WW1, WW2 na kinachoendelea sasa Middle east vilipangwa mwaka 1871 kama barua hii ni kweli

WW1, WW2 na kinachoendelea sasa Middle east vilipangwa mwaka 1871 kama barua hii ni kweli

si kweli vita vya dunia vina maana kubwa zaidi ya unavyofikiria kwa ufupi ni ivi Yesu aliwekwa Mfalme wa Ufalme wa Mbinguni mwaka 1914 na shetani alitupwa dunia(ujirani na dunia sio dunian kabisa) matokeo yakuwa nn soma ufunuo 12: 7-12

jw.org/sw
Uongo...
 
Kwanza kuna ushahidi kuwa marais wote wa Marekani wanahusiana kwa maana ya kuwa kwenye bloodline moja,kwanini hii iko hivi?

Ukiacha hilo,kuna muunganiko au bloodline inayowahusisha royal familly na Marais hawa wa Marekani,bado hujaelewa kitu hapo?

Wale Wanefili ni ilikuwa matokeo ya malaika na wanadamu,baadaye waliendelea kuzaliana na kuwa wengi.Kuna tofauti kati ya kizazi cha malaika na wanadamu ambapo ni wanefili na matokeo ya wanefili na wanadamu....

Hapo anazaliwa kiumbe ambaye anakuwa bi ninadamu nusu na nusu kitu kingine na wengi wa namna hii wapo sana tu....
Nawafuatilia sana wewe na Mseza. Hongereni kwa mada hii ya kufikirisha. Nami nina madukuduku yangu na pengine tunaweza kushea mawazo. Inasemekana wanefili ambao ni watoto wa malaika walioasi walikuja na ujuzi wa kila aina na kuwafundisha wanadamu kutengeneza vitu vingi. Hii ni kwa mujibu wa huyo Henoko. Lakini ukitazama kitabu cha kutoka 31:1-6 Musa anapewa maagizo na maelezo toka kwa Mungu.
31: 2 anasema, Angalia nimemwita kwa jina Bezaleli, mwana wa Uri, mwana wa Huri, kabila la Yida
31:3 anaendelea, Nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina

Sasa tunaona nae Mungu kwa upande wake kampa mwanadamu maarifa. Huku tunaambiwa maarifa tunayoyaona ni zao la wanefili. Nini mtazamo wako
 
Ahsante sana kwa swali lako hili...

Kwanza kabisa ni kwamba waliowafundisha na kuwapa wanadamu elimu mbali mbali ni malaika waasi siyo wale machotara wa malaika waasi na binadamu...

Wale machotara wa malaika waasi walileta tafrani kubwa sana kwasababu walikuwa wanawala binadamu,yaani walikuwa wakiwatumia binadamu kama chakula chao..

Malaika waasi waliwapa wanadamu elimu ambayo hawakupaswa kupewa na hili ni kosa kubwa sana na ndiyo maana lilileta matokeo hasi.Mambo kama kutoa mimba,kusoma nyota na mengine ya kufanana na hayo ni elimu iliyoletwa na malaika waasi kwa binadamu....

Binadamu alijua kusoma nyota na kutoa ujauzito miaka 6000 huko iliyopita na siyo juzi kama wengi wanavyodhani....

Elimu ambayo Mungu aliitoa kwa binadamu ni ile ambayo siyo mbaya bali njema,unapoona mahali ambapo Mungu anatoa elimu kwa watu jua kuwa hiyo ni elimu chanya kwa binadamu na hii ni chache sana.Elimu na ujuzi uliotamalaki leo ni matokeo ya elimu iliyotoka kwa malaika waasi na inatumika kwa njia hasi.....
 
Binadamu anatumia uwezo wa akili aliopewa na Mungu tofauti na viumbe wengine wanaotumia silika (instinct). Binadamu ana tabia ya kujiongeza na ndio maana tunafundishwa hivi mashuleni lakini mitihani tunaletewa kwa njia nyingine katika kupata jibu lililokuudiwa. Mathalani leo mtu anatumia simu iliyotengenezwa makusudi kwa mawasiliano, yeye anarekodia na kuhifadhia picha za utupu. Sidhani akili hiyo ni zao la wale malaika waasi bali ni mfano wa yule shetani aliyemjaribu Yesu. Na utashi ulio ndani ya mtu ndio humfanya kuamua njia atakayo kulingana na nguvu ya dhamira yake.
 
Unasema "sidhani akili hiyo ni zao la wale malaika waasi bali ni mfano wa yule shetani aliyemjaribu Yesu"....

Huyo shetani hakuasi?

Hakuwa miongoni mwa hao malaika waasi?
 
"You ever wonder why Jewish people own all the property in America?!!Jay z line in " The O J story" halafu mwisho anamalz kwa kusema Financial freedom!!
Me nina wonder vitu vingi sana Aseeh
Huwa nabaki Dilemma kwamba kivip Historia ya MTU mweusi iandikwe na MTU mweupE??Na kipi haswa kilipelekea mpk afrika tukawa ColoniseD,ni suala LA mapinduzi ya viwanDa km tulivyosoma ama yapo mengi nyuma ya Pazia?..
Ukweli unamuweka MTU huru Japo huwa ni mchungu kumeza na mtamu kutema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni kweli vatican ina play sehemu muhimu. NA IMEPEWA NGUVU YA KUFANYA HIVYO. Lakini sio hiyo peke ILIYOPO inayofanya kazi . Bible imeweka ufunuo wa mtiririko wa hizi nguvu(ufunuo 6) na imezigawa katika makundi makuu7, Manne ya kwanza YANAHUSIKA MPAKA KIPINDI HIKI na zote zinakwenda kuleta hali fulani/mazingira katika hizo nyakati za mwisho kuwepo hayo yalioonyeshwa yatatokea. Nafafanua nguvu hizi kwa ufupi kutoa mwangaza kwa wasiojua
Bible kwenye kitabu cha ufunuo kuna seven(7) seals zimeandikwa.[seal=muhuri] Hizi seals zinaelezea matukia tangu kipindi cha Yesu mpaka vita vya mwisho wa Dunia (Armageddon)
Four(4) seal za mwanzo ni farasi. na ni nguvu fulani za kiroho (unaweza ukasema Horse power za kiroho) kila moja imetolewa maelezo ya ziada katika kitabu (bible) cha Zekalia 6. Na imeeleza zaidi kuwa hizi Nguvu ni Four spirits (roho nne), yaani kila nguvu ni aina flani ya ROHO. Kwa hiyo mtu aliefunikwa na nguvu hizi atasukumwa katika roho yake kufanya kwa nguvu kile roho inataka (mtaelewa tu) mfano kichaa anasumbuliwa na roho ya ukichaa, ipo hivyo. Anaejiua sio yeye ni nguvu fulani inayomuwezeshakufanya hivyo.

Ufunuo 6,
  • Farasi wa kwanza MWEUPE; ROHO YA UKATORIKI, inamuhusisha papa na ukatoriki na namna wanavyoendesha mambo yao. Roho hii imeenea duniani. Hapa inahusu hayo yote Eiyer anatamani kuzungumzia
  • farasi wa pili mwekundu; Roho ya ukomunist na inajitambulisha kwa rangi nyekundu (angalia benera Zao mfano China na Urusi) Roho hii imepewa upanga ambao ni nguvu za kijeshi
  • farasi wa tatu mweusi; Roho ya ubepari. na Zekaria 6.6 anaonyesha roho hii imeelekea kaskazini. Ndio mana nchi za kibepari zipo huko kaskazini (northen hemisphere)
  • Farasi wa nne, kijani iliyopauka (pale green) kwenye biblia tafsiri ya kiswahili wameandika kijivujivu lakini ni kijani iliyopauka kwa tafsiri sahihi. Hii ni Roho ya Uislam na hapa ndipo UISLAM umetambuliwa rasm kwenye bible. Hii roho ndio imefuatwa na umauti na kuzimu. Roho hii imepewa nguvu kutawala robo ya dunia na inaendekeza sana MAUAJI kama njia ya kujieneza. Rangi inayojitambulisha ni hiyo kijani iliyopauka(angalia bendera zao)
Kwa hiyo Hizo nguvu bwana Eiyer unaweza ukaelezea ukatoriki na wataalamu wengine wakaelezea zingine. Wote hao wanafanya maovu kwa viwango vyao, kama kuna anayeonekana na nafuu, basi mbeleni lazima ataleta fujo sana hasa huyo farasi
mwekundu. Kufanana kwa hizo roho nne mpaka zote zikaonyeshwa kwa alama ya farasi ni kwamba, ZINAPOJITOKEZA KWENYE JUMUIYA ZINAJITAMBULISHA NA KUWA NI ZA AMANI NA NZURI, hakuna hata moja itajionyesha ni KATILI, lakini nyumba ya mgongo, uvunguni wanafanya maovu hatari katika kujieneza na kushughulikia wapinzani wao.

Tukirudi kwenye mada; Ni kuwa hata kwenye bible hivi vitu vimeonyeshwa, yaani WWI na WWII ni pale tarumbeta ya kwanza (WWI) na Tarumbeta ya pili (WWII) katika ufunuo.
Fuatilia tarumbeta hizi kwenye ufunuo zilipopulizwa nini kilitokea. Tarumbeta zinaenda mpaka ya saba. Kila moja ikipulizwa ni janga kubwa linatokea duniani.
Incomplete perfection
Wack

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wale wale ambao tunawajadili hapa ndio hao hao walioanzisha harakati za wanawake kudai haki zao.Kwa tafsiri zao ni kwamba mwanamke ni kiumbe ambaye hakuwa akipewa heshima yake na Mungu hivyo Shetani kwa kuwatumia watu hawa ndiyo anataka "kumkomboa" mwanamke kutoka kwenye makucha hayo.....

Lakini,ukweli ni kinyume kabisa.ili waweze kutawala vyema mwanadamu ni hadi pale ambapo watakapoweza kuwa na binadamu lazy wasiojielewa wasioweza ku reason.Kimsingi wanaweza kutumia akili nyingi zaidi kuweza kumtawala lakini hawakuona sababu ya kufanya hivyo wakaamua kutumia akili kidogo tu hapa...

David Rockerfeller alimambia Arron Russo kwamba,baada ya vita ya pili ya dunia wanaume walikufa sana vitani na hata wale ambao hawakuwa vitani waliuawa na vita maana wakati mwingine vita ilipiganwa kwenye makazi ya watu.Kutokana nba wanaume hawa kufa sana kukawa na upungufu wa wafanyakazi hivyo wakalazimika kuanzisha harakati ya kuwafanya wanawake kuingia makazini ili kuziba pengo hilo...

Anaendelea kusema kwamba,walihitaji wawapate watu wakiwa katika hatua zao za kwanza kabisa za ukuaji ili waweze ku shape namna yao ya kufikiri ili wasije kupata tabu wakati watakapotaka kuwa ongoza na kuwatawala,kwasababu hiyo,wanawake wanapokwenda kazini hii itawalazimu wasiwalee watoto wao wao wenyewe hivyo watatafuta wasaidizi.Kwa nchi za Ulaya na Marekani ni watu wachache sana ambao wanaweza kuaford kuwalipa wasaidizi hawa maana ni ghali....

Sheria hizi za kusimamia "haki" za wasaidizi wa ndani ziliwekwa na wao hao hao kwa malengo maalum ambayo utayaelewa kwenye maandishi haya haya....

Kwasababu ni ghali kuwalipa wasaidizi hawa wazazi watalazimika kuwapeleka watoto wao shule za watoto wadogo na vituo vya kulea watoto na huko wameweka watu wao ambao wataendelea kuwatengeneza watoto hawa kwa namna watakayo.David aliendelea kumueleza Risso kwamba,wanapowapata watoto wakiwa wadogo kiasi hiki ambacho ni kuanzia miezi mitatu na kuendelea kwasababu sheria [iliyowekwa na hao hao] ya mwanamke kumhudumia mtoto ni miezi mitatu tu na baada ya hapo anapaswa aende kazini na anakuwa amemaliza likizo yake ya uzazi...

Huyu jamaa aliendelea kumueleza Russo kuwa kwa kufanya hivyo waliweza kumshape mtoto afikiri kwa namna atakayo na leo tunaona matokeo ya jambo hili,unaweza kushangaa vijana wa kuanzia miaka 45 kurudi chini wanafikiri kwa namna ya kufanana kabisa na haya ni matokeo ya jambo hili....

Lakini pamoja na hilo,jamaa alisema kuwa wanawake wakienda kufanya kazi watakuwa wakikatwa kodi ya mapato hivyo kuongeza mapato.....

Kwa maana nyingine hakuna haki za wanawake zinazotafutwa hapa isipokuwa ni mipango mingine tu.Kuna zaidi ya hili kwenye jambo hili lakini nadhani jambo hili linatosha kukata kiu yako na umeridhika nadhani.....
Kuna mambo ambayo always uwa natamani kuyasema dunia ijue ila kila nikitaka kuyasema uwa napatwa na hofu ya ajabu, kuptia bandiko hili nitafanya uchaguzi wa mtu ambae nitampa habari zote then yeye atakuwa anazileta kwenye jukwaa kama hili.

Nb kile unachojua kuhusu ulimwengu uhu ni sawa na tone moja katka ukubwa wa bahari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii mada inafaa sana kuwafungua Waafrika na tutambue kuwa dini zipo ili tutawalike pili elimu tunayopewa ipo Kwa ajili ya kutumwa kuanzia msingi msingi mpaka vyuo na bila Waafrika kujitambua tutabaki watumwa mpaka Dunia itakapo koma ili tutoke hapa lazima turudi zama za mawe tuanzie pale babu zetu walipoishia ndio tutajua tuelekee wapi Kwa rasilimali tulizonazo na pia kuachana kabisa na elimu za kitumwa

Sent using Jamii Forums mobile app
umeandika kwa usahihi kabisa, ila kwa kifupi ni kuwa tukitaka maendeleo ya kweli kwenye nyanja zote tunahitaji kuukumbatia utamaduni wetu na kuachana na mambo ya nnje, ndio maana ya maendeleo endelevu.
 
Kuna mambo ambayo always uwa natamani kuyasema dunia ijue ila kila nikitaka kuyasema uwa napatwa na hofu ya ajabu, kuptia bandiko hili nitafanya uchaguzi wa mtu ambae nitampa habari zote then yeye atakuwa anazileta kwenye jukwaa kama hili.

Nb kile unachojua kuhusu ulimwengu uhu ni sawa na tone moja katka ukubwa wa bahari

Sent using Jamii Forums mobile app
Naelewa sana unachoandik hapa kwakuwa nina uzoefu huu....

Pia,kukaa na mambo napo ni mtihani kweli kweli....
 
Naelewa sana unachoandik hapa kwakuwa nina uzoefu huu....

Pia,kukaa na mambo napo ni mtihani kweli kweli....
Ni kweli kabsa, bahati mbaya sana watu wengi hawaelewi haya mambo hivyo unaitaji kuwa mvumilivu sana maana wapo wanaojifanya wanajua kumbe hawajui kitu kabsa.Nipe muda nitakutafuta pm hakika hautojuta kunifahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kabsa, bahati mbaya sana watu wengi hawaelewi haya mambo hivyo unaitaji kuwa mvumilivu sana maana wapo wanaojifanya wanajua kumbe hawajui kitu kabsa.Nipe muda nitakutafuta pm hakika hautojuta kunifahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili la kujiona wanajua wakati hawajui ni tatizo lingine kubwa kweli kweli na ni changamoto ngumu sana kwa watu kujifunza.Wakati naanza kuyafuatilia haya mambo huku kwetu hayakuwepo kabisa,kuna wakati unajikuta unakaa kimya tu huku ukiwa unaumia tu....

Haya mambo yalipoingia hapa nchini na watu kuyaingilia kwa sifa ndiyo matokeo ya ujuaji usiokuwa na maana,mtu anajua vitu "vya kawaida" lakini anaona anajua mengi sana,ukikosoa unaonekana wewe mjuaji,unajikalia kimya tu...

Karibu sana mkuu unipe maujuzi zaidi....
 
Nitakuja nimeweka alama.

Miamba wawili wapo kazini sasa niwakati wa kuvhukua maujuzi na kuongeza ufahamu.

Thank you msenza mkulu pamoja na ndugu yako.
 
Upapa ni kijisehemu kidogo ambacho ni sehemu ya mpango mkubwa kabisa wa kuutawala ulimwengu chini ya dini moja na mungu mmoja.Dhana ya Mungu mmoja haipo kwenye "Abrahamic religion" pekee bali ipo hata kwa Shetani maana yeye anataka awe ndiyo mungu wa dunia hii na yeye pekee tu....

Mpango wa kuitawala dunia na vilivyomo ulianza ramsi huko mbinguni miaka maelfu mengi yaliyopita pale malaika mmoja mzurisana alipoanzisha harakati za "kumpindua Mungu".Malaika huyu hakupendezwa na mambo mengi ikiwemo namna Mungu alivyokuwa akiendesha mambo yake hivyo akaanzisha "movement" huko mbinguni ya kufanya mapinduzi lakini bahati mbaya alishindwa kabisa baada ya Jemedari mkuu wa majeshi ya Mbinguni,Mikael kumsambaratisha malaika huyo pamoja na jeshi lake...

Malaika huyo wakati wa harakati zake alikuwa akiwashawishi malaika wengine waungane naye na alifanikiwa kuwashawishi robo ya malaika walioko mbinguni na hapo alipoona ameweza kuwashawishi hao aliamua "kulianzisha" lakini alishindwa...

Baada ya kushindwa alitupwa huku duniani lakini aliazimu kuendeleza harakati zake kama za mbinguni za kuwafanya viumbe wengine wamuone Mungu hafai na ni dikteta.Miongoni mwa harakati hizi ni tukio lililobadilisha kabisa maisha na hali ya duniani tukio lililotokea miaka zaidi ya 5500 iliyopita pale Eden baada ya malaika huyo kufanikiwa kumshawishi binadamu kumuasi Mungu....

Kuanzia hapo amekuwa akiendesha harakati zake kupitia njia nyingi na miongoni mwa njia hizo ni kuanzisha utaratibu wa kufanana na ule wa Mungu wa kumuokoa mwanadamu ambao ni dini.Ameanzisha dini nyingi fake na zinazofanana kwa sehemu kubwa na njia aliyoianzisha Mungu kwaajili ya kumuokoa mwanadamu...

Pia,ameanzisha harakati kupitia siasa,elimu n.k,lengo ni kumueweka mwanadamu mbali kabisa na Mungu na miongoni mwa alivyoanzisha ni hiyo taasisi uliyoitaja lakini kuna vitengo vya kiimani kama Freemason,Illuminati,Bohemia group,Roscrucian,Theosophical sociate n.k....

Hizi ni harakati zake katika kufanikisha kazi yake ambayo nimeisema hapo juu lakini hii ni sehemu ndogo sana ya yote haya....
Unaandika mambo kama vile una hakika nayo kabisa ....in short unasema Kanisa Katoliki ni mpango wa shetani ....hii ni kufuru ...hebu nitajie dhehebu au huduma ambayo link yake haijatokea Kanisa Katoliki (sijui kama unanielewa) .....Hata Biblia ni tunda la Kanisa Katoliki ....historia iliyonyooka ya Kanisa ipo ....tuache conspiracy ambazo ni kumpa tu utukufu shetani ....nguvu ya Kanisa Katoliki duniani miaka yote iwe ni kazi ya shetani? Sasa unabii wa Yesu juu ya Kanisa lake ungetimiaje? Au ndio hii kila mtu anaibuka akitafsiri biblia anavyojisikia? ....
 
Back
Top Bottom