Wizi wa wahudumu wa kwenye vituo vya kujaza mafuta


Hatari na nusu.

Kwa hiyo kuna uwezekano pia wa kupewa risiti isiyo ya kwako?
 
Hii nilishapigwa Segera pale kuna kakituo mshenzi😂😂😂 mafuta ya 20K sikufika nayo Mombo yameshakata halafu highway ambako gari inakula vizuri😝😝😝 matusi niliyomtukana yule mshenzi dereva wangu alikuwa anakufa mbavu maana nilisema nijazie tu ili nimalizie safari 😁 gauge ikishuka sana economy inapungua
 
Kuna siku nilimsingizia muhudumu hapo kaniibia mafuta kumbe gauge yangu ina tabia za ajabu. Baadae nikagundua hakuniibia ilibidi siku ingine nirudi nimuombe samahani.
Mimi iliwahi kunitokea,ameweka mafuta gauge yangu haikuamka ikawa inasoma zero,nikamshukia nikawasha moto vibaya kuwa hakuingiza mafuta,yule dada akasema ngoja aingize tena labda pump ina shida,wakati naondoka ilikuwa imenyanyuka kidogo sana,nikawa naondoka huku maneno yananitoka kuwa ni wezi sana wale wahudumu,ilipofika kama km 1 hivi gauge ikapanda mara mbili ya kipimo cha kwanza,nikabakia naona aibu mimi...
 

Asante sana kwa nondo Boss
 
Hela za kutafuta kihalali hazitoshi. Ukisikia kujiongeza ndiyo huko.

Tatizo ni pale mtu unagundua kwamba pale fulani kanipiga. Wapo wanaojenga kwa pesa za sheli.

Maisha ni kupigana na kupiga ndiyo huko uonavyo
Kaka tatizo sisi tunaozipata kwa kuungua jua na kunyeshewa mvua tuna hasira sana, ingekuwa zinakuja kwa ulaini wala isingekuwa tatizo, ingekuwa ni kugawana neema tu, lakini sasa jinsi tuzipatavyo ni mtihani ndio maana tuna hasira sana!
 
Mafuta hayawezi kuuzwa bila mashine ya risiti kurekodi. Ndo mana huwezi hata cku moja kumharibia kazi pump attendant kwa kumchongea kwa manager kwasababu manager anajua anaibiwa ni mteja sio boss
 
Hatari na nusu.

Kwa hiyo kuna uwezekano pia wa kupewa risiti isiyo ya kwako?

ilitoka risiti ya 3,000 lakini wanajua wengi hatunaga muda wa kusoma au hata kuchukuwa hizo risiti. Wanajiaminigi sana... nahisi kwa mtindo huu wengi wanapigwa
 

Na ukifika anakupokea kwa tabasamu na masalamu ya kukuzuga! Ukishaondoka huko mbele ya safari hata ukigundua umeibiwa inakuwa ngumu sana kwako kurudi kuanzisha ligi!!! Cha kuzingatia ukiingia pale angalia kilichokupeleka na utagundua janja janja zao
 
Hii style nimepigwa jana Bp ya Sinza super star .....pia ilitoka bodaboda nikafatia mm bahati mbaya sikuangalia.Nimekuja kugundua leo asubuh.Ipo cku yake atakanyaga waya...atajuta siku hyo.

Sent from my Infinix X571 using JamiiForums mobile app
 
Huwa wanaitegesha tu ukija wanakupa maneno mazuri na porojo ukizubaa wanaliunga zipo sana hizo.
 
Huwa wanaitegesha tu ukija wanakupa maneno mazuri na porojo ukizubaa wanaliunga zipo sana hizo.
... nikiingia sheli macho breki ya kwanza kwenye meter reading; nakuwa interested sana kujua aliyetangulia kanunua lita ngapi (sijui kwanini). Then nashusha kioo huwa salamu zao siitikiagi natoa order ya kiasi nachohitaji na kwa kutaja kabisa aina ya mafuta (mf. weka petroli ya elfu 30) huku macho yamekomalia kwenye reading na kuhakikisha ananyanyua handle sahihi (petro vs diesel); meter imeanzia 0000 na kaingiza kiasi sahihi.

Ukihangaika na mawigi sijui misambwanda uko kwenye mazingira hatarishi ya kuibiwa.
 
Hujui kitu nyamaza
.
 
Ndugu yangu, naomba tutafutane, twende pamoja pale na tukawahoji walioniibia kwa style hiyo watupe uzoefu, najua yaweza kuwa ngumu kupata ushirikiano, ila nakuhakikishia mimi ntawapa hata pesa ya kula waweze kutupitisha kwenye uzoefu huo.
Mkuu unaweza kukuta huyo jamaa ndo hao hao wezi wa hapo kituoni ndiyo maana Kakomaaa [emoji23] [emoji23]
 
Hizo Petrol Station za ajabu ajabu huwa sijazagi mafuta labda itokee gari imenizimikia karibu na hizo sheli. Kwa sasa sheli za uhakika ni Oryx na Total zimekaa ki proffessional zaidi ila kwengine ambako napaamini ni Lake Oil!
Mie Moro huwa najazia TOTAL pale Msamvu, hakuna janja janja kabisa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…