Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Tena mauno umkatie mtu mwenye umri wa baba yake. Bibi yangu aliniambia pesa kuitoa mfukoni mwa mwenzio iwe mfukoni mwako si shughuli ndogo.
Alizuga kuanzisha biashara ya furniture, Amorrette akawa anahonga mpaka Forbes wanamtangaza kwenye exhibitions za kibiashara anaenda Dubai kumbe zilikuwa mbwembwe tu.

Dunia ina maigizo sana. Ndio maana inashauriwa, kutotamani maisha mtu.

Kila mtu kabarikiwa kuliko anavyodhani vyovyote alivyo.


 
Case Ya Mirathi ya ya Dr. Reginald Mengi: Former Miss Tanzania Jackline Ntuyabaliwe adondokea pua kwa Mara Ya nane tena katika Rufaa

View attachment 1791249
View attachment 1790872

Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Dar es Salaam imetoa uamuzi kuwa watoto wa Marehemu Reginald Mengi;-Abdiel na Benjamin Mengi kuwa wasimamizi wa mirathi ya mali alizoacha marehemu baba yao (Reginald Mengi). Katika uamuzi huo, mahakama imeagiza usimamizi na mgawanyo wa mirathi uanze mara moja.

Akisoma hukumu hiyo yenye kurasa 72 mnamo Mei 18/2021 Jaji Mlyambina alisema kuwa wosia wa mwisho wa Marehemu Dkt. Mengi ulioandikwa Agosti 17,2017 haukuzingatia misingi ya kisheria ya uandishi wa wosia.

Katika shauri hilo watoto wa marehemu Dkt. Mengi walikuwa wakipinga wosia uliodaiwa kuachwa na Marehemu baba yao kwa madai kwamba wosia huo haukufungwa ‘sealed’ na saini iliyopo kwenye wosia huo ni tofauti na sahihi zingine za Marehemu na pia kwa wakati huo baba yao hakuwa na uwezo wa kuandika kutokana na matatizo makubwa ya kiafya aliyokuwa nayo tangu mwaka 2016.

Aidha watoto hao walidai kuwa wosia uliwabagua na urithi wote aliachiwa mkewe mpya na watoto mapacha na hivyo wosia huo ulikuwa kinyume na sheria sababu uliwabagua watoto bila sababu za msingi na za kisheria.
Wata appeal , ngoja tuone. Huyo Ntulabaliye alikuja kurithi mali, maana katika hali ya kawaid huwezi kulipenda lizee la uri huo kama hana mali. Kuna driving force ilimleta pale. Uzinzi mbaya na lizee likaingia mkenge!
 
Huyo Jack ni msanii tu
Alidhani mali ya mchaga inapotea kizembe hivyo?
Bora angeandika nusu kwa nusu,lakini kila kitu kajiandika yeye!
 
Dah kulamba 100% ya urithi hata watoto wa primary level wanaweza kususpect kuwa something is fishy about the whole thing.
Afu bila aibu eti "Atakayekata rufaa mahakamani na kushinda, apewe tshs buku moja" ... Yaani mwendazake aliamua kabisa kuipangia mahakama....???

Matusi mengine ni bora uitwe kuku asiyevaa viatu...

Jamaa wangeamua kufanya autopsy unaweza kukuta haka kaJaklini kalimdedisha mzee wa watu mara tu baada ya kuiweka will fake kwenye sidiria yake...
 
kama hujui kiswahili, Title umeandiakje na umeipata wapi
Aiseee acha kumpa stress huyu Dada za makasiriko.Kwani tatizo Ni Nini so nenda kwa Mange au Google au huko huko mahakamani? Imekuwa kesi sasa
 
Hapo Jack ajindae kukaa chini ya mila zetu za kichaga. Atapata tunachoona kinafaa kumsaidia na sio more.
Sisi ndio WACHAGA TAIFA TEULE TANZANIA MZIMA.
Wasukuma fools mpoooo.
 
Hakuna mgonjwa anayeweza kuratibu na kuandika wosia wa kiwango chenye weredi na uhakika kwa kiwango kile. Tuache masihara, ule ni wosia wa mtu mwenye akili timamu na akili kubwa sana.
Tuseme tu, wosia alioandika Mengi akiwa na akili timamu umekataliwa na Mahakama.
Hakuwa Yeye ulichapishwa na wanasheria kanjanja we uliona Ni mwandiko Wake?
 
Hakuna mgonjwa anayeweza kuratibu na kuandika wosia wa kiwango chenye weredi na uhakika kwa kiwango kile. Tuache masihara, ule ni wosia wa mtu mwenye akili timamu na akili kubwa sana.
Tuseme tu, wosia alioandika Mengi akiwa na akili timamu umekataliwa na Mahakama.
Kwamba hata wakienda mahakamani wapewe buku
Hii sio akili ya kawaida
 
Back
Top Bottom