Umekuwa ukisema tu jambo fulani kibiblia linatia mashaka lakini tukija kwenye hiyo biblia mara zote imekula kwako kwenye mjadala huu,sijaona mtazamo wako hata mmoja ambao umekuja kuwa sahihi kwenye mjadala huu.Kwasababu hiyo hata jambo hili nalitilia mashaka kwa asilimia nyingi tu.....
Si hivyo tu,bali hata kwenye Biblia yenyewe kuna ushahidi pia kuwa Suleiman alikuwa mweusi,Yesu alikuwa mweusi n.k...
Kuhusu Wabantu kuwa ni Waisraeli hili nalo kuna maeneo kwenye Biblia linaonesha hivyo....
Mkuu,hili halihusiano moja kwa moja na mada yako,lakini pia ni kweli nimeshajadili jambo hili hapa lakini kwenye mada hizo hukuwepo,nilijadiliana na watu wengine na mkuu
Wickama atakuwa anakumbuka sana jambo hili vizuri sana maana hadi Biblia tuliijadili kule na pia ulikuwepo ushahidi kuonesha hawa wanaoitwa Waisraeli leo siyo wenyewe.....
Sijaona sababu ya kulijadili hili sasa kwakuwa linahitaji maandalizi,tumalize hili la mada yako kisha tutajadili siku nyingine suala hili....