World Bank to officially declare Tanzania a Middle Income Country (MIC) on July 01, 2020

Ujui nguvu ya tz wewe na historia yetu hao EPA watatii tu kwa tz
 
Unaweza kunitajia ni nchi gani au taasisi gani nyingine imetusamehe madeni apart from Brazil?

Sababu unaongea as if kila siku tunasamehewa madeni.
 
Sawa kichaa
Yaani wewe huwa hauna akili kabisa, ulibadilishana na katambuga

Uzuri una haki na uhuru wa kusema chochote kunihusu ilimradi usinidhuru tu. Umetumia haki yako vizuri kabisa
 
Nakutafuta nikuunganishe na wasiojulikana so get ready.

Dah! Usihangaike kunitafuta wewe niambie unataka taarifa gani zinazonihusu na nizipeleke wapi mkuu wangu.

Usihangaike sana kunitafuta.
 
Dah yaani ukisikia ile ukisimama nchale, ukichuchumaa nchale na ukikaa nchale ndo hii inawatokea wakenya muda huu. Yaani wameleta uzi wa kutusifia ila wanavopewa za uso ni kama uzi ni wa kutuponda😀😆😀
 

Kwanza kabisa sio jukumu lao wale kuhakikisha nchi imesimama, wao husaidia tu kupiga tafu mara moja moja, lakini ni jukumu la uongozi wa kila nchi kupambana na kuhakikisha wao wanasimama, ni kama uwe na mdogo wako chapombe, miaka inaenda yupo 35 hajaoa, hajipangi, kila mara moja moja huwa unamkwamua, mara unapigiwa simu kakamatwa na mapolisi akiwa kwenye gongo, mara katia mdada wa watu mimba mara hiki mara kile.
Utaendelea kumsaidia mara moja moja lakini sio jukumu lako kuhakikisha amesimama, inapaswa ianze naye mwenyewe.
 
Watamwelewa tu Magu wetu!
 

Mideni tuliyonayo ni ya kusaidiwa mara mojamoja?
Ikiwa dogo wako hasikiii na hajatulia kuendelea kumpa mikopo ukijuafika unatupa pesa kwa shimo isiyojaa si upunguani? Vinginevyo unataka ujiko tu kwamba huyu namsaidia sana lakini hasaidiki.

Na hapa naongelea wote, WB, IMF, Mashirika yote ya Umoja wa Mataifa n.k. mfano nilioutoa hapo juu niliuliza kwa shirika mojawapo la Umoja wa mataifa wanaojipambanua kusaidia nchi masikini kujikwamua.

Unakumbuka walivyochukizwa na kitendo cha Rais wa Venezuela marehem Hugo Chaves aliposema hahitaji tena hawa jamaa kwa kuwa hana mikopo, hahitaji msaada wa kimaendeleo?

Umewahi kuona watu wanaotaka kukusaidia kwa dhati na wanania ujikwamue hawafurahii anapotokea mtu mwingine anataka akusaidie au akukopeshe?

Yaani katika ule mfano umeutoa awali, wewe unamsaidia dogo wako, mie nikitaka kuja kumpa msaada au kumkopesha unamind kwamba wewe utaonekana si chochote kwake.
Ina maana hapo wewe ile kujimwambafy tu kwamba unampiga tafu dogo na umwendeshe unavyotaka kwa maslahi flani ndio unachohitaji.
 

Kwanza kabisa mfano niliotolea wa dogo, sikua nahusisha mikopo, hapo nilikua nazungumza kuhusu misaada ya kawaida. Na misaada yenyewe namtolea kwa masharti, kwamba aache upumbavu ajipange, na ndio nitakua na wasiwasi nikisikia kuna mtu mwingine anampa misaada, maana huyo huko hampi masharti, akiagiza anapewa tu mihela na mtu mwingine asiyempa masharti, dogo anakua teja hajipangi.

Suala la mikopo pia linakuja na masharti yake, kama sio mtu wa kulipa wala hata senti yangu hapati. Kwanza mimi sipendi kuwapa ndugu mikopo maana husababisha mahusiano kuharibika ikija kwenye kudai.

Dunia hii sio rahisi kwa taifa lolote kuendelea bila mikopo, hata mataifa matajiri yanakopa, ila kwa Afrika mikopo tunayokopa mara nyingi huwa tunaitumia vibaya wenyewe na kulaumu wanaotupea. Unakuta serikali inakopa halafu inatumia kitita kikubwa cha hizo hela kununua viongozi wa upinzani na kuminya demokrasia kwenye nchi, na wakisemwa wanapiga makelele kwamba wao ni taifa huru wasiingiliwe.
 
Kweli kabisa unachosema, au unakuta nchi nyingine zinakopa lakini hizo ela badala zitumike kwenye maendeleo unakuta viongozi wanazitumia kwa mambo yao binafsi unakuta wanaspend one bilion kwenye chai, na kuishia kutengeneza miradi mibovu, huku nchi ikiendeshwa kwa fedha za mikopo na misaada lakini utasikia wakiwaambia raia wao nchi ipo vizuri sababu wana gdp kubwa
 

Hehehe!!! Ungeacha watu wazima waendelee kujadili mambo ya kiutu uzima, wewe subiri muda wa kutupiana madongo utapewa haki yako kwenye level ya uwezo wako. Kwa sasa nawapuuza nyie timu CCM JF brigade aka mataga mpaka nipate nafasi ya kuwajibu, niliwaambia mtafute mmoja wenu awawakilishe maana sina muda wa kujibu kila mmoja wenu mnaponishukia kwa povu, inabidi nawapuuza bila hata kusoma mnaponi-quote.
Ningekua nalipwa ningewapelekesha sana nyie maana uwezo wenu wa kufikiri ni mdogo sana, kwa sasa kwaheri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…