Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 2,235
- 4,252
Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kwa bandari ya Dar es Salaam kukabidhiwa kwa DP World, lakini sababu kubwa zaidi ni wizi wa mapato ya Serikali uliokithiri pamoja na dhuluma kubwa kwa wateja wanaoagiza mizigo bandarini.
Mizigo inayopita bandarini ni mingi sana lakini Serikali imekuwa haipati mapato sahihi ya bandari hiyo kwani fedha hizo zimekuwa zikidhulumiwa tangu kipindi cha Mwl Nyerere na hata alipokuja Dr Magufuli wizi huu ulimkera sana na kujaribu kuchukua hatua ambazo hazikuzaa matunda.
Watanzania tujitoe boliti kwenye macho yetu ndipo tumnyooshee kidole raisi Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali kwa uamuzi waliochukua.
Watanzania tujiulize je tumekuwa tukipeleka mapato sahihi serikalini kama tulivyopaswa kufanya? Je hatukuwa tukidhulumu wateja wanaoagiza mizigo kupitia bandari hiyo? Lengo la Serikali kuleta wawekezaji DP World ni kupata mapato makubwa kwasababu ya uendeshaji wao mzuri wa bandari usiokuwa na hujuma.
Kama kusingekuwa na wizi na ubadhilifu unaofanyika bandarini basi Serikali isingewakumbuka wawekezaji wa nje ya nchi.
Watanzania tujifunze kuacha hujuma kupitia uamuzi huu wa DP World kwenye mali za Serikali kwasababu kadiri itakavyozidi kukosa mapato sahihi ndipo itazidi kualika wawekezaji kutoka nje ya nchi yetu ili wasimamie kwa haki.
Reference: