MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,607
- Thread starter
- #221
nimegundua haya madude yamekushika sana mkuu. Yaani vitu ambavyo havina proof. Sikuwahi kutegemea kuwa kuna mtanzania anaamini mambo mepesi kishabiki hivi.Hahahahahaaaaaaaaaaaaaa.......
Mkuu unanifurahisha sana aisee.Nani kasema kuwa Phil Schneider ni mtu wa kwanza kuzungumzia haya mambo? Masuala ya UFOs yapo since B.C huko halafu nije niseme mtu aliyekuja kusema kwenye miaka ya 1990's ndiye wa kwanza?
Hivi hao akina Senetor Barry Goldwater, Lord Hill Norton mkuu kitengo flani British loyal army, Brigedia General Urther Axon.Director ni reliable source namna ipi aisee?
Nilikupa hiyo video kwasababu nilitaka usikilize kutoka kwa mtu ambaye ana wadhifa ambao hutaweza kutilia mashaka kirahisi rahisi tu anachokisema kama unavyotilia mashaka ninayosema mimi hapa kwakuwa hata hunifahamu....
Masuala ya UFOs sijui unataka uyasikie kutoka kwenye vyanzo vipi unavyoviamini.Ungeelewa msingi wa hoja zangu ni kwamba tunadanganywa juu ya uwepo wa hawa viumbe na wenye mamlaka makuu kabisa duniani kwaajili ya faida zao binafsi na kwasababu wao wanahusiana kwa namna moja au nyingine na hawa viumbe wala usingekuwa unataka vyanzo kutoka kwa watu ambao ndiyo wanatudanganya kama unamaanisha vyombo vya habari vikubwa vukubwa kusema au wataalam wenye noble prize waseme....
Unataja watu ambao ni wahusika wa serikali,unarudi kule kule.Kama hujui ni kwamba kuna web nyingi sana za hawa hawa wanaotudanganya ambao wanatoa fake info kupoteza watu.Wale ambao waliasi na baadaye kuuawa ndiyo hutoa ushuhuda unaoshikika....
Unaposema ushahidi usio na shaka kutoka kwa Phil Schneider unakuwa na maana ipi? Yaani kwa mfano hilo "jiwe" ulitaka awape watu wakahakikishe asemacho au ulitaka afanye nini? Hivi unajua ni nini alichokuwa anamaanisha huyu mtu? Unajua ni aina ipi ya maisha alikuwa anaishu huyu jamaa? Unajua ni madhara yapi ambayo aliyapata akiwa kazini akijihusisha na haya masuala?
Hoja zako ni nyepesi sana kwa wale ambao tunajua ni namna gani haya mambo yanaendeshwa lakini kwa watu ambao hawajui wanaweza kuona zina mashiko.Ni ngumu sana kuthibitisha kitu ambacho kwanza ni kinyume cha sheria kuwa nacho halafu ni ngumu kumpa mtu yoyote tu aka verify ili aamini.Mazingira haya ni magumu sana.Mtu alikuwa hadi anahama nyumba tano kwa usiku mmoja ili aendelee kuwa hai unakuja kusema tu hapa "hataki kutoa nafasi kwa wengine kuthibitisha asemacho" utadhani ni mtu tu ana gari halali halafu anasema linakimbia kuliko yote kisha ukahoji sababu ya yeye kutompa mtu mwingine aendeshe kuthibitisha....
Unayohoji yangekuwa ya maana sana kama ingekuwa ni kitu halali tu tunakijadili hapa ambapo tungeweza kwenda kwenye maabara zozote za kisayansi tukathibitisha....
Bado,huwezi kupata majibu ya maswali yako kirahisi hivyo kwa kuangalia video moja....
Eti tuje tujadili ukweli na uongo kwenye maelezo yake.Utatumia nini kusema hiki ni uongo au hiki ni ukweli? Hisia au nini hasa? Una hilo "jiwe" lake ili ukalipime uone ni uongo aliyokuwa akiyasema kulihusu?
Unafurahisha sana aisee...
Tunazungumzia Extraterestrail being wenye uwezo zaidi ya Mara Mia wa Binadamu (Kwa mujibu wa Wanaoamini). Jamaa wanachimba Underground Station tena HAO VIUMBE ETI pamoja na uwezo mliowapa wanamsubiria huyo jamaa aje awapige risasi. Kwa akili ya kijijini kabisa hizo stori hazina mantiki. Ngoja niiandike yote. Eti UFO akampiga na kumkata Vidole Kisha kukimbia. Daa!!! nimeelewa kwa nini hauna ujasiri wa kuyanena haya waziwazi hadi tukupress sana maana unajua hayana Mantiki. Na wengi walishazipuuza hizo stori maana hakuna Uthibitisho na ni za kufirika. Nimegundua tunakazi kubwa sana bado. Na nafikiri haya ni madhara ya kuaminishwa haya mambo ni siri hivyo unajilimit kufikiri. Ni bora sana ungeyaweka kama MYTH au Assumptions ili ikiwa sio kweli iwe safi sasa mkuu unajiaminisha kabisa stori zile daa!!!!