Wizi wa wahudumu wa kwenye vituo vya kujaza mafuta

Wizi wa wahudumu wa kwenye vituo vya kujaza mafuta

Sio lazima usubiri ajira, unaweza ukaajiriwa hukohuko au kujiajiri huko kwenye sekta ya gari na ukapita pale kujaza mafuta, mimi kwa taarifa yako nimejiajiri kama bodaboda!
Safi sana mkuu

Ushauri wako nitaufanyia kazi
 
Kwa kuwa nilishajua ni majini na walishaniliza. Nikifika napaki gari nazima, nafungua tank, nashuka chini namwambia sasa weka ya Sh kadhaa na acha pump ifanye kazi automatic. Na walishanizoe kwa kuwa ndiyo kituo changu Kikuu hata nikiwa sina mafuta nikiongeza kituo kingine nafanya hivyo hivyo.
 
Wizi wao kwasasa ni kua na pampu ilio jikunja ndefu mafuta yanabaki kwenye pampu na anarudisha pampu vizuri tu ukiondoka anamimina kwenye dumu dogo la lita tano likija wanauzia bodaboda ndo wizi wao kwa wasasa.

Haya wanafanywa kwenye vituo ambavyo supervision sio nzuri, hao pampu attendants hawakosi 20,000 to 30,000 kwa siku hususani wanao fanya night shift wanahudumia walevi wengi na watu wakusafiri usuku.
 
Huwa ni hivi anapokuja mtu wa boda boda akaweka mafuta ya elfu 5 ile handle inarudishwa sehemu yake lakini sio kamili ile pini inayokata namba inakuwa bado ipo mbali kama vile imeegeshwa tu.

Tatizo lake hapo mmiliki wa kituo anapata hasara ya umeme maana yake ile pump itakuwa ina endelea kuunguruma mda wote mota inazunguka inakula umeme.

wanafanya hivyo kwa kuwa kituo chao magari mara kwa mara yana kuja. Pili jitahidi kusoma risiti yako inasoma kiwango cha pesa na lita sawasawa
... how possible is this? Kwa sababu, unless ulimkuta ile handle kaishikilia mkononi, ila ikisharudishwa mahali pake na kunyanyuliwa tena automatically ina-clear digits zote to zero. Yaani anawezaje kuanzia kiwango tofauti na zero? Naomba kuelimishwa.
 
Wizi hutokea hasa kama umetangulizana na bodaboda. Bodaboda huwa wanajaza mafuta yasiyozidi 5000, kwa hio ukienda ww anaanzia pale alipoishia wa bodaboda. Kwa kuwa mara nyingi mafuta yanaweka ya 2000 ama 3000 basi ww kama hujaangalia pampu huwezi kushituka mapema kwamba kuna elfu 2 imeibwa. Ukiona unaitiwa kwenye pampu ilipotoka pikipiki basi uwe makini sana.
Nilishawahi kupigwa Simba Oil ilioko kwenye junction ya kwenda kambini na njia ya kwenda maji chumvi! Wizi wa kipumbavu sana.

Alinipiga buku 6 na ilikuwa naweka mafuta nikalaze gari mi huwa silazi gari bila kuweka mafuta ya kulalia.😁! Gauge huwa inatick after 1.5-2 Km ukiona haijatick jua mafuta hayajaingia.
 
Hao wahudumu wamegundua wateja wengi wana tabia ya kuwekewa mafuta wakiwa ndani ya gari, sasa wameamua kujiongeza, hapa jambo la msingi kila mwenye gari akifika kituo cha mafuta ahakikishe anatoka ndani ya gari atazame pump inasomaje ili ajiridhishe, kinyume cha hapo nikupigwa sana.
Kwani ukiwa kwenye gari huwezi kusoma? Labda iwe basi au lori.
 
NAWAFUNDISHENI DAWA MOJA TU MUITUMIE HUWEZI KUIBIWA.UKIFIKA KITUO CHOCHOTE CHA MAFUTA KABLA HAJAANZA KUKUWEKEA MAFUTA.MFANO UNAWEKA YA ELFU 10 MWAMBIE AKUBONYEZEE PALE KWENYE BUTTON ZA PUMP ELF 10 ILI MAFUTA YAINGIE YENYEWE BILA YEYE KUPRESS LOCK YA PUMP IKIFIKA ELF 10 ITAJIKATA YENYEWE. lakini kama utamwacha yeye mwenyewe anacontrol lock ya pump kwa kidole huku anangalia pump ifike elf 10 ujue atakuibia tu.na saa zingine huwa wana press kile kibutton cha kutolea mafuta mara anachia mara anabonyeza maana yake zile namba zinakwenda haraka anaposimamisha meter inakimbia huku mafuta hayatoki
 
Hizo Petrol Station za ajabu ajabu huwa sijazagi mafuta labda itokee gari imenizimikia karibu na hizo sheli. Kwa sasa sheli za uhakika ni Oryx na Total zimekaa ki proffessional zaidi ila kwengine ambako napaamini ni Lake Oil!
Hii michezo ipo petrol station moja ipo tabata sheli kituo after kwa bibi.....

Pale ukizubaa unaachwa feri....

Wengine wapo pale kituo after external kabla hujafika mwananchi upande wa kuelekea buguruni ni wapigaji hataree ...
 
NAWAFUNDISHENI DAWA MOJA TU MUITUMIE HUWEZI KUIBIWA.UKIFIKA KITUO CHOCHOTE CHA MAFUTA KABLA HAJAANZA KUKUWEKEA MAFUTA.MFANO UNAWEKA YA ELFU 10 MWAMBIE AKUBONYEZEE PALE KWENYE BUTTON ZA PUMP ELF 10 ILI MAFUTA YAINGIE YENYEWE BILA YEYE KUPRESS LOCK YA PUMP IKIFIKA ELF 10 ITAJIKATA YENYEWE. lakini kama utamwacha yeye mwenyewe anacontrol lock ya pump kwa kidole huku anangalia pump ifike elf 10 ujue atakuibia tu.na saa zingine huwa wana press kile kibutton cha kutolea mafuta mara anachia mara anabonyeza maana yake zile namba zinakwenda haraka anaposimamisha huku mafuta hatoki
Kama nia yake ni kukuibia si lazima mtalumbana tu 😂
 
Huwa ni hivi anapokuja mtu wa boda boda akaweka mafuta ya elfu 5 ile handle inarudishwa sehemu yake lakini sio kamili ile pini inayokata namba inakuwa bado ipo mbali kama vile imeegeshwa tu.

Tatizo laki hapo mmiliki wa kituo anapata hasara ya umeme maana yake ile pump itakuwa ina endelea kuunguruma mda wote mota inazunguka inakula umeme.

wanafanya hivyo kwa kuwa kituo chao magari mara kwa mara yana kuja. Pili jitahidi kusoma risiti yako inasoma kiwango cha pesa na lita sawasawa
... thanks. Nimeelewa. Ni muhimu ku-confirm meter reading kabla mafuta hayajaanza kuingia kwenye tank.
 
Kuna namna wanaitegesha haifiki mwisho na kuruhusu kutoa risiti, wale binadamu wa mbinu sana, nami nilidhani nawasingizia ila nimekuja kugundua wameshagundua kuwa kuna namna ule mkonga ukiutegesha bila kuufikisha mwisho basi haita-clear zile digits pale kwenye meter reading na risiti haitoki.
Kwahio akiunyanyua anaendelea alipoishia mwenzio 😂
 
Habari za majukumu wanajamii,

Habari hii ni kupata uzoefu zaidi, kutahadharishana na kuwekana sawa wakati huu mgumu wa uchumi wa kati.

Nimekutana na matukio mawili kwa nyakati tofauti ya kuibiwa na wahudumu wanaotoa huduma ya kuweka mafuta katika kituo kimoja cha mafuta cha TOTAL kilichopo Oysterbay (pale ambapo kuna vituo pacha katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na mataa ya kwenye makutano ya kuelekea St. Peter, kile kilichopo upande wa FAO, upande ambao kuna JANGID BUILDING).

Mara ya kwanza nilimgundua muhudumu kuwa ameanza kunijazia mafuta hali ya kuwa kwenye pampu kulikuwa kunasomeka Tshs 5,000 ambayo inaonekana alimuwekea mteja aliepita na hakutoa risiti, nikamueleza alichofanya na akakiri kosa lake na kuniwekea mafuta yangu ya Tshs. 5,000 nikaridhika na kimoyomoyo nikasema kuwa haya ni matokeo ya malipo duni kutoka kwa waajiri na ugumu wa maisha, mara ya pili leo (ambayo imenilazimu kuandika uzi huu mrefu), muhudumu kama kawaida kanifanyia ujanja wa kuniita pampu ya mbele halafu baadae akabadili mawazo na kuniambia nisogee nyuma ili aniwekee kutokea pampu ya nyuma (kumbe hii ilikuwa janja yake ya kunifanya nisiweze kusoma vema pale kwenye pampu).

Nami kwa haraka haraka nikakumbuka nilichofanywa mara ya kwanza, nikashuka kwenye gari na kuwahi kusoma kwenye pampu, nikakuta keshaanza kuweka mafuta na kwa sekunde kama 5 tayari pampu imeshafika Tshs 12,000, nikamwambia dada najua umeanzia kwenye elfu 10, akataka kubisha na kuwa mkali, nikamwambia ntakuharibia kazi yako kwa sababu ya Tshs. 10,000 naomba uniwekee mafuta yangu kama pesa niliyokupa. Akataharuki na kuniwekea mafuta yangu yote kulingana na pesa niliyompatia, kwahiyo kwenye pampu ikasoma Tshs 10,000 zaidi ya ile pesa niliyompa aweke mafuta na risiti nikapata ikiwa na Tshs. 10,000 zaidi.

SOMO KWA WAMILIKI WA KITUO
Tafadhali sana wamiliki wa vituo hivi, siwaingilii kwenye biashara yenu ila ni vema kuwashauri kwa ustawi wa biashara yenu: Wale wahudumu sio waaminifu, fanyeni uchunguzi wenu na mkibaini hilo chukueni hatua stahiki, kwa sababu haya wanayoyafanya yatawaharibia biashara zenu na kuleta mdororo. Walipeni vizuri, wapeni mazingira mazuri ya kazi, hakikisheni mnaweka mashine nzuri zinazosomeka kwa ufasaha bila shida.

USHAURI KWA WATUMIAJI WA HUDUMA HII
Tuwe makini wakati wa kuwekewa mafuta, tuhakiki kuwa namba zote kwenye display ya pampu zinaanzia sifuri (zero) kwenye Lita na Kiasi cha pesa. Ikiwezekana tusikubali kuwekewa mafuta mpaka tushuke na kuhakiki kuwa pampu inasomeka vema na inaonesha inaanzia sifuri. Tusiwaamini wahudumu, nao ni binadamu, wanaingiwa na majaribu na vishawishi. Kuna mbinu nyingi za udanganyi kwenye hizi pampu tushirikishane ili tupambane na kuumizana huku ambako hakuna sababu. Tumuogope Mungu na kusema ukweli wakati wote, ikiwezekana unapokutana na uovu kama huu ukomeshe kwa njia yoyote inayowezekana ili kuwaokoa wengine na udhalimu huo.

Ahsanteni sana
Mkuu sisi haya maswahibu hayatukuti, sisi wazee wa vidumu!! Yaani wese la buku kumi kumi haibi hata mia...anaanzaje kwanza!!
 
Hizo Petrol Station za ajabu ajabu huwa sijazagi mafuta labda itokee gari imenizimikia karibu na hizo sheli. Kwa sasa sheli za uhakika ni Oryx na Total zimekaa ki proffessional zaidi ila kwengine ambako napaamini ni Lake Oil!
Sio kweli kaka labda unaziamini kwa kuwa hazina wizi.ila kwa ubora wa mafuta na kuifanya engine yako idumu ni vituo viwili tu. Kwanza kabisa PUMA ukiikosa puma basi nenda TOTAL
 
Hii michezo ipo petrol station moja ipo tabata sheli kituo after kwa bibi.....

Pale ukizubaa unaachwa feri....

Wengine wapo pale kituo after external kabla hujafika mwananchi upande wa kuelekea buguruni ni wapigaji hataree ...

Una maanisha Victoria Petrol Station iliyopo pala kituo kinaitwa Garage? Njia panda kwenda Makuburi?
 
Back
Top Bottom