Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Jack tatizo alikua ana tamaa sana, yeye angewazuga hata kidogo.

Mtu baba yake asipate urithi hata kidogo eti alipata kwa mama yao, ngumu sana aisee.

Ni bora hata angewagana nao nusu kwa nusu, ila pamoja na yote kuwa na wale watoto wadogo hawezi kusahaulika

Mwanakutaka mwanakulipata

Sasa watoto watasomeshwa na yeye atapewa kinachotakiwa kupewa kwa mjane kisheria

Akisusa wenzie wanakula
 
Wosia uliandikwa marehemu akiwa katika hali ya kutoweza kuwa na maamuzi sahihi (mgonjwa)
Hakuna mgonjwa anayeweza kuratibu na kuandika wosia wa kiwango chenye weredi na uhakika kwa kiwango kile. Tuache masihara, ule ni wosia wa mtu mwenye akili timamu na akili kubwa sana.
Tuseme tu, wosia alioandika Mengi akiwa na akili timamu umekataliwa na Mahakama.
 
Hakuna mgonjwa anayeweza kuratibu na kuandika wosia wa kiwango chenye weredi na uhakika kwa kiwango kile. Tuache masihara, ule ni wosia wa mtu mwenye akili timamu na akili kubwa sana.
Tuseme tu, wosia alioandika Mengi akiwa na akili timamu umekataliwa na Mahakama.

Inawezekana pia uliandikwa yeye akapelekewa kutia saini tuu
 
1. Kuwa msimamizi wa mirathi haimaanishi 100% lazima u benefit na mali za marehemu

Unaweza kuwa msimamizi wa mirathi lakini kwenye mgao usipate chochote.

2. Kazi ya msimamizi wa mirathi ni kuisaidia mahakama kutambua mali zote za marehemu ili izigawe kwa kufuata taratibu za kisheria

3. Hii hukumu ni ya msingi sana kwa wale wanaodhani kuwa WOSIA ni final and conclusive
Pale ambapo wosia unaonekana una kasoro kama huu mahakama inautupilia mbali

4. Dakika za mwisho mzee alikuwa sio yeye, akaunti za WhatsApp, instagram zilifunguliwa bidada akajifanya mzee amekuwa kijana ghafla eti ni yeye alikuwa ana post.
 
Mahakama kuu yatupilia mbali wosia wa marehemu Reginald Mengi na kumchagua mtoto wa marehemu Abdiel Mengi na kaka wa marehemu Benjamin Mengi kuwa wasimamazi wa mirathi

Maamuzi hayo yamekuja baada ya mahakama kujiridhisha pasi shaka kwamba wosia huo uliandikwa marehemu akiwa hayuko sawa kiafya, kuna mali ambazo zimejumuishwa kwenye wosia huo kimakosa kwani sio za marehemu peke yake, na pia wosio huo umewanyima watoto wengine halali wa marehemu haki yao

Waschana wadogo kuolewa na mtu mzima mwenye mali zake sio dhambi ila mnapoolewa mkumbuke kumtunza sana huyo mume pamoja na mali zake. Pia muache tamaa inayopelekea kujenga uadui na watu wa karibu na marehemu maana matokeo yake ndio haya pale mume anapofariki

Hapa ndio Jacky ataukumbuka ule usemi wa wahenga usemao - Kisicho rizki hakiliki!
Hapo wosia uliandaliwa kidijitali, kuorodhesha mali ambazo sio za marehemu ndiko kulikowaponza hao walio tengeneza wosia feki
 
Back
Top Bottom