Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Kwa akili tu zakawaida ilionekana wazi huyo mwanamke ni msanii na alikua ana nia mbaya na mali za huyo mzee.ningeshangaa kama hao wamachame wangeamua kumkalia kimya akajirithisha mali zote mwenyewe kisa tu alikua anampanulia mzee wawatu.wanawake wakati mwingine sio viumbe wazuri.Tuishi nao kwa akili.
 
Kweli kabisa.Wanawake wengi ni wasanii sana.wakati mother angu amefariki kuna mother mmoja alijisogeza sana kwa mzee,akawa anajipitisha pitisha sana kwakujifanya anamjali sana dingi.sasa dingi sababu ya upweke nikaona ameanza kumbonyeza yule mother kimtindo.badae yule mother akawa anamlazimisha dingi waweke mahusiano yao wazi alafu wafunge ndoa.Dingi akaja kutuambia eti nimeona siwezi kukaa mwenyewe nataka kuoa tukamtolea uvivu akawa mkali.maana tuliwaza mzee mwenyewe visukari na presha vinamtafuna kila siku ata kama ni kubonyeza akibonyeza kimoja anakua hoi wiki nzima.nikamfwata yule mother nikamwambia asije akalogwa akajifanya hatujui nia yake kwa mzee wetu.mbona yule mama alikata miguu.Kwahiyo kuna kipindi wanaume tunashikwa upofu tusijue nia za wanawake zetu.unaweza kudhani unapendwa kumbe unahesabiwa siku.tuishi nao kwa akili.
 
Mengi ana mtoto anaitwa benjamini??
 
Hawa jirani zetu wana mambo kwa kweli yaani alitaka kuwatosa kabisa wale watoto angejua angejitoa kabisa kwenye mambo ya mirathi ili ndugu wa Mengi wamfikilie vizuri ila alivyokwenda anaweza pewa buku mbili na maisha yakaendelea...
 
Marehemu alifanya maamuzi kwa kutumia kichwa kidogo...acha sharia ifuate mkondo wake

Sheria ichukue vipi mkondo kwa mali ya mtu? Wasia wa marehemu ulitakiwa uhushimiwe, hata kaa kuna wengine inageonekanwa kama wameonewa lakini mwenye mali daima ndie mwenye maamuzi.
 
Wewe jinga suala la migogoro ya mali za maremu si wachagga tu hata makabila mengi kuna migogoro mingi tu.
 
Mali ya mke wa kwanza walishagawana. Na walishapewa watoto makubwa,uridhi wa Mama yao. Wanadai ni mali zilizoachwa na baba wagawane. Na Mzee Mengi alishagawa mali hizo kwa watoto wake wengine, wale wadogo.
Mali za mke wa mengi unazozisema ni shares tu za mke katika makampuni yao ndiyo walirithi watoto. Shares za mengi ndiyo hizo zenye utata, eti zote apewe jackie! Kwa lipi? Alikuwepo wakati mercy na reginald wanaazisha hizo kampuni? Halafu watoto wa mengi wasiambulie kitu? Haiwezekani. jackie kazikuta hizo mali hivyo hazimhusu. Ndiyo maana kashindwa kesi. Eti mtu akicontest hiyo will apewe shs 1000!!!! We umeona wapi mtu anaandika wosia kama huo???? jackie mhuni tu gold digger. Hata yeye hana akili. Mtu anadeny watoto wake urithi yeye anaona sawa tu? Naona akili yake haina akili!!!! Mtu mwenye akili timamu huwezi kuandika wosia wa kihuni kama ule anbao jackie anadai kaandika mengi. Atakuwa hakuwa na akili timamu wakati anaandika kama kweli aliandika yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…