Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Dar es Salaam imetoa uamuzi kuwa watoto wa Marehemu Reginald Mengi;-Abdiel na Benjamin Mengi kuwa wasimamizi wa mirathi ya mali alizoacha marehemu baba yao (Reginald Mengi). Katika uamuzi huo, mahakama imeagiza usimamizi na mgawanyo wa mirathi uanze mara moja.
-
Akisoma hukumu hiyo yenye kurasa 72 mnamo Mei 18/2021 Jaji Mlyambina alisema kuwa wosia wa mwisho wa Marehemu Dkt. Mengi ulioandikwa Agosti 17,2017 haukuzingatia misingi ya kisheria ya uandishi wa wosia.
-
Katika shauri hilo watoto wa marehemu Dkt. Mengi walikuwa wakipinga wosia uliodaiwa kuachwa na Marehemu baba yao kwa madai kwamba wosia huo haukufungwa ‘sealed’ na saini iliyopo kwenye wosia huo ni tofauti na sahihi zingine za Marehemu na pia kwa wakati huo baba yao hakuwa na uwezo wa kuandika kutokana na matatizo makubwa ya kiafya aliyokuwa nayo tangu mwaka 2016.
-
Aidha watoto hao walidai kuwa wosia uliwabagua na urithi wote aliachiwa mkewe mpya na watoto mapacha na hivyo wosia huo ulikuwa kinyume na sheria sababu uliwabagua watoto bila sababu za msingi na za kisheria.
Kuna Mambo huwa yanashangaza Sana 🤣🤣

Yaani kijana wa kiume aoe na kupata watoto wake halafu atajirike na kuendelea na UKWASI mpaka uzee wake ,Kisha atokee mwanamke(mke) mpya huko uzeeni ARITHISHWE NA KUTEULIWA KUWA MSIMAMIZI WA MALI NA URITHI WA HUYO MUMEWE MZEE 🤣🤣🤣🤣

Ha ha ha ha maisha hayawezi kufanywa RAHISI namna hiyo ha ha ha ha

Duuuuh kweli Kuna watu huhusudu "MTELEZO WA GANDA LA NDIZI" 🤣🤣
 
Kuna Mambo huwa yanashangaza Sana [emoji1787][emoji1787]

Yaani kijana wa kiume aoe na kupata watoto wake halafu atajirike na kuendelea na UKWASI mpaka uzee wake ,Kisha atokee mwanamke(mke) mpya huko uzeeni ARITHISHWE NA KUTEULIWA KUWA MSIMAMIZI WA MALI NA URITHI WA HUYO MUMEWE MZEE [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Ha ha ha ha maisha hayawezi kufanywa RAHISI namna hiyo ha ha ha ha

Duuuuh kweli Kuna watu huhusudu "MTELEZO WA GANDA LA NDIZI" [emoji1787][emoji1787]
Alitaka arithi kila kitu na ndomaana aliandika wosia fake. Safi sana
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Dar es Salaam imetoa uamuzi kuwa watoto wa Marehemu Reginald Mengi;-Abdiel na Benjamin Mengi kuwa wasimamizi wa mirathi ya mali alizoacha marehemu baba yao (Reginald Mengi). Katika uamuzi huo, mahakama imeagiza usimamizi na mgawanyo wa mirathi uanze mara moja....
Na wewe danga la mwendazake umepewa urithi wako?
 
Back
Top Bottom