Wizi wa kwenye mabasi wanaswa na kamera ya bus la ABC

AISEEE!!!

Mwizi aliekwapua begi kavaa kiheshima huwezi kumdhania, hata alieibiwa kampisha apite kiheshima.

  • Kavaa miwani kujifeki kaelimika + hekima.
  • kofia yenye bendera kuonekana mzalendo
  • shati la kitenge kuonekana anajali maadili, tamaduni na dini.
  • mkononi ana maji kuzuga kipaumbele chake ni afya.

Binafsi nikisafiri lazime niwe na mabegi mawili, la nguo suitcase ntaweka juu (kama halitoshi ntalikabidhi liwekwe chini ya basi) lakini kwa upande wa begi dogo la mgongoni azima nilipakate muda wote, huwa naweka laptop, Simu, nyaraka, vyeti, pesa, n.k, yani hata nikienda kuchimba dawa ninalo, Hata nizoeane vipi na jirani siwezi kuliacha hata kwa dakika.

 
Wezi wanaiba kutokana na mazingira
Yaliyopo

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…