Wolper anusurika Kupigwa Risasi Kituo cha Mafuta

Usupar star wa bongo kweli hauna mana. Mbwembe zote insta mafuta ya nyekundu mbili. Ndio mana walimuibia. Mana kutwa wanajisifu wanatumia milioni kupaka rangi kucha.
 
hyo n script ya bongo movie ama ni nini. mbona sielewi maana gari lilizima mwishoni akarudi, mlinzi kakoki bunduki wolper katoka nduki na gari mbona haina mashiko.😀😀.
gari kuzima alirudije
 
Tumewahi kuibiwaa Morogo pale Mafuta Lita 40 hakika sitakuja kusahau na mimi ndo nilipewa hela za kulipia mafuta Kwenye Mashine ilionekana zimeingia Lita 40 lakini hata haziwa hivyoo daaaaa wahudumu wa Sheli wa kibongo ni pasua kichwaaa Sitakaa tena kujaza mafuta Pale!!!! Wolper alikuwa sawa tuu
 
Vituo vingi hapa mjini ndio mchezo wao huo,mtu anakuja wa bodaboda anamuwekea elfu 5 ile pampu haizimwi ule mkono unakuwa umeegeshwa tu sasa unakuja na wewe na baby walker yako niwekee ya elfu 10 hapo,inashikwa ile paipu anatupia mashine inaendelea kuhesabu toka elfu 5 inakuja kustop elfu 10 ukitazama unaona elfu 10 kweli kumbe umewekewa elfu 5,
mara nyingi ukiona sehemu kuna harakati nyingi kituoni basi jua hapo ndio wanapigwa mno watu,
muhimu ukitaka kuweka mafuta usiwe na haraka mwache awashe ianze 0 halafu mwambie kamua wese,
kwa vituo vya Dar 75% huo mchezo upo mno mno
 
Mnatembelea magari msiyoyaweza kuyahudumia, unatembea na gari geji empty mpaka inakula mafuta ya reserve, halafu unawaka Na kielfu ishirini chako.
 
Naomba kufahamu iwapo mafuta hamna kwenye kisima kama pump inaweza kuwashwa na mtu akafanya kama amekuuzia mafuta kumbe umelipia hewa maana inawezekana kutokujua kwangu nimeshalizwa sana.
Zaidi sana nitajuaje kama mafuta hamna kwenye kisima ili nisiingizwe mkenge?
Asante!
 
Source bongo movie? Aaah ni nilijua kweli, kumbe ni muendelezo wa upuuzi wao. Sasa gari lililozima kwa kuishiwa mafuta alirudi nalo vipi sheli, alilibeba? Kisha baada ya kuona kimenuka akatoka tena nduki na gari, mafuta ya 20000? Fuel gauge ya mark X ni mdebwedo hata ishindwe kusoma kuwa kuna wese limeongezwa? Ama huyu Wolper ni kilaza kiasi ashindwe faham km anaibiwa hadi aende, arudi?
 

Kitu cha kwanza ukifika kwenye kituo cha mafuta ukakuta hakuna gari wala pikipiki inajaza mafuta au unakuta pump zote hakuna muhudumu hisipo kuwa pump moja ukiona hivyo shituka kidogo, pili ukiona muhudumu ana wasi wasi kidogo au anatumia muda mchache kukuwekea mafuta nenda mbele kidogo subiri zima gari alafu iwashe tena kwa kawaida gauge lazima ipande labda kama ina itirafu. All in all kisaikolojia ni rahisi kutambua mtu mjanja kwenye vituo vya mafuta.
 

Mbano amesema aliazimwa mafuta na msamalia mwema.
 
Anha basi sawa ana haki ila ajifunze kusoma gauge
 
Iyo sheli itakua ile ya africana pembeni ya nmb na ndio tabia yao. Ata mimi kuna siku mafuta ya elfu 40 haya kuchukua round
 
Ndio maana nchi nyingine, unalipa hela, unajaza mafuta mwenyewe Kisha unajikata. Sometimes gass station ziko zenyewe Tu wala hakuna longolongo. Huu ujamaa unaleta wizi Tu. Kijisehemu kidogo wafanyakazi kibao matokeo ndo hayo
 
raha ya JF kila member ana ndinga yake. Hata mimi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…