Kwa maelezo yako sioni haja ya kukueleza historia ya maendeleo ya mwanadamu(karne hizi 17 -21). Maana unaamini wanadamu wa siku hizi akili zao ni ndooogo mno kiasi kwamba chochote kizuri au advanced ni Product ya Hao Viumbe wako.
Unafikia mahitimisho ya ajabu kabisa na ambayo hata sijayasema na sijui ni kwanini uko hivi.Unashindwa kabisa ku stick kwenye kile ninachokisema na matokeo yake unaibuka na mahitimishi ya ajabu ajabu tu...
Wapi nimesema "chochote kizuri ni cha advanced being"?
Mimi kusema kuwa kwa kiwango kikubwa maendeleo na sayansi tunayoijua ni matokeo ya viumbe hawa simaanishi kwamba binadamu ni zuzu kiasi hicho,unasomaje maandiko yangu aisee?
Point yangu ya msingi ni kwamba haya unayoyaona siyo yote ni production ya akili ya binadamu wa kawaida,hii kauli unaielewa lakini?
Sasa hata shetani mwenyewe anaweza kukushangaa. Kwa nini Shetani atafute intermediate beings wakati anajeshi kubwa la Malaika zake waovu ambao idadi yao ni kubwa saaana mbali kabisa na idadi ya wandamu.
Ukumbuke alifukuzwa mbinguni: Ufunuo12:4 na 1/3 ya maraika wote wakati maraika idadi yao ni kubwa mno tena hawahesabiki (Daniel7:10, waebrania 12:22).
Unataka hili jeshi lote la Shetani lifanye nini kwa mfano?
Shetani anahitaji nini?
Nakuuliza haya maana hata sielewi mantiki ya hiki ulichokiandika hapa,ukifafanua huenda nitakuelewa....
Ukisema wamefungwa unakoswa uhalali wa kuwepo hao viumbe.
Moja,sijasema mimi kuwa wamefungwa bali ni Mungu mwenyewe kupitia maandiko ambayo nilishakupa...
Mbili,Kwanini uhalali wa kuwepo hawa viumbe ukosekane? Kwani baada ya kukosea huyu Shetani alifungwa hapo hapo?
Pili Turudie matokeo ya dhambi;
1: Utazaa kwa uchungu
2:Utakula kwa jasho
Haya siyo matokeo ya dhani bali haya ni adhabu baada ya kukosea.Matokeo ya dhambi ni sisi kupokwa mamlaka ambayo tulipewa na Mungu ambayo sasa anayo Shetani...
Tofautisha matokeo ya dhambi na adhabu ya dhambi....
3:Na tokeo kubwa kabisa ni KIFO(Kwa ufupi hili ndio tokeo ambalo tunashare wote sawa adam NA SISI),
Hapana,hili nalo siyo tokeo la dhambi bali ni matokeo ya kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya.Binadamu hakuumwa na mwili wa ku withstand ujuzi wa mema na mabaya na ndiyo maana anakufa leo.Ili aweze kuishi milele huku akijua mema na mabaya alitakiwa ale tena tunda lingine ambalo ni la uzima na hili Mungu alilizuia na kumfukuza mwanadamu kwenye bustani ya Eden...
Ni sawa na wewe ulibebeshe gari mzigo mkubwa zaidi ya uwezo wake wa kuubeba.Gari lile litaharibika kwa namna mbali mbali.Inawezekana chesis ikavunjika kwa mfano.Kuvunjika kwa kifaa hiki kwenye gari ni matokeo ya gari kuwa dhaifu kuhimili uzito wa mzigo ambao gari hilo lilibebeshwa.On the other hand binadamu naye ni hivyo hivyo,hakuwa na uwezo wa kuhimili kujua mabaya na mema na matokeo yake ni kuharibika kwa mwili wake na kusababisha kifo,hatukuumbwa kuweza kuhimili jambo hili mkuu...
Kwa hiyo kifo ni matokeo ya kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya....
Ni kweli tuliathirika kiasi ila siamini kama Dhambi ilipunguza idadi ya Brain Cells kwenye kichwa cha mwanadamu.
Ndio maana kila zama ya mwanadamu kila mwanadamu aliyejishughulisha alikuwa zaidi ya wenzake.
Nilikuambia kwamba tangu binadamu akosee mambo yalibadilika kabisa...
1;Kwanza unapaswa ujue kwamba binadamu hakuumbwa na maarifa ya kujenga majengo,kugundua nguo au mengine yoyote yale ndio maana kabla ya kukosea alikuwa uchi na hakuona kama jambo hilo ni tatizo na hakuishi kwenye nyumba yoyote maana halikuwa hitaji lake,haya mambo yalikuja baadaye baada ya kukosea na kwasababu hii Mungu ndiyo akawa anampa mwanadamu maarifa kutokana na mahitaji yake lakini Mungu amekuwa specific kwenye mambo haya kama maandiko ambayo umekuwa ukinipa huko juu ambayo Mungu amekuwa akisema amewapa wanadamu akili au uwezo wa kufanya hiki na kile lakini huyu mwanadamu hakuwa hivyo kutokea mwanzo...
Lakini pamoja na hayo,ubora wa mwanadamu kuanzia akili hadi mwili umekuwa ukipungua kadiri siku zinavyokwenda.Kukupa mfano rahisi kabisa ni kwamba,ukiangalia tu kwenye mazingira yako ya shughuli za mwanadamu utaona ushahidi wa haya....
Angalia hata muziki kwa mfano,muziki wa kipindi cha nyuma unaonekana bora kabisa kuliko wa sasa.Angalua hawa wanaomaliza chuo leo,angalia uwezo wa michezo mbali mbali,kwa sisi ambao tunaangalia soka tunaliona hili maana siku hizi ni kama hakuna kabisa vipaji ukilinganisha tu na miaka ya juzi juzi hapa ya 2000...
Nini kinasababisha yote haya?
Watu wanaendelea tu kuwa wajinga na hili halijaanza leo bali tangu anguko la mwanadamu.Nina mifano mingi sana lakini huenda hiyo ikakusaidia kuelewa angalau ninachokisema....
Kuhusu Uwezo wa Kiakili ni Suala la Lifestyle na Chakula.
Mfano hai kwenye bibilia SOMA DANIEL MOJA KUNA JARIBIO LILIFANYWA AMBALO UKILIANGALIA LINAHAFIFISHA KABISA HOJA YAKO.
Daniel, Meshack, Shedrack na abednego walitakiwa kula vizuri ili pamoja na wenye busara wengine wa Mesopotamia na sehemu nyingine duniani. Wao Wakaigomea ile MENYU ya mfalme. Wakaomba wapewe nafaka,Maji,Matunga (Live foods). Walipokuja kujaribiwa walikuwa na Uwezo mkubwa mara kumi ya wale wengine mkuu.
Kwanza naomba ujue kwamba uwezo wa Danieli ulikuwa ni kutoka kwa Mungu moja kwa moja kwasababu maalum...
Pili;Ni kweli kwamba vyakula vinamfanya mtu awe na afya nzuri ya akili,lakini kuna kitu inaonekana hukijui mkuu.Ni kwamba baada tu ya dhambi kuingia duniani ardhi nayo ililaaniwa.Hii ina maana kwamba vyakula navyo vinaendelea kufifia ubora wake,kile ambacho chakula kilikuwa kikiupa ubongo wakati ule wa Adamu siyo kile kile ambacho kinaupa ubongo wako leo...
Haya ni mambo ambayo yapo wazi kabisa na ukiyatazama yanaeleweka.Kipindi cha nyuma wakati niko kijijini kwa mfano,nakumbuka tulikuwa tukilima mahindi na yalikuwa yanazaa mahindi makubwa sana na kuanzia mahindi matatu hadi manne bila kutumia mbegu feki za kisasa lakini leo hii hakuna kabisa.Huu ni mfano wa kawaida kabisa ambao kila mtu anaweza kuuona.Hili lipo wazi kabisa mkuu,afya ya ubongo najua inategemea unachokula lakini hiki nacho kinafifia kutokana na ardhi nayo kuendelea kuzeeka na kupoteza rutuba yake kadiri siku zinavyokwenda na ndiyo maana dunia hii inaondolewa kwenye maisha ya baadaye na kuletwa nyingine....
Tena Usijeukajidanganya au kuwadanganya watoto wako (Kama wapo) kuwa hawana akili kwa sababu ya dhambi, na kwasababu wao ni 6000th copy ya adam. Laana haikugusa akili. Ukisema kuongea na wanyama. Mtamo wangu ni kuwa unataka kuhafifisha Uwezo wa kiakili wa kibinadamu ili ukubwishe uwezo wa hao allien ili upate ground ya kupenyezea uzushi huu kuwa aliens wako nyuma ya haya maendeleo kwa sababu sisi hatuna akili.
Mbona haya unayakanusha tu hivi hivi bila hata kusema ni kwa vipi laana haikugusa akili?
Ni akili ipi unayoizungumzia wewe kwanza?
Akili ya kujenga ghorofa au akili ipi?
Kilichotokea kwenye ENLIGHMENT AGE watu waliambiwa maneno kama yako na kuamini ni kasisi tu au kiongozi wa dini ndiye mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kumpangia mwanadamu nini cha kufanya.
Kwanza kwangu mimi hakuna hiki kipindi.Hata kama kilikuwepo na kama nikaimua ku assume kuwa ilikuwa kama unavyosema wewe hili linaeleweka kuwa lilikuwa ninamfaidisha nani.Sasa kwenye hili nani anafaidika?
Swali hili nimekuwa nikikuuliza lakini umekuwa uki skip tu bila hata kulijibu.Hebu nieleze,habari za kuwepo Aliens zinamfaidisha nani?
Watu walipanza kufikiri nje ya box na utando huu uliowekwa na imani. Ndio nata newton alijiuliza kwa nini APPLE lianguke kwenda chini badala ya Juu, Watu wakaanza kutafuta majibu from nature. Jamaa wa uingereza akagundua steam engine ambayo baadae ikaja kuwa pivotal kwa industrial revolution. Hata Benjamin Franklin alipoenda england kikazi akiwa anamiaka 15 vuguvugu alililikuta huko lilimbadili maisha yake na Philadefia mji aliotoka na baadae marekani nzima. Waliamini Radi ni Ni adhabu kutoka kwa Mungu, Ben akagundua ni Charges na Kudesign Thunder arrester na Fire system, Magonjwa mengi mtaani, Akaanzisha Sewage system philadelphia nzima.
Kwa ufupi hiki unachokiona na kukihusudu kiasi cha kusema ni product ya aliens ni matokeo ya hawahawa wanadamu walioanguka dhambini kutumia 1/100000 ya ubongo wao wenye zaidi ya 100 billion cells. Nadhani kwa uwezo huo wa mwanadamu ndio maana mwenye hekima alisema Muhubiri 1:9- Hakuna Jipya chini ya jua.
Hizi hadithi zako zitakuwa na maana kama ukinijibu hoja zangu huko juu lakini tofauti na hapo utakuwa ni kama unasema riwaya ambayo ulikaririshwa tu bila kuwa na ushahidi wowote ule...
Alikuwa na akili sasa anaendelea kuwa mjinga tu....
Mkuu hapa naomba ututake radhi, Bibilia inamzungumzia huyuhuyu mwanadamu unayedhani hana akili yaani makapi ya adamu kiakili Mungu anasema NiMEMFANYA MWANDAMU PUNDE KIDOGO YA MALAIKA (Little Lower than angels). Yaana kimsingi Unamdharirisha na kumdogosha mwanadamu ili upate upenyo wa kuhalalisha story za UFO/ALIEN.
1PSALM 8
what is mankind that you are mindful of them,
human beings that you care for them?
c
5You have made them
a little lower than the angels
and crowned them
f with glory and honor.
6You made them rulers over the works of your hands;
you put everything under their
g feet:
7all flocks and herds,
and the animals of the wild,
8the birds in the sky,
and the fish in the sea,
all that swim the paths of the seas.
9Lord, our Lord,
how majestic is your name in all the earth!
Waebrania/Hebrew 2:7
Umenifanya nicheke kabisa mkuu.....
Haya yanayosemwa hapa context yake ni nini?
Kabla au baada ya dhambi?
Ukijibu hayo nitaelewa kama unasoma Biblia kama gazeti au vinginevyo....