Huyu alikuwa anachimba shimo, tena mita nyingi ardhini kuna jambazi gani ardhini ndio maana nilitoa mfano wa shimo la choo. Huo mfano wa daktari hauko compatible na mada.
Msingi wa hoja yako ni mtu kuingia kwenye eneo la kufanyia kazi ambapo halihusiani na yeye kumiliki silaha.Bahati mbaya kabisa hujaeleza ni kwa vipi huo mfano wangu hauko sawa na ulichokisema....
Unashangaa huyu mtaalam wa miamba kuingia shimoni na silaha mahali ambapo hapaswi kuingia na silaha,je,hospitalini tena kwenye chumba cha kumhudumia mgonjwa ni sawa kuingia na silaha?
Hivi huyu jamaa,tena kwa wadhifa aliokuwa nao,siyo jambo la ajabu kumiliki silaha,wakati anatoka nyumbani kwake kuelekea kazini ni lazima alichukua silaha yake ambayo ni kwaajili ya kujilinda na kufika nayo kazini,kuna ubaya gani kwenda nayo kwenye eneo la kazi? Ulitaka aiache wapi? Ni sawa kuacha silaha yako mahali tu hivi hivi?
Mkuu u nafikiria namna gani?
Hizo stori za huyo jamaa tuziache tu maana zote ni uongo labda kama una source nyingine, kwa sifa unazowapa alliens na hilo tukio havina uhusiana labda ndio maana analyst wengine wanasema alikuwa anaugonjwa wa akili. Hiyo ni Invalid source sio lazima utoe nyingine endelea na tafiti zako mkuu.
Bila hata kueleza ni kivipi ni uongo ushahitimisha kuwa ni uongo,inastaajabisha kabisa....
Ulisema kwamba utakuja kusema kipi ni uongo na kipi ni kweli kwenye maelezo uliyoyaleta, na mimi nikawa nasubiria uchambuzi ambao utakuja kuelezea kwa kina ni kivipi siyo kweli mambo fulani na fulani na kwanini mambo fulani na fulani ni kweli lakini naona umeishia kukanusha tu.Hii ni hatari sana kwa afya ya akili na inaonekana hukuwa na haja ya kufanya ulichosema kuwa utafanya.Nimesikitika sana aisee.....
Sifa ninazowapa aliens ni uongo based on this only siyo? Tena bila hata kusema ni uongo kivipi,interesting.....
Mgonjwa gani wa akili anauawa?Kwanini?
Mgonjwa gani wa akili anawindwa kuuawa kwa matukio zaidi ya 10?
Mgonjwa gani wa akili anafanya kazi serikalini kwenye kitengo maalum kama hiki?
Mkuu vipi aisee?
Aisee....
Mbona unapinga tu bila basic ya unachopinga?
Tueleze pia kwa tafiti zako What happened WW2 na WW1 maana unaweza kusema kombora la masafa la kwanza duniani ( Vergeltungswaffen-2 ) lililootengenezwa na NAZI Scientist
Wernher von Braun, underground huku mashahidi (Jews) walioshiriki kama vibarua hadi leo wapo hai na Musseum ipo utaniambia ni Aliens walishiriki na Hitler. naomba mtazamo wako.
Kwanza nilikushauri kwamba unapotaka mtazamo wangu kuhusu suala fulani ni afadhali ukaniuliza nikakueleza kuliko ku assume halafu ukafanya assumption zako kuwa sahihi wewe mwenyewe...
Pili,kuna ushahidi pia kuwa Hitler na NAZI walikuwa na secret meeting na hawa viumbe na pia walikwenda bara antarctica na hiki ndiyo kilichompeleka Admiral Raymond Byrd askari ambaye alikuwa ni Navy Officer wa jeshi la Marekani kule na alikaa sana kule na kuna mambo alikuja kuyasema baada ya kutoka huko unaweza kuyatafuta na utayapata...
Angalozo;
Usije kuanza kusema tena msinbgi wa ninayoyasema ni huyu askari maji wa ki-Marekani maana wewe namna unavyofikiri unaijua wewe mwenyewe tu.Lakini ishu ya Hitler na Aliens pia ipo unaweza kuitafuta mwenyewe na ukajua....
Pia unaweza kufuatilia na ukajua ni nani aliyekuwa mtaala wa kemikali wa NAZI kipindi kile na aliyesaudua sana kupatikana kwa acid na silaha za kinyama kabisa zilizotumika na NAZI kuua watu Ulaya wakati wa vita vile pamoja na kuhusika kwao na "Hallocast"....
Kuna mengi sana na naona kama hatuwezi kujadili jambo hili mkuu maana mimi na wewe tunayatazama mambo haya kwa namna tofauti sana na naona kama unakataa mambo bila ku reason jambo ambalo linanifanya nisione kama kuna nitakachojifunza kutoka kwako na kama nitapata changamoto nzuri kutoka kwako.....