Wizi wa wahudumu wa kwenye vituo vya kujaza mafuta

Sio lazima usubiri ajira, unaweza ukaajiriwa hukohuko au kujiajiri huko kwenye sekta ya gari na ukapita pale kujaza mafuta, mimi kwa taarifa yako nimejiajiri kama bodaboda!
Safi sana mkuu

Ushauri wako nitaufanyia kazi
 
Kwa kuwa nilishajua ni majini na walishaniliza. Nikifika napaki gari nazima, nafungua tank, nashuka chini namwambia sasa weka ya Sh kadhaa na acha pump ifanye kazi automatic. Na walishanizoe kwa kuwa ndiyo kituo changu Kikuu hata nikiwa sina mafuta nikiongeza kituo kingine nafanya hivyo hivyo.
 
Wizi wao kwasasa ni kua na pampu ilio jikunja ndefu mafuta yanabaki kwenye pampu na anarudisha pampu vizuri tu ukiondoka anamimina kwenye dumu dogo la lita tano likija wanauzia bodaboda ndo wizi wao kwa wasasa.

Haya wanafanywa kwenye vituo ambavyo supervision sio nzuri, hao pampu attendants hawakosi 20,000 to 30,000 kwa siku hususani wanao fanya night shift wanahudumia walevi wengi na watu wakusafiri usuku.
 
Hiwa wanawekaga tangazo, kwamba hakikisha pump inasoma kuanzia Zero
 
Huwa ni hivi anapokuja mtu wa boda boda akaweka mafuta ya elfu 5 ile handle inarudishwa sehemu yake lakini sio kamili ile pini inayokata namba inakuwa bado ipo mbali kama vile imeegeshwa tu.

Tatizo lake hapo mmiliki wa kituo anapata hasara ya umeme maana yake ile pump itakuwa ina endelea kuunguruma mda wote mota inazunguka inakula umeme.

wanafanya hivyo kwa kuwa kituo chao magari mara kwa mara yana kuja. Pili jitahidi kusoma risiti yako inasoma kiwango cha pesa na lita sawasawa
 
Nilishawahi kupigwa Simba Oil ilioko kwenye junction ya kwenda kambini na njia ya kwenda maji chumvi! Wizi wa kipumbavu sana.

Alinipiga buku 6 na ilikuwa naweka mafuta nikalaze gari mi huwa silazi gari bila kuweka mafuta ya kulalia.😁! Gauge huwa inatick after 1.5-2 Km ukiona haijatick jua mafuta hayajaingia.
 
Kwani ukiwa kwenye gari huwezi kusoma? Labda iwe basi au lori.
 
NAWAFUNDISHENI DAWA MOJA TU MUITUMIE HUWEZI KUIBIWA.UKIFIKA KITUO CHOCHOTE CHA MAFUTA KABLA HAJAANZA KUKUWEKEA MAFUTA.MFANO UNAWEKA YA ELFU 10 MWAMBIE AKUBONYEZEE PALE KWENYE BUTTON ZA PUMP ELF 10 ILI MAFUTA YAINGIE YENYEWE BILA YEYE KUPRESS LOCK YA PUMP IKIFIKA ELF 10 ITAJIKATA YENYEWE. lakini kama utamwacha yeye mwenyewe anacontrol lock ya pump kwa kidole huku anangalia pump ifike elf 10 ujue atakuibia tu.na saa zingine huwa wana press kile kibutton cha kutolea mafuta mara anachia mara anabonyeza maana yake zile namba zinakwenda haraka anaposimamisha meter inakimbia huku mafuta hayatoki
 
Hizo Petrol Station za ajabu ajabu huwa sijazagi mafuta labda itokee gari imenizimikia karibu na hizo sheli. Kwa sasa sheli za uhakika ni Oryx na Total zimekaa ki proffessional zaidi ila kwengine ambako napaamini ni Lake Oil!
Hii michezo ipo petrol station moja ipo tabata sheli kituo after kwa bibi.....

Pale ukizubaa unaachwa feri....

Wengine wapo pale kituo after external kabla hujafika mwananchi upande wa kuelekea buguruni ni wapigaji hataree ...
 
Kama nia yake ni kukuibia si lazima mtalumbana tu 😂
 
... thanks. Nimeelewa. Ni muhimu ku-confirm meter reading kabla mafuta hayajaanza kuingia kwenye tank.
 
Kwahio akiunyanyua anaendelea alipoishia mwenzio 😂
 
Mkuu sisi haya maswahibu hayatukuti, sisi wazee wa vidumu!! Yaani wese la buku kumi kumi haibi hata mia...anaanzaje kwanza!!
 
Hizo Petrol Station za ajabu ajabu huwa sijazagi mafuta labda itokee gari imenizimikia karibu na hizo sheli. Kwa sasa sheli za uhakika ni Oryx na Total zimekaa ki proffessional zaidi ila kwengine ambako napaamini ni Lake Oil!
Sio kweli kaka labda unaziamini kwa kuwa hazina wizi.ila kwa ubora wa mafuta na kuifanya engine yako idumu ni vituo viwili tu. Kwanza kabisa PUMA ukiikosa puma basi nenda TOTAL
 
Hii michezo ipo petrol station moja ipo tabata sheli kituo after kwa bibi.....

Pale ukizubaa unaachwa feri....

Wengine wapo pale kituo after external kabla hujafika mwananchi upande wa kuelekea buguruni ni wapigaji hataree ...

Una maanisha Victoria Petrol Station iliyopo pala kituo kinaitwa Garage? Njia panda kwenda Makuburi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…