World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Mkuu usimsahau macherano, ile block aliyompiga Roben dakika ya 90+, kipa alikua keshapotea.

Unajua kuna jambo moja kwa teamGermany. Wanataja kuwa hamna superstar wa kiwango cha Messi au Ronaldo de Lima ila kwamba wote ni wa kiwango kizuri cha kati kwamba ukimkaba Muller ujue atafunga Kroos au Khedira au Klose au Ghotze au Shurrle kwamba wote ni world class players ambao wote ni wafunguji. Hoja hii aliifafanua vema mchambuz wa soka dr Liki( sorry spelling za jina). Akasema pia upande unaoamini hilo hapo juu ni kweli lakini sifa hizo za Ujerumani wanazo pia Argentina kwamba achilia mbali Lionel Messi, unaweza kufungwa na Di Maria au Higuan au Aguero na nyota wengine. Kimsingi game ya Jumapili ni 50%/50%, ukijichanganya unakula goli moja kwa bila shughuli imeisha. Kila timu itakuwa na nidhamu, penetration pasi hazitazaa matunda, njia zote zitafungwa. Magoli ni counter attack, long pass, adhabu na kona au penalt ndani ya dk90/120 au shootout!
 
Kuna mwana JF yupo mitaa ya Kimara Temboni!Njooni hapa mkabala na stand mpya Bar inaitwa Mashineni tujadili soka!Njooni tujadili soka jamani
 
Kati ya watu wanaoimbea Argentina mabaya ni Pele. Unajua kwa nini? Kwa sababu kama Argentina watashinda ina maana Messi atakuwa naye amepata kombe la dunia sawa na yeye(Pele) na Maradono. Ikumbukwe Messi analinganishwa na hawa wakongwe wawili. Akipata hili kombe hakika atakuwa amewafunika Pele na Maradona.
 
Mpira katika standard yake anastahili German ubingwa

Mpira katika maajabu yake basi Argentina atashinda

I wish German wabebe kombe
 
Kitu gani kinakuashiria kama Germany anamfunga Argentina?Kuifunga Brazil ya Benard na Fred au?Mbona walisumbuka sana kwa Ghana,Algeria,USA na France?

Messi anaimaliza mechi hii dakika ya 45

wajerumani walikuwa na hofu na ghana, algeria kwa hiyo hawakucheza kwa confidence walicheza kwa tahadhari zaidi kuepuka kashfa ya kufungwa na timu ya africa..

Ghana hawaku-take advantage ya uoga wa german. Wachezaji wengi wa hii timu ya ghana walikuwemo kwenye vikosi vyao vya U21 ambavyo vilifanya vizuri sana kwenye WC ya U21, German wanatambua hilo.

Algeria waliwafunga German zamani, wakati huo German walikuwa na timu kali mno, kwa hiyo algeria walijua kuwafunga german inawezekana hivyo walikuwa na confidence na ile mechi algeria alicheza vuzuri kuliko mechi zote, na german walijua kwanba kufungwa na algeria inawezekana. Ukumbuke pia mpira ni psychological sometimes.

Kuhusu France: Defence ya France ukiangalia vizuri wanavyocheza sio rahisi hivyo kupenya, wanajipanga vizuri sana kwenye ku-defend, ingawa individually watu wanawadharau. Kama france wangekuwa na mfungaji mwingine wa kueleweka zaidi ya Benzema german wangeweza kutolewa.

Argentina ni wazuri isipokuwa wanaonekana nguvu zao kubwa zipo kwa messi , di maria na higuain. Wakati German nguvu zao zipo kwa wachezaji wao 11 wanaokuwepo uwanjani.

Nionavyo mimi, uchezaji wa argentina, brazil, colombia, chile, costarika unafanana. Sasa tusubiri tuone hiyo jumapili.

Messi hatokuwa na kazi rahisi kama unavyofikiria.
 

Mkuu ebu nikumbushe nyakati za mimi msimbazi kushangilia "yeboyebo"......hakuna kitu km hicho,na subirikesho akitandikwa Argentina kutakuwa na samba nchi nzima Brazil....kiasi watasahau 7-1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…