waeleze wamefanya wamefanya nini dhidi ya wizi huo mfulilizo?
3. Mapungufu ya CCM sio uimara wa upinzani. Moja ya sababu za CCM kibaki madarakani miaka mingi ijayo, apart from huo wizi wa kura, ni kukosekana kwa credible opposition. Let's face it, chama ambacho ukipishana nao tu mtazamo inakuwa halali kwao kutukana, kikikabidhiwa dhamana ya nchi kitakuwa na tofauti gani na CCM?
 
Unalaumu wapinzani bila kushauri nini kifanyike ili waimarike.Wewe mwenyewe upo ughaibuni hutaki kurudi ila unataka sisi tuliopo huku tufanye kitu tuvunjwe viuno.watanzania niwaelewa sana tutaendelea kupinga ccm kwa njia ya kura hadi pale watakapochoka kuiba kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…