Wolper anusurika Kupigwa Risasi Kituo cha Mafuta

Huyu Wolper nilikua namchukulia kama laini-laini, kumbe anaweza akamudu multiple attacks kimtindo, manake mpaka mtoto wa kiume akimbilie silaha ya moto, hali ilikua tete!
 
Huyu Wolper nilikua namchukulia kama laini-laini, kumbe anaweza akamudu multiple attacks kimtindo, manake mpaka mtoto wa kiume akimbilie silaha ya moto, hali ilikua tete!
Walaini wakiwa mbele ya kamera.

Ila behinde the scene ni wagumu balaa.
 
Mi mwenye kwenye Altezza yangu siwezi kuweka mafuta ya kimasikini hivyo. Mafuta ya 20,000? Not me.
 
Huo mchezo nilikuwa nachezewa sana sheli ya apo kinondoni. Kila nikienda posta kurudi lazma niweke elfu20 pale. Nikajiuliza ivi hii gari consumption yake imekuwa jini? Nikawa nawekea pale sheli ya national audit pale. Ndio nikagundua alaaa kumbe nishaibiwa sana. Nikasahau taa nyekundu. Kweli baadhi ya sheli staff wao sio wazuri aisee.
 
..Pole mdada. 90% ya vituo vya mafuta ni wezi. Kuna vituo vichache sana kam oryx ndiyo wa kweli na mafuta yao hayana magumashi.
 
Wolper is as realist as late Tupac was, while other artists are acting their lives Wolper is living it.
 
Hahahahahaa ilikua imepungua mafuta? halafu ukafika mbele ikazimika? haahahahahahaaaa haya bhana
 
Mi mwenye kwenye Altezza yangu siwezi kuweka mafuta ya kimasikini hivyo. Mafuta ya 20,000? Not me.


We mama una kwere wewe, pengine hata baiskeli huna humu unajifanya huwezi kuweka mafuta ya elfu 20.
 
Reactions: ora
Pole yake ndio maana mimi huwa naweka kwenye kidumu kisha ndio naenda kuweka kwenye gari, siwaamini hao wafanyakazi hata kidogo ni wezi balaa.

Wakiona mtu anakuja na kidumu wanakasirika sana, baadhi ya wahudumu vituoni ni wezi balaa hasa nyakati za usiku, mwanzo nilifikiri wanaume ndio wenye tabia hii chafu lakini siku hizi hata wanawake/wasichana wamekwisha ingia kwenye wizi huo.

Usiku chunga sana, wakati mwingine kituo kinaweza kuwa hakina mafuta lakini wahudunu na walinzi wanakaa hapo kuzuga tu, ukija wanajidai wanakuwekea mafuta kumbe kwenye kisima hakuna kitu!!

Siku moja niliwahi kwenda kituo cha mafuta pale Tabata relini, zamani OilCom - hawa walikuwa ni wezi kweli kweli, niliingia kituoni nikamkuta binti na mlinzi , mwazo nilishituka kidogo baada ya kuona hakuna gari hata moja inajaza mafuta pale, binti alikurupuka kutoka alipokuwa amejibanza akanielekeza kwenye mojawapo ya pumps nikampatia elfu thelathini za kujaza mafuta, baadae nikaondoka kupitia barabara ya Dampo kwenda Magomeni - kufika Kigogo nikaona gauge haijapanda kufikia kiwango ninacho kijua mimi, nikalazimika kwenda kituo cha Mafuta cha Magomeni kujaza mengine tena!!!

Kesho yake asubuhi nikawahi kituo cha Mafuta cha Tabata na kwenda kulalamika kwa mmiliki wa kituo, nilishangaa mmiliki alipo niambia kwamba kituo hicho kilishiwa mafuta kabla ya saa kumi na mbili jioni, hivyo usiku wote kituo kilikuwa hakina mafuta, mmiliki alikuwa muungwana akanirudishia pesa zangu na kuwashughulikia wahusika wa kisa hicho. Hivyo kuweni makini sana mnapokuwa vituoni.
 
wakati akitoka nduki lazima atakuwa alijamba,
chezea risasi.
 
Itakuwa wanalipwa mshahara mdogo sana nn?
Kwann zile tubu za mafuta hazionyeshi mafuta yanavyopita
 
Ndio maana najaza TOTAL au PUMA tu. Makampun mengine ni longolongo
 
Staa mzima unatembelea gari mpaka linazima mafuta mfyuuu
 
Mngeanika wazi jina la hicho kituo cha mafuta ili watu wengine wasije wakakutana na huo "ukibaka" ebo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…