Wizi wa Tsh milioni 400 katika ujenzi wa vituo vya Afya Ndago na Kinampanda wilayani Iramba, nini hatma ya DC na DED?

Wizi wa Tsh milioni 400 katika ujenzi wa vituo vya Afya Ndago na Kinampanda wilayani Iramba, nini hatma ya DC na DED?

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Mtakumbuka mwaka 2019 waziri Mkuu Kasim Majaliwa aliibua wizi mkubwa wilayani Iramba mkoani Singida. Waziri Mkuu katika ziara yake aliwaambia wanainchi kuwa serikali ilitenga mabilioni ya fedha kwa ujenz wa vituo vya Afya kote nchini.

Alisema ktk wilaya ya Iramba zaidi ya Tsh million 400 zimefujwa katika ujenzi wa vituo vya Afya Ndago na Kinampanda. Aliilamu Ofisi ya DC na DED kwa wizi huo. Waziri Mkuu aliahidi hatua kuchukuliwa lakini hatua hizo hazijachukuliwa hadi leo April 2021.

Kuna tetesi kuwa Majaliwa sio mamlaka ya teuzi na tenguzi kwa viongozi hao na hakusikilizwa.

Jeje nini hatma ya fedha hizi za umma? Je, vituo vya Afya Ndago na Kinampanda vitaletewa hela nyingine?

Je, DC na DED Iramba walilindwa na nani?
 
Back
Top Bottom