MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,607
- Thread starter
- #341
It's all true and is about new world order, religion unification for sake of fake peace and unity!! And roman catholism under papacy are match maker and the master mind! But the Bible warns about this,through the Revelation,,!!
Naomba nitoe muhutasari wa bandiko lote hili.Kabla hujaniambia niseme hiki unachonitaka niseme unachopaswa ni kuunganisha ukisemacho na biblical prophecies ndipo uniambie haya.lakini unapodai tu haya madai yako bila kufanya ninachokutaka ufanye ni kupoteza tu muda....
Unatoa madai bila hata kusema ni kivipi unasema hivyo....
Huo mtiririko wa unabii wa Biblia kwenye Danieli 2 unahusiana nini na unachokisema hapa?
Hii sensa ilifanyika dunia nzima mkuu?
Mbona unaongeza chumvi sana?
Pia,haya nayo yanahusiana nini na unachokisema?
Hakuna mahali ambapo Mungu alisema kutakuwa na tofauti ipi ya miaka baina ya ufalme mmoja na mwingine...
Kama kutakuwa na tofauti ya wiki moja au hakutakuwa na tofauti hata ya siku moja baina ya ufalme A na ufalme B hii haimaanishi pia itakuwa hivyo baina ya ufalme B na C au C na D,hili ndilo tatizo kubwa sana kwa ninyi ambao mnauhusisha unabii huu na Rumi....
Moja:Unapaswa uwe makini sana kwenye maswali ninayokuuliza kwasababu sikuulizi kwasababu sijui bali nakuuliza ili nipate ufafanuzi kwako kuhusu suala husika ili nione kama unatumia mantiki au sivyo hivyo usidhani kwamba nauliza kitu nisichokijua...
Mbili:Ishu ya kuhusishwa kwa ufalme wa nne kwenye sanamu ya Danieli 2 na miguu miwili ni assumtion tu na jambo hilo halipo kwenye maandiko.Mungu anapotaka kukitolea kitu maelezo huwa anakuwa wazi,tazama Danieli 2:42,hivyo kwasababu Mungu hakutaja suala la miguu kuhusiana na ufalme ule wa nne basi hili suala la wewe na wenzako mnaokubaliana na hiyo fasiri yenu ya unabii siyo sahihi ni asumption yenu tu na tunawaachia ninyi wenyewe....
Tatu:Kosa kubwa kabisa ambalo huwa mnalifanya wewe na hao wanaokubaliana na hii fasiri ya unabii wenu wa Danieli 7 na 2 ni kudai kwamba Rumi ilianguka mwaka 476 wakati ufalme ulioanguka mwaka huo ni Rumi ya Magharibi tu.Rumi ya mashariki haikuanguka mwaka huo na iliendelea hadi karne ya 13 huko ikaja kuangushwa na Ottoman Empire kule Istanbul Constantinople] hivyo madai yenu hayapo sahihi...
Rumi ya mashariki ilianguka mwaka 1453 soma hapa Byzantine Empire - Wikipedia
Nne:Unabii wa Danieli 7 kuhusu mnyama wa nne na pembe zake unazungumza kinyume na usemacho.Malaika alipokuwa akimpa ufafanuzi Danieli juu ya pembe za mnyama wa nne alisema "hao ni wafalme watakaoinuka kwenye ufalme huo" hakusema "hizo ni falme" zitakazoinuka katika ufalme huo kwa sababu unaposema pembe zile ni nchi unakuwa unamaanisha hizo ni mamlaka ambazo kiunabii ni falme na hazihusiano kabisa na ufalme husika wakati siyo kweli kama unabii unavyosema....
Danieli 7:24
24 Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.
Kwa context ya ufafanuzi huo wa unabii kutoka kwa malaika ni kwamba hao wafalme kumi ndiyo watakuwa wanaongoza ufalme huo wa nne na mmoja ataibuka ambaye atakuwa tofauti na wengine ambapo atawaangusha wafalme watatu na siyo kuobndoa falme tatu kama tafsiri yako inavyosema,kwa maana hii ni kwamba haupo sahihi kabisa mkuu....
Ili twende sawa tutofautane kwa hoja jengefu. Nimetoa Msimamo na Uelewa wangu kuhusu Daniel 2, 7 kuwa ni vitu vinaendana. Msimamo huu ndio ulikuwa msimamo wa waprotestant wote kabla hawajachakachuliwa sasa wakiwemo waldenses, hussites, wycliff, martin luther, john gill, baptist theoregians, tyndale, na wengine wengi na mimi naungana nao mkono pasipo shaka. Ndio maana wao walienda mbali hadi kuziweka sanamu hizo makanisani na viongozi wao akiwemo na kiongozi wa Rumi enzi hizo kaisari. Luther alitamka wazi kabisa kuwa anti christ ni nani.
Picha.
Sasa nikuombe kitu kimoja.
Eleza vyote unavofahamu kuhusu Daniel 2, 7 then nijue naongea na mtu anayeamini nini, naona kama unmarukaruka na kupita pembeni. Pia nitakueleza hata mwanzilishi wa hicho unachoamini maana nimeshapata mwangwi wake na kwa nini aliiweka hivyo.