WW1, WW2 na kinachoendelea sasa Middle east vilipangwa mwaka 1871 kama barua hii ni kweli

Mambo ya Mungu tusiyajadili na ma conspiracy theories....ni mazito kuliko uwezo wa akili zetu ...tuwe makini ingawa najua kwa hulka ya kibinadamu tutajiona tuko makini ....
 
Nimesoma michango yenu yote nahisi kupotea zaidi,hebu naomba kuuliza tu kwa wajuvi wa mambo.Mungu ndiye kaumba ulimwengu na vyote vilivyopo je kwanini ameruhusu huyu SHETANI amharibie kazi yake aliyoifanya? kumbuka hata shetani kaumbwa na mungu huyuhuyu.WHY asimtupe kwenye ziwa la moto binadamu wakaishi kwa amani.Vinginevyo kuna theory fulani itapata nguvu sana tunakoelekea.
 
Mkuu Eiyer we ni noma your genious mkuu vya mambo aisee nu vizuri kuyafahamu sana

Mseza Mkuu Uko vizuri Sana Mkuu umetupa elemi ya kutosha kama hamtojali basi vitu Kama vitabu hata vijarida kama kuna soft copy muwe mnatuwekea hapa tunapitia angalau tupate kidogo au hata vichwa au jina la kitabu
Nashukuru sàna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hongera kwa kunyooka moja kwa moja kwenye shabaha.
 
Umeweka darasa hauru ila mimi hapa naomba nifunge kwa kusema nachoamini mimi kuwa mtazamo wa kidini siku zote huwa right kuliko mtizamo mwingine wowote bila kupingana.

Hii mingine hugongana sana pia ina ukakasi mwingi sana.
 
Mkuu eiyer na mseza mkulu naona wote mna hoja nzito sana na zote zimekua msaada mkubwa kwetu kuweza kufahamu kiduchu kati ya mengi yaliyo ya siri.
Lakini naona mnashindwa kuelewana sehemu moja tu.
Mseza mkulu anadai kinachoendelea duniani kwa ujumla ikiwemo vita na mipango mingine ya siri ni mpango wa mwanadamu mwenyewe bila nguvu yoyote Ile kutoka nje ya ubinadamu, which is wrong.
Ukweli ni kwamba binadamu ni kama TV tu inayoendeshwa kwa remote control, nyuma ya yote haya Kuna nguvu ya ziada inayoratibu everything na kuhakikisha yanatimia kwa wakati, nae si mwingine ni muovu shetani kupitia mawakala wake, hivyo mseza mkulu sio kweli kwamba binadamu mwenyewe Ndio anapanga hichi kinachoendelea.

Na mkuu eiyer unadai Kuna vitu vinaitwa aliens, UFOs kiuhalisia hakuna vitu kama hivyo ni vitu vya kufikirika na kutengenezwa ili kuwatia hofu wanadamu ili iwe rahisi kwao kusimamisha NWO, kivipi... Aliens wamekua wakizungumziwa sana kwenye vyombo mbali mbali vya habari vikubwa duniani na pia kuandikwa sana kwenye vyanzo mbali mbali vya habari, Kuwa ni viumbe kutoka sayari nyingine na wana uwezo mkubwa sana wa kiakili na teknolojia yao ni ya hali ya juu sana, tunaaminisha haya kupitia movies mbali mbali kutoka Hollywood, yote hii ni kufanya akili zetu zione ni jambo la kawaida kwa viumbe hawa kutoka sayari nyingine, na ya kwamba kumbe duniani hatupo peke yetu!!! Kuna wageni toka sayari nyingine. Lakini ukweli ni kwamba si kweli ni vitu vya kutengenezwa tu, Ndipo hiyo siku itakapofika mpinga kristo atakapokua tayari kuja kuitawala dunia kupitia project ya blue beam light itakayokuwa displayed kwenye anga kutaonekana kama Kuna uvamizi wa hao aliens, na ili dunia tuweze kujikomboa dhidi ya huo uvamizi kutoka sayari nyingine tutalazimishwa kuungana kwa pamoja dunia nzima tuweze kumkabili adui kutoka sayari nyingine, ambapo kwa akili ya kawaida wengi wataona kweli Kuna ulazima wa kuungana ili kumkabili adui ambae kiukweli ni adui "fake" na hapo Ndipo wengi wataingia kwenye mtego wa NWO bila kutegemea na tayari Kuwa under one government, one currency, one religion na siku moja ya kuabudu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji445] [emoji445] [emoji445] [emoji444] [emoji444] only God can judge me[emoji444] [emoji444] [emoji443] [emoji443] [emoji445] [emoji445] [emoji445] [emoji441] [emoji441] RIP 2PAC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaupeo mkubwa sana Nimepata elimu Kubwa sana katika hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu

Naona unanishutumu sana kuwa ninaandika kama vile nina uhakika wakati [kwa mtazamo wako] uhakika sina,hili ni kosa la kwanza kati ya makosa mengi tu kwenye maelezo yako....

Historia ya kanisa Katoliki naijua vizuri sana tu,ninajua kuhusu madhehebu mengine,lakini umenishangaza kwa kudhani kuwa ninadhani kuna dhehebu ambalo halijatokana na kanisa katoliki au kuna dhehebu safi.Mimi kusema shida ya kanisa katoliki hakuyafanyi makanisa au madhehebu mengine kuwa safi,yote yana uchafu wake na ni mbaya kweli kweli hivyo haya mawazo yako siyo sahihi kabisa....

Ninafahamu namna biblia ilivyopatikana,ufahamu wangu haujafungwa,sijaelewa kuwa,kama Kanisa katiloki ndilo lilihusika na upatikanaji wa Biblia ndiyo kunalifanya vipi kutokuwa na makosa jambo ambalo ni kawaida kabisa kwasababu linaongozwa na binadamu.Ninachoelewa mimi ni kwamba,kwakuwa linaongozwa na binadamu lina uchafu wake kama vile ambavyo sehemu yoyote inayoongozwa na binadamu inavyoweza kuwa na uchafu kwasababu ya udhaifu wa kibinadamu....

Nina uhakika na niandikayo wala sibahatishi,kuna mambo inawezekana huyajui kuhusu Kanisa hili lakini kutokuyajua kwako hakuwezi kuyaondoa jambo ambalo ni sawa sawa na mtu wa dhehebu lingine atakaposhindwa kujua ya dhehebu lake,kutokujua huko hakuyaondoi mabaya hayo....
 
 
eiyer
habari hii inatisha! Je kila aingiaye kwenye utawala katika Marekani, Urusi, China na sasa Korea Kaskazini wanazifahamu hizi habari?
 
Mkuu haya mambo niyakufikirisha na ukiwaza kwa makini ni ukweli mtupu lakini wanaochukulia mambo kirahisi hawawezi kuamini.
Ni ukweli kuwa wapo watu wanaondesha dunia na kupanga dunia iende vipi ,pia inavyoonekana hizi secret societies chimbuko lake ni moja au viongozi wao wa juu ni kitu kimoja,kuna sehemu kwenye mabandiko yaliyopita ulisema skulls & bones ni wanajihusisha vyuo,Freemason wanajihusisha na mambo ya imani,je hata haya tunayoyaita ni vitabu vitakatifu tuna uhakika gani kwamba may be ni conspiracy za hao majamaa?iwapo Pindar ni yupo Vatican na kitabu kitakatifu kinachotumika ndo hiki at the same time yeye ni kati ya wakuu wa illuminati.

Ni kweli kwamba kuna vitu binadamu hakupaswa kufahamu lakini akafunuliwa na huyu jamaa mwenye busara,ingawa biblia inasema shetani ni mwongo ila ni kama aliyoeleza kwenye bustani ya eden ni kweli na hajamdaganya mtu maana tunda alilosema kweli ilimfunua ufahamu wa kujua mema na mabaya.

Ukifuatilia hawa watu illuminati na Freemason wanamchanganyiko wa dini mbali mbali na kwenye ceremony initiations biblia ni kati ya vitabu vinavyotumika kufanya viapo kwa wale ambao ni wakristo,na pia ukiangalia hata codes za kupanda madaraja ya degree zao zinasemekana zipo ndani ya biblia,sasa tuamini vipi kwamba hivi vitabu vitakatifu hawajahusika ?isije ikawa ni mwendelezo wa hawa majamaa kutuingiza mkenge
 
Sijajua kama Pindar anapatikana Vatican ila ninafahamu ndiye mkuu wa Illuminati...

Kuhusu vitabu vya dini ni kwamba kuna dini ambazo ni product ya hawa "watu" lakini kuna moja tu ambayo siyo.Jambo hili siyo rahisi moja kwa moja kama wengine wanavyoweza kudhania,ni gumu sana.....

Shetani hakuwa mkweli pale Eden kwa asilimia 100 bali kwa sehemu tu.Lakini pia Mungu hakuwahi kusema kisichokuwepo,alipowaeleza Adam na Hawa matokeo ya ulaji wa tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya ilikuwa ni kweli...

Mungu hakukataa kuwa Adam na Hawa walifumbuliwa macho,lakini Mungu hakutaka wawe hivyo kwasababu hawakuumbwa namna hiyo.Hawakuumbwa kuweza kuhimili uwezo wa kujua meam na mabaya na matokeo yake tunayaona kila uchao.Shetani hakuishia hapo tu bali aliendelea kuwafundisha mengine yaliyosababisha mengi sana na ya hatari.....

Binadamu walifundishwa elimu ya nyota,walifundishwa namna ya kutoa ujauzito,walifundishwa namna ya kutengeneza silaha za moto,walifundishwa elimu ya anga,fizikia na nyingine ambazo binadamu hakupaswa kujua....

Kwenye rituals zao na initiations kuna biblia na vitabu vingine vya dini zingine,kila kitabu kiko pale kwaajili ya kazi maalum na siyo kama wengi wanavyodhani....

Nirahisi sana mtu kuhusisha jambo fulani na kitu kingine lakini kuthibitisha ni suala lingine kabisa mkuu.....
 
Asante cc Eiyer inabid nitafute hiki kitabu
 
Biblia imekuwa kama Keepleft without outlet
 
Bwana wee hawa watu wawil eiyer na mseza mkulu wapo smart sana. Nimefurahishwa sana na kutolewa ujinga kwa kiasi kikubwa na eiyer na hili lisingewezekana bila maswal na mtazamo wa mseza mkulu. Tunameng ya kujifunza kutoka kwenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…