World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Naamini safari haijaisha, ni mapema mno kusema hivyo. Kimsingi kufungwa 5-1 kwa timu kama Spain ni pigo kubwa. Lakini tukizungumzia umri, hata wale Waholanzi wengi umri wao sio vijana kama utakavyodhania. Mpira uliwakataa Spaniard jana na Dutch uliwakubali, hilo tu ndo pekee ambalo naweza kusema.

...not true brother waholanzi ni makinda yote isipokuwa van,babu na snaider ambao pia bado wananguvu na kasi,wengine wote hawajafikisha hata mechi 50 za timu ya taifa. Kwa spain karibia wote wanazaidi ya mechi 100 wakiongozwa casilas mwenye mechi 150. So spain wengi wazee na kurudi kwenye gemu itakuwa kazi sana kwao maana kipigo cha jana lazima kimewatibua na kuvuruga kambi yao,lawama na kunyoosheana vidole kutawagharimu sana na ndo safari imewadia kama ilivyokuwa kwa wafaransa...
 
...naamini man united wamepata dawa ya kuipiga barca...
 
Kuhusu cameroon au spain

Cameroon kufungwa wakati kajitahidi kwa saa zima bila ruhusu goal.
Spain nimefurahi maana wangeshinda wangeongea sana leo nao wapate raha ya kufungwa
 
Hata ufunguzi sijaona kilichonifurahisha.south walijitahd sana na ilikuwa nzuri na yenye kuvutia

Akuna cha zaidi brazil..shamra shamra za south ilikua ni usipime..culture na natural thngs vilitawala.nmemis kelel za mavuvuzela
 
Naamini safari haijaisha, ni mapema mno kusema hivyo. Kimsingi kufungwa 5-1 kwa timu kama Spain ni pigo kubwa. Lakini tukizungumzia umri, hata wale Waholanzi wengi umri wao sio vijana kama utakavyodhania. Mpira uliwakataa Spaniard jana na Dutch uliwakubali, hilo tu ndo pekee ambalo naweza kusema.

Nakuunga mkono!
Pia ikumbukwe, kule Afrika Kusini, Hispania walifungwa mechi ya kwanza 1-0 na Uswiss, timu ambayo watu hawakutegemea ingeifunga Hispania. Bado mapema sana, na Hispania bado ni moja ya timu zinazotegemewa kuchukua ndoo msimu huu lisha ya hiyo dhoruba!
 
Si umeona wanaume wanatandaza mpira mtu kachapika 5 brazili yako wanauweza ule mziki? umewaona chile lakin? bado wanaume wengine,italy,ujeruman,uruguai,argentina mbona patachimbikasafari hii spaini ndo tumeanza kuwaaga hivyo kwa africa safari ya cameroon inaandaliwa
 
Naombea timu zifuatazo zisionje kabisa fainali na ikiwezekana hata nusu fainali:
1. Brazil (japo watabebwa)
2. Spain (wanajidai sana tena wana masifa mno)
3. Portugal
(kama no.6 hapo chini)
4. England (kama no.2 hapo juu)
5. Cameroon (hawawezi)
6. Ivory Coast (wataponzwa na wachezaji mashuhuri)
 
Jaslaws umenchekesha sana,dah
sawa wamepata dawa ya kuifunga barcelona lakini watakutana wapi?wakati manure ni mamotherhouse kazi yao kulinda nyumba wakati mababa wamekwenda kutafuta
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom