Leo umeongea point.
Zamani huko yashawahi kunikuta.
Mimi kuna jamaa yangu mno rafiki wa siku nyingi, tulishirikiana kibiashara. Mtaji ukakua vizuri tu. Jamaa akapata mpenzi akaona aoe kabisa. Baada ya hapo mapichapicha yakaanza. Mwanamke alianza kuleta MANENO maneno mengi jamaa yangu wa siku nyingi mno anageuka anaaza kunituhumu mambo ya ajabu, mke wake ananituhumu wizi mara wizi, siku nyingine ananisakizia ninamtaka kimapenzi (ni mzuri mweupe na ana tako kubwa). Mimi na jamaa yangu tulikuwa na utaratibu wa kukuza mtaji tokea kwenye faida. Mwanamke wake akaanza kuwa anataka hela moja kwa moja toka kwenye biashara kwa ajili ya matumizi yake na mtoto. Pesa akipata ni kujiremba , nguo na kununua mawigi. Nikikataa kumpa hela ananizushia namtaka. Mara ananidanganya mme wake kamtuma nimpe hela. Nikimpigia jamaa yangu anasema yeye hajamtuma, halafu mwanamke ananiruka anasema hajataka hela, anaanzisha varangati. Ikabidi niwe na daftari la mahesabu mwanamke akawa anakula faida na mtaji wa upande wa jamaa wangu ambaye ni mume wake, jamaa yangu nikimuelezea anakuwa haelewi ananiona mimi mbaya, mke wake anaanzisha varangati. Siku zikaenda Nilijicontrol hasira, Siku moja uvumilivu ulinishinda, mwanamke akaanza varangati kama kawaida, nilimwasha kibao kimoja heavy tu mpaka wigi likaruka juu yeye akaanguka chini. Watu wakaja kunishikilia ikawa vurugu kweli kweli.
Jamaa yangu akaja akataka kuleta vurugu, watu wakamshikilia, mimi na rafiki yangu wa siku nyingi tukaaa maadui rasmi. Mwanamke akasema nilikuwa namtaka mara aseme nilikuwa nataka kumbaka.
Jamaa yangu wa siku nyingi akanichukulia RB polisi. Nikalala ndani. Nilivyotoka tukaamua tugawane biashara. Kila mtu achukue chake. Tukaanza kupiga hesabu kumbe mwanamke amekula hela nyingi mno toka kwenye biashara. Nilitoka na 70% jamaa yangu 30%. Kila mtu akajitegemea.
Mimi mpaka leo nipo. Ila kule kwa jamaa yangu kiliumana zaidi. Mwanamke wake aliifilisi biashara ikafa kabisa halafu mwanamke ni spender anapenda lavish lifestyle nguo kali, nywele, viatu simu kali. Waliishia kugombana na jamaa wangu walishaachana na huyo mwanamke wake. Ni single mother huko. Jamaa yangu alikuja kupiga magoti kuniomba msamaha ofisini kwangu. Jamaa anasema huyo mwanamke kamfilisi na kamletea mgogoro na kila mtu kuanzia na mimi rafiki wake wa kibiashara, majirani, ndugu zake. Jamaa yangu alikuwa anazungumza machozi yanamlengalenga. Nilimboost kidogo angalau asife njaa.
Omba Mungu akuepushe na Mwanamke