Wizi wa viatu msikiti wa Manyema

Wizi wa viatu msikiti wa Manyema

Viatu vinawekwa nje wewe huingii navyo msikitini so kila mtu wa dini yeyote anaweza kuiba.Huwezi ku assume tu kwamba aliyeiba ni wa dini fulani.Ukiwa unatumia ubongo kufikiri ungelielewa hilo.Hata mtoto mdogo anaweza kulielewa hilo.Au taa tu zimewaka na wapangaji hamna?
Hapa naomba nipingane na wewe kidogo,mwizi lazima ni muislam na tena aliingia ndani ya msikiti kama muumini wa kawaida na kuswali aliswali kama wengine!

Kama mimi mwizi siwezi kuwa napita tu njia nikaona pale nje kwenye mlango wa msikiti pana viatu nikaenda kujiokotea nikaondoka salama(kwa mji kama Dar) huyu mwizi anakuwa miongoni mwa hao hao waumini na anaingia anaswali tofauti yeye anawahi kutoka kupishana second kadhaa na wenzake.
 
Hii kujichukua video na kuitupa mtandaoni naona haijakaa sawa yeye siyo wa kwanza kuibiwa viatu msikitini,unawezakuta ni baba wa familia ya watoto watano..
asipost ili muzid kuibia wengine wasiojuwa ? kawastua watu msikitin uwe na ndala local mtu haez zitamani kbs
 
Kule Tanga kuna mtaa mmoja unaitwa mti mkavu unapatikana kata ya Makorora,
Basi siku moja mwizi alijichanganya akaenda kuiba pale .
Bwana bwana kumbe maostaadhi walishachoka kuibiwa wakaamua kuweka mtego na jamaa akanasa,
Wallah maostaadh wamebarikiwa sana katika nyanja nzima ya kutoa kipigo heavy,picha linaanza wakajifungia nae ndani ya msikiti ili wasiohusika wasije kufaidi kumpiga kuliko wao ,
Bwana bwana kibano kikaanza maostadhi kanzu wamezikunja zimekuwa kama mashati🤣🤣🤣 nikasikia" maalim Omary hivi lile teke la maiguch unalikumbuka mwenzake akajibu hapana mara tukasikia shwaaaah puuuuuuh, mpaka polisi kuja wamekuta nyanya si mtu hoooi mno
 
Hii kujichukua video na kuitupa mtandaoni naona haijakaa sawa yeye siyo wa kwanza kuibiwa viatu msikitini,unawezakuta ni baba wa familia ya watoto watano..
Huyo mzee ni mswahili mswahili. Kasema amezaliwa Dar, kakulia Dar na ujanja wake kaibiwa viatu. Sasa sijui ukiwa mjanja umo msikitini unaweza kujua ya nje? Halafu kaenda na kuwachukua video hadi hao walinzi ambao hata hawahusiki na ulinzi wa msikitini, ila inaonekana ni rafiki wake.
 
Kuna mtego waliweka jamaa alisema leo mpaka nikamate waizi wa viatu
Baada ya Sala kuanza dogo akaja akaanza kukusanya viatu kama vya kwake
Jamaa kamdaka akamwambia utakaa hapa mpaka waumini watoke kuswali
Dogo akaulizwa viatu huwa unapeleka wapi ukiiba akasema mtumbani daa
Sio muumini bali kibaka tu
 
Wa Dini yoyote ile si ana ajiriwa tu.
Kama walinzi wengine.
Ila ni vizuri awe wa Dini hiyohiyo.
Mkuu hao wahuni wataingia peku kuzuga zuga msikitini harafu anazuga kutoka anachangua vile viatu vikali anasepa navyo, harafu mguu ule ule unaomtosha huyooo anapotea🤣
 
Back
Top Bottom