Ngumu sana....Mimi mpaka Leo na RB ya dogo mmoja ni wanted aliiba 10M video na camera Kila kitu zilimuonyesha hatua zake zote.....................
Hii dar es salaam ni kubwa sana na ni ngumu kumpata otherwise wangekua na program kama za KGB au FBI au CIA au Mossad alama za mikono na picha zao zingeingizwa kwenye data base...
Kama walijiandikishaga
Mambo ni mengi muda mchache..😊
Wizi upo tu mkuu.
Niliwahi kupigwa matukio mara 2 kipindi fulani nikakoma.
Safari inaanza kwenda Mbeya.
Rungwe express.
Doc zoote ziko ndani ya begi kubwa na laptop nimejaza humo na camera mazaga kibao.
Fika Msamvu kuchimba dawa nilikua na kijana wangu.
Foleni chooni.
Tulikua tumekaa mbele pale na dereva nikamuaga kabisa kasema poa nawangoja.
Tunatoka kule Bus halipo
Nikapagawa
Wazo langu lile begi mle ndani wameenda nalo.
Boda wakanifata kaka rungwe imeenda ila tuifwate tu kabla haijashika njia kuu.
Sikuuliza
Tukapiga mshkaki mbio zikaanza.
Kweli tukalikuta mbele tu ndio linakamata barabara ya mikumi.
Piga mkono kasimama tukapanda.
Aisee ilibaki kidogo nimpe makofi yule dereva.
Bahati alikua mpole kaomba msamaha yakaisha.
Tukio la pili.
Mbeya pale 8×8.
Tumefika wale wapiga debe wanangangania begi kubwa.
Mmoja kalilamba.
Kapakia mzigo tulikua wanne.
Tumeingia ndani gari imejaa.
Ikabidi tushuke maana gari za kyela nyingi zipo.
Ile tunashuka yule konda msenge yule kumwambia dereva amsha.
Wakatimua kwa fujo zote.
Nikashikwa kiwewe tena.
Mle kwenye begi kubwa😁.
Toka mbio chukua taxi pale baloon nikajua ataiwai.
Kumbe gari mbovu kichizi na haina mafuta.
Tumetoka kidogo tu kufika pale relini likagima
Aisee nilichanganyikiwa.
Mungu alikuwepo.
Mara boda huyu anapita.
Piga mkono tukadandia.
Mbio tena.
Mpk Uyole mbele pale Uporoto ndio tukaikuta.
Huyo konda aliyepakiza begi anapiga debe.
Aisee sikuuliza kwanza nilipiga kichwa kadondoka kule.
anainuka aah brother ni wewe mawenge kibao.
Nikamwambia shusha begi.
Kashusha mwenyewe.
Sasa sijui alikua analipeleka wapi,
Ikabidi nimpigie mdingi aje na private car tutimke.
Niliapa sipandi tena mabus public