Tutamkumbuka kwa mengi sana aliyotutendea Hayati JPM
Biashara ya dawa za kulevya ilishamiri sana nchini, alipoingia Jpm biashara ikakomeshwa haswa.
Wimbi la ujambazi na uvamizi wa vituo vya polisi na kupora silaha aliukomesha mara moja ikiwemo hata ugaidi wa kule Kibiti
Reports za CAG enzi hizo ilikuwa kila mwaka lazima ioneshe Serikali inavyopoteza mapato kwa kulipa watumishi hewa, alipoingia JPM alishughulika na hilo ipasavyo
Ameanzisha mifumo ya ukusanyaji kodi kwa kupitia ulipaji wa control number ambayo imeimarisha sana namna nzuri ya kukusanya na kudhibiti uvujaji wa mapato.
Alijitoa muhanga kudhibiti utoroshaji wa madini yetu, ambapo makampuni yalikuwa yakitorosha na hvyo Serikali kukosa kodi
Sekta ya miundombinu imeimarika sana ktk awamu yake, tumeshuhudia ujenzi wa barabara kiwango cha lami mitaani na barabara kuu za kuonganisha mikoa, Wilaya na vijiji
Sekta ya Afya nako tumeshuhudia ujenzi wa vituo vingi vya afya na kuimarisha usambazaji wa madawa na vifaa tiba
Enzi zile za miaka nyuma tulishuhudia mpaka Twiga wakitoroshwa kwenye ndege, tembo wakiuawa, ikafikia hatua mpaka ujio wa Rais wa China nchini ukiingia kwenye kashfa ya kuondoka na pembe za ndovu.
Ila alipoingia jembe Magufuli haya yote yalibaki historia
Pamoja na madhaifu yake machache lakini kiukweli MAGUFULI amepiga kazi, ameonesha ujasiri wa hali ya juu ktk kushughulikia changamoto ambazo tuliona ni ndoto kutatuliwa, ameonesha nia na uzalendo wa kupambania kulinda rasilimali za nchi ili ziifaidishe nchi
RIP JPM