WW1, WW2 na kinachoendelea sasa Middle east vilipangwa mwaka 1871 kama barua hii ni kweli

Mkuu EIYER,shukrani sana kwa uchambuzi wako uliotukuka kuhusu udanganyifu anaofanyiwa binadamu. JF kupitia kwa magwiji kama wewe,juve 2012 na kiranga (angalia mada ya "ijue familia ya rothschild") mmenifumbua macho kwenye mambo ya kiroho. Lakini kiu yangu bado ipo kuhusu hawa "hybrids" wanefili. Je,katika zama hizi tunazoishi bado kuna mwingiliano mpya wa kimwili kati ya binadamu na malaika mwovu au ni ile bloodline ndo inaendelea kuingilia na mwanadamu wa sasa?Kuhusu uwepo wa gharika na uteketezaji wa viumbe vyote isipokuwa walioingia kwenye safina,roho hizi ziliepukaje angamizo hili? Natanguliza shukrani mkuu.
Kwa mujibu wa watafiti mbali mbali na vitabu na makala mbali mbali na utafiti wangu mwenyewe na ushahidi wa maandiko matakatifu ni kwamba hakuna tena muingiliano ule kwakuwa wale malaika wapo kifungoni lakini kuna kitu sijaweza kukielewa ni kwa namna ipi hii blood line ipo hadi leo baada ya gharika maana hata Biblia inasema kwamba Wanefili walikuwepo kabla ya gharioka na baadaye....

Waisraeli,wakati wanawaona Wakanaan walijiona ni kama panzi mbele yao,hii inaonesha walikutana na Wanefili,Goliathi alikuwa ni Mnefili n.k na hii ni baada ya gharika....

Hili ngoja niendelee kufanya utafiti ili nijue ilikuwaje....
 
Tangu niliposoma na kujua alichokuwa anakimaanisha Plato kwenye kitabu chake cha Republic hasa kwenye story yake ya Allegory of the Cave ndiyo nilianza kuelewa kabisa hasa tunaishi kwenye dunia ya namna ipi....

Kimsingi,watu wote ambao leo tunawachukulia kama "majiniaz" walipata ujuzi waliokuwa nao kutoka mahali fulani,Mesopotamia huko.Pythagoras,Socrates,Galileo,Alexander the Great,Plato na hadi hawa akina Sir Francis Beacon na John Dee ni watu ambao walipata elimu hizi tofauti kabisa na wanafunzi wengine waliikuwa kwenye madarasa ya watu hawa....

Socrates aliwahi kumueleza mwanafunzi wake mmoja aitwaye Plato kwenye madarasa yao kwamba,elimu anayowapa ni elimu iliyoko kwenye makundi mawili.Kunsi la kwanza ni lile la kawaida ambalo wanapewa elimu ya kawaida kuhusu mafuzo waliyokuwa wanapewa na kundi la pili ni lile ambalo linapewa elimu maalum na nyeti ambayo hakupaswa kupewa mtu yoyote na ni elimu maalum ambayo ndiyo lengo kuu la wao kufundishwa....

Kwenye darasa maalum ambalo walipewa elimu maalum ambayo Socrates alimueleza Plato,miongopni mwa wanafunzi waliokuwemo ni Plato mwenyewe.Utaratiobu huu ambao Plato alielezwa na mwalimu wake ulikuwepo tangu Socrates mwenyewe alipopata ujuzi huo kutoka kwa Pythagoras na Plato aliendelea kuwa nao na hata wanafunzi wake waliofuatioa kama akina Alexander The Great waliendelea nao....

Hapa sasa dipo tunakuja kupata maana mbili za hadithi ya Allegory of the Cave inayopatikana kwenye kitabu cha Plato kiitwacho The Republic.....

Hadithi ile inazungumzia watu waliokuwa kwenye pango ambao walikuwa wamefungwa kwa minyororo kwenye miguu yao wakati huo huo nyuma yao kukiwa kuna mto unaowaka.Watu hawa waliishi kwenye pango hili kwa miaka mingi sana,wakiwa wameelekezea nyuso zao kwenye ukuta wa pango lile wakitazama vivuli vyao ukutani na waliamini ule ndiyo ulikuwa uhalisia [the dancing shadow became their reality]....

Kwao maisha na dunia ilikuwa ni ile waliyokuwa wakiiona kwenye pango lile.vivuli ndiyo mazingira yaliyowazunguka na huo ulikuwa ni ukweli mkubwa sana kwao....

Uhalisia ule ambao ulikuwa wazi kabisa kwenye macho yao ndiyo ulikuwa ukweli.Haikuwa rahisi kabisa kuja kumueleza mmoja wao au wote kwamba ule hukuwa uhalisia kwakuwa walikuwa wakiona kwa macho yao.Waliamini kila walichokuwa wakikiangalia kilikuwa ndicho halisi...

Bahati mbaya kabisa ni kwamba hawakujua kwamba uhalisia ule ulikuwa umetengenezwa tu,haukuwa halisi.Waliamini kila walichokuwa wanakiona ni halisi.Waliamini hakuna anayeweza kutengeneza kitu halafu kikaonekana kuwa halisi hadi siku mmoja wao alipokata mnyororo na kutoka nje na kuuona uhalisia halisi na kurudi ndani kuwafungua wenzake minyororo ile na wao kuja kuuona uhalisia ambao hata kwa bunduki wasingekubali kuwa upo kama mtu angeenda kuwaeleza hili.....

Ukiangalia au ukitaka kujua maana ya hadithihii ndipo utakuja kuona kile ambacho kinaendelea duniani.Plato aliwaeleza maana halisi ya hadithi hii watu wachache sana wanaitwa "the elect ones",watu ambao walikuwa wakielezwa haya kwa sababu maalaum ili waje kutawala dunia....

Kinachoendelea duniani leo sicho kilichopo kwenye uhalisia,siyo uhalisia bali ni uhalisia uliotengenezwa tu.Wengi na nadhani hata wewe unaamini kuna ugonjwa unaosababishwa na kirusi fulani kinachoitwa HIV,unaamini kuna ugonjwa unoitwa EBOLA unaoua kikatili kabisa,unaamini kuna mafua ya ndege,unaamini kuna watu wanaotishia maisha ya watu wanaoitwa magaidi,unaamini rais wa Marekani anachaguliwa na wapiga kura kidemokrasia,unaamini kuna uadui kati ya Marekani,China na Urusi,unaamini dunia ina watu wengi sana hivyo inaweza kuja kuleta matatizo hapo baadaye hivyo tunapaswa kutumia uzazi wa mpango.Unaamini kuwa dunia ina mabilioni ya miaka,Unaamini kuwa viwanda vinaharibu hali ya hewa na kuzababisha mvua kutonyesha na kuongeza joto duniani,fake relity ziko nyingi sana....

Tunaishi kwenye pango,vivuli vilivyotengenezwa na moto ndiyo uhalisia wetu,giza lililoko ndani ya pango ndiyo ukweli wetu.Minyoror inatufanya tuamini hivyo kwakuwa hatuwezi kutoka humo....

Sasa basi pango ni nini,minyororo ni nini?Moto na vivuli ni nini? Maana za haya yote utaweza kupata angalau clue kama utanisoma hapo juu kwa makini.Hapa ndipo tunapokuja kuamini kwamba vita vinasababishwa kwasababu tunazoambiwa,lakini kuna sababu za kweli ambazo hatuambiwi....

Tunaishi kwenye dunia ambayo ukipata hata nukta kidogo ya ukweli utaogopa....

Nimesema haya ili kukufanya mkuu MSEZA MKULU uangalie tena mara mbili sababu za vita ulivyovisema hapo kwenye mada yako ili uone kama hazina chumvi au uongo.....

Ashante......
Lecture yako ni kama nimeielewa kupitiliza. Please uwe unatupia tupia vitu adimu kama hivi. Napenda kusoma masomo yasiyopendwa na wengi ili nifundishe wengi.
 
Hii dunia ina mambo mengi yamejificha, huwa najiuliza kwanini Rothschild family na Rockefeller families hawamo kwenye Forbes au kwa sababu wao ni trillionaires?

2b38bc01fa0ac4d8366381a2ed359ee3.jpg
 
SHETANI yupo ila mchananuo wako mkuu unahitaji uuambatanishe na RELIABLE SOURCE
1: Source ya wanefili kuwa uzao au matokeo ya Shetani (kaumbwa kwa Moto) Kufanya ngono na Binadamu (Kaumbwa kwa udongo), Creation inasemaje je kuna uwezekano wa interbreed kati ya watu na maraika au mashetani?. Tuanzie hapo. Kama sio Bibilia pia iweke.
Labda nikuulize,ni Malika wote wameumbwa kama Shetani?

Nijuavyo mimi Lucifer ni malaika wa nuru,aliumbwa kwa namna ya kuvutia sana pamoja na malaika wengine,unachokifikiria wewe kiko kibinadamu zaidi wakati haya ni zaidi ya hapo,na ujue tu kuwa hawa malaika hawakufanya ngono na binadamu tu bali pia hadi na samaki,sasa jiulize hapo iliwezekana namna gani...

Hapa unchopaswa kujua ni kwamba tunawazungumzia viumbe ambao wanaweza kumanipulate kanuni zote unazozijua wewe maana wao wanajua kile kilichofanyika tangu mwanzo na ujuzi huo wanautumia kwa njia hasi....
2:Je Maraika wa shetani walioasi WANAJINSIA. Yaani Kuna maraika majike na madume.
Mkuu unawaza kirahisi sana,sijui kama unanielewa....

Kuanza kufikiria tu ili kiumbe kzaliane ni mpaka kiwe na njinsia ni kosa kubwa,lakini maandiko yanasema kuwa malaika hao [waana wa Mungu] waliwatamani wanawake wa kibinadamu na wakaona ni sawa kisha wakajitwalia wakawa wake zao,sasa hapo unaona wazi kilichotokea ni nini....
Mwanadamu waliwekewa sexual organs ili wainterbreed kama ilivyo kwa wanyama wote. Vipi kuhusu hao maraika kwani huko mbinguni walikuwa wanajifungua hadi walipohasi waweze kufanya mapenzi na Mwanadamu.
Uelewa wetu kuhusu wanachkifanya malaika huko mbinguni uko very limited hivyo kuna mambo ambayo hatujui,lakini kwakuwa malaika wameumbwa na uwezo mkubwa zaidi yetu naweza kusema kuwa [hapa natumia akili yangu tu kutafakari] inawezekana wale malaika walikuwa na uwezo wa kuwa na jinsia watakayo au wakawa hawana jinsia hapo hapo hivyo kurahisisha watakacho kwa wakati husika maana maandiko yameeleza kuwa waliingiliana na wanawake wa kibinadamu lakini hayajasema kuhusu mbinguni na kuhusu jinsia za malaika.....
Nini lengo la Mungu kuruhusu inerpreed ya viumbe wasiohusiana kama ni kweli?
Kwenye kitabu cha Danieli ule ukurasa wa 2 kuna mahali amesema kuhusu jambo hili kutokea nadhani ni Danieli 2:44 [sina uhakika] lakini kuna mahali pameandikwa "nao watajichanganya nafsi zao na wanadamu lakini hawatafanikiwa",kwa nijuavyo hapo anazungumza suala hili la wao kutaka kujichanganya na sisi kwa kutumia DNA....

Mambo haya kwenye Biblia yameandikwa kwa Sammary zaidi lakini ukiyachunguza yapo kabisa na yameonywa sana....
3:Baada ya Gharika walipona watu wanane dunia nzima. Unaushahidi gani kuwa watu hawa walikuwa na satanic genetic make up. Je gene za mwanadamu na shetani zinaweza kucross each other kuexchange genetic information. DOES DEMONS HAVE GENES as Humanbeing? Source.
Hili sijajua ni kwa namna ipi hii blod line iliendelea kuwepo lakini ilikuwepo na hata Biblia inasema hilikwenye Mwanzo 6:4 maan walikuwepo wakati ule na baada ya hapo na ukitaka kuona ushahidi huu angalia ile battle ya Waisraeli na Wakanaan ambao waisraeli walijiona kama panzi mbele ya yale majitu makubwa....
4:Hii ngono kati ya shetani na wanadamu bado inatokea hadi leo. Kwa nini tunaambiwa Mungu atamuhukumu Kila mwandamu kwa maamuzi aliyofanya kwa akili yake timamu zio matokeo ya Kuwa Shetani/mtu. Hii concept inadistort maana nzima ya HUKUMU YA KWELI NA HAKI.
Hili mkuu umelitoa wapi?
5:Maelezo yote hayajaweka wazi nafasi ya Mungu na Maraika wake ktk Pambano hilo. Ila imemkuza shetani na maraika zake.
Hujahitaji kujua hili mkuu na nitalielezeaje?
Kwa mtazamo wangu Unayosema ni mchanganyiko wa FACTS NA ASSUMPTIONS. Ni kweli kuna wanadamu wachache wenye akili wenda kwa kukubali kwa maagents wa shetani na sio kuwa product ya mchanayiko wa shetani na mwanadamu. Hii mipango mikubwa duniani inapangwa na pure wanadamuw alioamua kushirikiana na Shetani kudanganya watu ili siku ya hukumu ajiongezee washirika. Kuna watu

ndio maana naomba source za research yako pia kukuza uelewa.
sorry nilikuwa sijamaliza kucompile maswali yangu
Haya ni mawazo yako mkuu na una haki ya kufikiria hivyo....

Sijui unahitaji source ipi na ya namna ipi maana haya huwezi kuyakuta kwenye kijitabu kimoja au makala moja mkuu,ni rundo la makala na maeneo tofauti tofauti ya kiutafiti....
 
Napiga kambi ya kudumu hapa, Eiyer hapo kwa wabantu umeniongea kitu, kuna mtafiti mmoja alieleza namna zile kabila 12 za Israel zilivyotawanyika, akasema kwamba kabila la Yuda walihamia magharibi mwa Afrika, nikifuatilia historia ya wabantu naona walitokea huko magharibi mwa Afrika na kufika ukanda huu. Hapo kuna muunganiko flani
Jamaa yupo sahihi kabisa kwa namna ambayo na mimi nimepitia hiyo historia....

Pia,siyo kabila hilo tu bali na yale mengine pia....
 
Hii dunia ina mambo mengi yamejificha, huwa najiuliza kwanini Rothschild family na Rockefeller families hawamo kwenye Forbes au kwa sababu wao ni trillionaires?

2b38bc01fa0ac4d8366381a2ed359ee3.jpg
Namfahamu sana marehemu Arron Russo....

Huyu jamaa walimuua aisee....

Aligoma kabisa kuwa miongoni mwao na kwa kupitia huyu jamaa nilijua hasa ni kwanini kuna kitu kinaitwa "haki za wanawake"....

Hawa watu angalia sana kile wanachokipinga ndicho salama kwa binadamu na uwepo wake....
 
Jamaa yupo sahihi kabisa kwa namna ambayo na mimi nimepitia hiyo historia....

Pia,siyo kabila hilo tu bali na yale mengine pia....
Alikuwa ni Freedom fighter, yaani kama huko nao umekwisha, yaani dunia tuione hivi hivi ukifatilia mambo mengi unaweza kimbia kuvuli chako.
 
Namfahamu sana marehemu Arron Russo....

Huyu jamaa walimuua aisee....

Aligoma kabisa kuwa miongoni mwao na kwa kupitia huyu jamaa nilijua hasa ni kwanini kuna kitu kinaitwa "haki za wanawake"....

Hawa watu angalia sana kile wanachokipinga ndicho salama kwa binadamu na uwepo wake....
Tushirikishe nasisi kuhusu haki za wanawake.
 
Watu wale wale ambao tunawajadili hapa ndio hao hao walioanzisha harakati za wanawake kudai haki zao.Kwa tafsiri zao ni kwamba mwanamke ni kiumbe ambaye hakuwa akipewa heshima yake na Mungu hivyo Shetani kwa kuwatumia watu hawa ndiyo anataka "kumkomboa" mwanamke kutoka kwenye makucha hayo.....

Lakini,ukweli ni kinyume kabisa.ili waweze kutawala vyema mwanadamu ni hadi pale ambapo watakapoweza kuwa na binadamu lazy wasiojielewa wasioweza ku reason.Kimsingi wanaweza kutumia akili nyingi zaidi kuweza kumtawala lakini hawakuona sababu ya kufanya hivyo wakaamua kutumia akili kidogo tu hapa...

David Rockerfeller alimambia Arron Russo kwamba,baada ya vita ya pili ya dunia wanaume walikufa sana vitani na hata wale ambao hawakuwa vitani waliuawa na vita maana wakati mwingine vita ilipiganwa kwenye makazi ya watu.Kutokana nba wanaume hawa kufa sana kukawa na upungufu wa wafanyakazi hivyo wakalazimika kuanzisha harakati ya kuwafanya wanawake kuingia makazini ili kuziba pengo hilo...

Anaendelea kusema kwamba,walihitaji wawapate watu wakiwa katika hatua zao za kwanza kabisa za ukuaji ili waweze ku shape namna yao ya kufikiri ili wasije kupata tabu wakati watakapotaka kuwa ongoza na kuwatawala,kwasababu hiyo,wanawake wanapokwenda kazini hii itawalazimu wasiwalee watoto wao wao wenyewe hivyo watatafuta wasaidizi.Kwa nchi za Ulaya na Marekani ni watu wachache sana ambao wanaweza kuaford kuwalipa wasaidizi hawa maana ni ghali....

Sheria hizi za kusimamia "haki" za wasaidizi wa ndani ziliwekwa na wao hao hao kwa malengo maalum ambayo utayaelewa kwenye maandishi haya haya....

Kwasababu ni ghali kuwalipa wasaidizi hawa wazazi watalazimika kuwapeleka watoto wao shule za watoto wadogo na vituo vya kulea watoto na huko wameweka watu wao ambao wataendelea kuwatengeneza watoto hawa kwa namna watakayo.David aliendelea kumueleza Risso kwamba,wanapowapata watoto wakiwa wadogo kiasi hiki ambacho ni kuanzia miezi mitatu na kuendelea kwasababu sheria [iliyowekwa na hao hao] ya mwanamke kumhudumia mtoto ni miezi mitatu tu na baada ya hapo anapaswa aende kazini na anakuwa amemaliza likizo yake ya uzazi...

Huyu jamaa aliendelea kumueleza Russo kuwa kwa kufanya hivyo waliweza kumshape mtoto afikiri kwa namna atakayo na leo tunaona matokeo ya jambo hili,unaweza kushangaa vijana wa kuanzia miaka 45 kurudi chini wanafikiri kwa namna ya kufanana kabisa na haya ni matokeo ya jambo hili....

Lakini pamoja na hilo,jamaa alisema kuwa wanawake wakienda kufanya kazi watakuwa wakikatwa kodi ya mapato hivyo kuongeza mapato.....

Kwa maana nyingine hakuna haki za wanawake zinazotafutwa hapa isipokuwa ni mipango mingine tu.Kuna zaidi ya hili kwenye jambo hili lakini nadhani jambo hili linatosha kukata kiu yako na umeridhika nadhani.....
 
Labda nikuulize,ni Malika wote wameumbwa kama Shetani?

Nijuavyo mimi Lucifer ni malaika wa nuru,aliumbwa kwa namna ya kuvutia sana pamoja na malaika wengine,unachokifikiria wewe kiko kibinadamu zaidi wakati haya ni zaidi ya hapo,na ujue tu kuwa hawa malaika hawakufanya ngono na binadamu tu bali pia hadi na samaki,sasa jiulize hapo iliwezekana namna gani...

Hapa unchopaswa kujua ni kwamba tunawazungumzia viumbe ambao wanaweza kumanipulate kanuni zote unazozijua wewe maana wao wanajua kile kilichofanyika tangu mwanzo na ujuzi huo wanautumia kwa njia hasi....

Mkuu unawaza kirahisi sana,sijui kama unanielewa....

Kuanza kufikiria tu ili kiumbe kzaliane ni mpaka kiwe na njinsia ni kosa kubwa,lakini maandiko yanasema kuwa malaika hao [waana wa Mungu] waliwatamani wanawake wa kibinadamu na wakaona ni sawa kisha wakajitwalia wakawa wake zao,sasa hapo unaona wazi kilichotokea ni nini....

Uelewa wetu kuhusu wanachkifanya malaika huko mbinguni uko very limited hivyo kuna mambo ambayo hatujui,lakini kwakuwa malaika wameumbwa na uwezo mkubwa zaidi yetu naweza kusema kuwa [hapa natumia akili yangu tu kutafakari] inawezekana wale malaika walikuwa na uwezo wa kuwa na jinsia watakayo au wakawa hawana jinsia hapo hapo hivyo kurahisisha watakacho kwa wakati husika maana maandiko yameeleza kuwa waliingiliana na wanawake wa kibinadamu lakini hayajasema kuhusu mbinguni na kuhusu jinsia za malaika.....

Kwenye kitabu cha Danieli ule ukurasa wa 2 kuna mahali amesema kuhusu jambo hili kutokea nadhani ni Danieli 2:44 [sina uhakika] lakini kuna mahali pameandikwa "nao watajichanganya nafsi zao na wanadamu lakini hawatafanikiwa",kwa nijuavyo hapo anazungumza suala hili la wao kutaka kujichanganya na sisi kwa kutumia DNA....

Mambo haya kwenye Biblia yameandikwa kwa Sammary zaidi lakini ukiyachunguza yapo kabisa na yameonywa sana....

Hili sijajua ni kwa namna ipi hii blod line iliendelea kuwepo lakini ilikuwepo na hata Biblia inasema hilikwenye Mwanzo 6:4 maan walikuwepo wakati ule na baada ya hapo na ukitaka kuona ushahidi huu angalia ile battle ya Waisraeli na Wakanaan ambao waisraeli walijiona kama panzi mbele ya yale majitu makubwa....

Hili mkuu umelitoa wapi?

Hujahitaji kujua hili mkuu na nitalielezeaje?

Haya ni mawazo yako mkuu na una haki ya kufikiria hivyo....

Sijui unahitaji source ipi na ya namna ipi maana haya huwezi kuyakuta kwenye kijitabu kimoja au makala moja mkuu,ni rundo la makala na maeneo tofauti tofauti ya kiutafiti....
Nitaeleza kwa upande wangu. kisha nitakuomba urudi kwenye mada, hATA KAMA UTAPENDA KUELEZA KIROHO JIKITE HIYO KIROHO IMESABABISHABISHAJE WW1,WW2 AND WAR ON TERROR KWA UNDANI. Au ueleze kwa kina hao unaowaamini alliens/Hybrid ya Shetani na watu wamechangia vipi MADA TAJWA.

Naomba pia uelewe kitu kingine, Kuna BOTTOMLESS KNOWLEDGE about everything katika dunia nje ya BIBILIA ambazo zinaweza kuwa associated na bibilia au kuonekana wakati mwingine bora kuliko bibilia kuamini au kutokuamini ni Uchaguzi.

BINAFSI NAOMBA NITOE MTAZAMO WANGU KATIKA HAYO YA KIROHO UNAYOAMINI.

1: Bibilia inayoaminiwa na waprotestant na wakristo wengi ni Yenye vitabu 66, lakini wenzetu wakatoriki wanaamini ndani zaidi vitabu hadi vinafika 74 kwa sababu ambazo wao wanaweza kujua vizuri na wanweza kueleza.

2: Vitabu kama wamakabayo,tobiti, Ysuph bin sira, Judith etc kama sijakosea. Ila vitabu hivi wakristo wengi hasa waprotestant hawavioni kama vinaumana na kama viko inspired to regarded as Inspired world of God. Pia kuna vitabu vingi tu viliibuka na kutaka kuingizwa kwenye bibilia bila mafanikio. Hii ni mada nyingine Hapa tunzaungumzia Vita vya Bibilia Iliyopiotia. Ila Common Bible ambayo inatumika Duniani kote na wakristo wa aina karibu zote ni ile yenye vitabu 66 na mimi hiyo ndiyo reference yangu tunapozungumzia mambo ya kiroho.

3: VITABU UNAVYOAMINI KAMA PARTNER AU VILIPASWA KUWEPO NDANI YA BIBILIA: 1 BOOK OF ENOCH na nadhani ndio source ya elimu hii unayoileta.
Nimeipitia kidogo na Inamapungufu megi ambayo kama ni mwaminifu kwa bibilia 66 Books hakina adhi ya kuwa equally yoked na other inspired world of God.

KWA UFUPI SANA NAOMBA NIKUONYESHE MACHACHE YASIYO NA MASHIKO KATIKA KITABU HICHO
1: Kimegawanyika katika sehemu kuu tano
a/ The Book of WATCHERS (Chapter 1-36)
b/ The Book of similtudes (Chapter 37 -71)
c/ The book of ASTRONOMICAL WRITTINGS (Chapter 72-82)
d/The book of Dreams and Visions (Chapter 83 - 90)
e/ The book of the epistle of Enoch (Chapter 91 - 107)
Maelezo na Mapungufu
Vitabu vyote hivyo vilivyomo kwenye kitabu kinachosadikika kuandikwa na ENOCH wa kwenye Bibilia Vikipimwa vinaonekana vimeandikwa katika mida tofautitofauti na muda husiohusaiana na Muda aliokuwepo ENOCH. Kuna vingine vinaonekana kuwaandikwa AD.

MAelezo zaidi juu ya udhaifu wa SOURCE YAKO YA SHETANI WATU

1:NENO wana wa Mungu limetokea mara 18 kwenye kitabu kimoja tu cha Similtudes wakati sehemu nyingine haionekani. Na kama Sons of God alikuwa anaongelea Maraika basi na Yesu nae ni Maraika maana Aliitwa hivyo na pia HAta Daniel amezungumziwa pia ila watetezi wa hoja hii huruka kitabu cha daniel wana wa mungu walipoziungumziwa.

2:GEOCENTRIC: INASUPPORT HOJA YA ARISTOTLE na WENZAKE WA FLAT EARTH SOCIETY kuwa JUA NDIO LINAZUNGUKA DUNIA which is Biblically and scientific Wrong. NA RUNNERS WA HIZI IDEA mbili ni wapinga Mungu. HIi ni Gnosticism . Fungu lipo.

3:1 Enoch 67:1-3 inasema maraika walitengeneza safina kitu ambacho ni bibilically incorrect
Inafanya kitabu chote kisikubalike

4:Bibilia kutoeleza kwa kina uumbaji wa maraika na shetani japo imeelizwa haikifanya kitabu kingine nje yake ambacho kwanza chenyewe kinajipinga na kinapingana na bibilia kuwa sahihi.

5:Kinasema MASHETANI walifungwa miaka 10000 baada ya gharika. Lakini chenyewe kinajipinga kuhusu hoja hii katika chapter ya 10, 18 na 21. Na kuna sehemu nyingi kinaandika vitu vinavyojipingha kana kwamba kimeandikwa na watu wanne au mwandishi alikuwa msahaulifu.

6:KUISOMA 1ENOCH 22:13 Inakifanya kitabu hiki kisifae kabisa kuhusianishwa na Bibilia maana Kinazungumza eti kuna baadhi ya watu waliokufa hawata fufuliwa kabisa na wala hawatahukumuiwa kinyumbe na Ufunuo 20:12 - 13
Na mafundisho yote ya bibilia kuwa kila mtu ataletwa hukumuni.

7:Kinasema ENOCH alirudi kuja kumsaidia NUHU katika Gharika na akashindwa kurudi tena mbinguni. Atawezaje kutoka mbinguni alafu ashindwe. Mambo haya kwenye bibilia hayamo na kufanya hizi kuwa ni ujanjaujnaja wa wachache.

8: Kinasema Enoch alionekana kwenda katika mji wa dan. Dani kwenye bibilia ni mtoto wa YAKOBO, na MAKazi ya UZAO wa DAN israel baada ya kutoka Misri ni kipindi ambacho enoch alikuwa amekwisha kuchukuliwa. Inaonekana Muandishi aliandika wakti Israel imeshakuwepo ambacho kinapingana na bibilia maana enoch wakati ENOCH YUPO HUyu dani, wala baba yake yakobo, wala Ibrahim,. Wla baba yake ibrahim HAwakuwa wamezaliwa. Hii inamfanya mwandishi wa maandishi haya kutiliwa shaka sana yawezekana akwa ni mtu mwingine mwenye malengo ya kuitumia bibilia kupitisha hoja zake.

Na mengine mengi.

Naomba turudi kwenye mada, Tumia maarifa yako hayo kurespond kwenye mada maana huku unaibua maswali ambayo yanazidi kupoteza kabisa mwelekeo wa kinachojadiliwa. Unaweza kutumia elimu yako hjiyo kueleza inauhusiano Gani na kile kilichoandikwa na nini msimamo au mawazo yako juu ya mada husika
 
Nitaeleza kwa upande wangu. kisha nitakuomba urudi kwenye mada, hATA KAMA UTAPENDA KUELEZA KIROHO JIKITE HIYO KIROHO IMESABABISHABISHAJE WW1,WW2 AND WAR ON TERROR KWA UNDANI. Au ueleze kwa kina hao unaowaamini alliens/Hybrid ya Shetani na watu wamechangia vipi MADA TAJWA.
Sawa nitaeleza lakini acha nijibu hizi hja zako hapa chili ili kuweka ulinganifu na sio niache kujibu halafu niende kwenye ukitakacho...

Pamoja na hayo,post yangu ya kwanza iliyomtaja Plato imeelezea link baina ya hiki nilichokisema na mada yako labda uwe hujaielewa....
Naomba pia uelewe kitu kingine, Kuna BOTTOMLESS KNOWLEDGE about everything katika dunia nje ya BIBILIA ambazo zinaweza kuwa associated na bibilia au kuonekana wakati mwingine bora kuliko bibilia kuamini au kutokuamini ni Uchaguzi.
Binafsi sioni kama kuna ambacho kipo zaidi ya Biblia,huo ndiyo msimamo wangu kwenye hili....
BINAFSI NAOMBA NITOE MTAZAMO WANGU KATIKA HAYO YA KIROHO UNAYOAMINI.
Mgoja niangalie kama unayodai naamini ndiyo hayo au kuna shida mahali.....
1: Bibilia inayoaminiwa na waprotestant na wakristo wengi ni Yenye vitabu 66, lakini wenzetu wakatoriki wanaamini ndani zaidi vitabu hadi vinafika 74 kwa sababu ambazo wao wanaweza kujua vizuri na wanweza kueleza.
Sijui unamaanisha nini unaposema "Wakristo wengi" lakini kama unamaanisha wingi wa kuwa na kundi kubwa ukweli ni kwamba siyo kweli biblia ya vitabu 66 inakubaliwa na Wakristo wengi kwasababu wakatoliki ni wengi kuliko Wakristo wengine wa Madhehebu yote ya Kikristo hivyo dhana yako haiko sahihi

Sababu za Wakatoliki kukubali vitabu zaidi ya vile ambavyo Waprotestant wanavikubali ni jambo ambalo linashangaza kidogo,kwakuwa hii siyo mada acha niliache kwa sasa.....
2: Vitabu kama wamakabayo,tobiti, Ysuph bin sira, Judith etc kama sijakosea. Ila vitabu hivi wakristo wengi hasa waprotestant hawavioni kama vinaumana na kama viko inspired to regarded as Inspired world of God. Pia kuna vitabu vingi tu viliibuka na kutaka kuingizwa kwenye bibilia bila mafanikio. Hii ni mada nyingine Hapa tunzaungumzia Vita vya Bibilia Iliyopiotia. Ila Common Bible ambayo inatumika Duniani kote na wakristo wa aina karibu zote ni ile yenye vitabu 66 na mimi hiyo ndiyo reference yangu tunapozungumzia mambo ya kiroho.
Naona unaendelea kutumia wingi kama kigezo cha kutaka watu waamini kwamba hiyo ni sababu ya biblia yenye vitabu 66 kuwa sahihi kitu ambacho siyo kweli kabisa...

nijuavyo mimi ni kwamba kama ni kuna ukweli kwenye ukisemacho basi ukweli huo hufanywi kuwepo na wingi wa wanaoikubali bali kilichomo kwenye vitabu hivyo...

Pamoja na hilo,siyo kweli kuwa biblia yenye vitabu 66 inakubaliwa na wengi na ndiyo inayotumika duniani kama biblia ramsi,hili haliko sahihi kabisa na nimekuambia hapo juu....
3: VITABU UNAVYOAMINI KAMA PARTNER AU VILIPASWA KUWEPO NDANI YA BIBILIA:
Mkuu ngoja niachane na mengine yote kwenye kauli yako hii maana tutaenda mbele sana,nikuulize swali moja tu....

Kati yako wewe na wanafunzi wa Yesu ni nani ambaye anajua uhalali wa kitabu hiki?
1 BOOK OF ENOCH na nadhani ndio source ya elimu hii unayoileta.
Hapana,siyo source pekee bali kuna Biblia pia....
Nimeipitia kidogo na Inamapungufu megi ambayo kama ni mwaminifu kwa bibilia 66 Books hakina adhi ya kuwa equally yoked na other inspired world of God.
Hebu tuone hayo mapungufu mkuu....
KWA UFUPI SANA NAOMBA NIKUONYESHE MACHACHE YASIYO NA MASHIKO KATIKA KITABU HICHO
1: Kimegawanyika katika sehemu kuu tano
a/ The Book of WATCHERS (Chapter 1-36)
b/ The Book of similtudes (Chapter 37 -71)
c/ The book of ASTRONOMICAL WRITTINGS (Chapter 72-82)
d/The book of Dreams and Visions (Chapter 83 - 90)
e/ The book of the epistle of Enoch (Chapter 91 - 107)
Hicho ulichotaja cha mwsho ni toleo jingine la kitabu hiki.Usichokijua ni kwamba kitabu hiki kimetolewa matoleo mengi na mengine ni fake na nadhani haya umeyatoa kwa wapinzani wa kitabu hiki ambao wengi wamepotosha tu kwa sababu zao wenyewe na wengine ni miongoni mwa hawa ninaowataja hapa ili watu wasikitafute kitabu hiki....

Kuna toleo la kitabu hiki ambalo ni la zamani sana hata kabla ya Musa....
Maelezo na Mapungufu
Vitabu vyote hivyo vilivyomo kwenye kitabu kinachosadikika kuandikwa na ENOCH wa kwenye Bibilia Vikipimwa vinaonekana vimeandikwa katika mida tofautitofauti na muda husiohusaiana na Muda aliokuwepo ENOCH. Kuna vingine vinaonekana kuwaandikwa AD.
Hili nimekueleza hapo juu kuwa kuna udanganyifu,inawezekana unazungumzia toleo jingine kabisa ambalo lina shida fulani.

Usichokijua ni kwamba kuna vitabu huwezi kuvipata kiurahisi nyakati hizi hivyo unapaswa kujua unachokitafuta na siyo kwenda tu kwenye net na kujichukulia....
MAelezo zaidi juu ya udhaifu wa SOURCE YAKO YA SHETANI WATU

1:NENO wana wa Mungu limetokea mara 18 kwenye kitabu kimoja tu cha Similtudes wakati sehemu nyingine haionekani. Na kama Sons of God alikuwa anaongelea Maraika basi na Yesu nae ni Maraika maana Aliitwa hivyo na pia HAta Daniel amezungumziwa pia ila watetezi wa hoja hii huruka kitabu cha daniel wana wa mungu walipoziungumziwa.
Hahahahaaaa.....

Mkuu umenichekesha sana,kwa kuanzia ni wapi yesu ameitwa "sons of God"?

Anyway,kuna haja ya kuandaa mada kwaajili ya hili...
2:GEOCENTRIC: INASUPPORT HOJA YA ARISTOTLE na WENZAKE WA FLAT EARTH SOCIETY kuwa JUA NDIO LINAZUNGUKA DUNIA which is Biblically and scientific Wrong. NA RUNNERS WA HIZI IDEA mbili ni wapinga Mungu. HIi ni Gnosticism . Fungu lipo.
Hata hili nalo lina ukakasi sana tu.Acha niliache lakini suala la umbo la dunia unaposema Biblia imesema ni umbo la tufe kama wanasayansi wanavyoongea sidhani kama ni kweli.Biblia imezungumzia "duara ya dunia" duara hii haijasemwa kuwa ni ya tife maana duara inaweza kuwa yoyote maana hata CD nayo ni duara.....
3:1 Enoch 67:1-3 inasema maraika walitengeneza safina kitu ambacho ni bibilically incorrect
Inafanya kitabu chote kisikubalike
Kutokana na haya maelezo yako yalivyo nachelea kusema kwamba hujakisoma hiki kitabu,hebu tumia muda kutafuta ukwli kwenye hili na nakushauri hii hoja achana nayo na ifute kabisa kwenye kichwa chako halafu ujifunze kwanza kisha urudi hapa,kama kuna kitabu umesoma basi siyo kitabu cha Enoch....
4:Bibilia kutoeleza kwa kina uumbaji wa maraika na shetani japo imeelizwa haikifanya kitabu kingine nje yake ambacho kwanza chenyewe kinajipinga na kinapingana na bibilia kuwa sahihi.
Kitabu ninachokisema hakina makosa unayosema.Kwasababu hii basi nakushauri hizi hoja zako achana nazo kabisa maana naona umesoma kitabu tofauti....
5:Kinasema MASHETANI walifungwa miaka 10000 baada ya gharika. Lakini chenyewe kinajipinga kuhusu hoja hii katika chapter ya 10, 18 na 21. Na kuna sehemu nyingi kinaandika vitu vinavyojipingha kana kwamba kimeandikwa na watu wanne au mwandishi alikuwa msahaulifu.

6:KUISOMA 1ENOCH 22:13 Inakifanya kitabu hiki kisifae kabisa kuhusianishwa na Bibilia maana Kinazungumza eti kuna baadhi ya watu waliokufa hawata fufuliwa kabisa na wala hawatahukumuiwa kinyumbe na Ufunuo 20:12 - 13
Na mafundisho yote ya bibilia kuwa kila mtu ataletwa hukumuni.

7:Kinasema ENOCH alirudi kuja kumsaidia NUHU katika Gharika na akashindwa kurudi tena mbinguni. Atawezaje kutoka mbinguni alafu ashindwe. Mambo haya kwenye bibilia hayamo na kufanya hizi kuwa ni ujanjaujnaja wa wachache.

8: Kinasema Enoch alionekana kwenda katika mji wa dan. Dani kwenye bibilia ni mtoto wa YAKOBO, na MAKazi ya UZAO wa DAN israel baada ya kutoka Misri ni kipindi ambacho enoch alikuwa amekwisha kuchukuliwa. Inaonekana Muandishi aliandika wakti Israel imeshakuwepo ambacho kinapingana na bibilia maana enoch wakati ENOCH YUPO HUyu dani, wala baba yake yakobo, wala Ibrahim,. Wla baba yake ibrahim HAwakuwa wamezaliwa. Hii inamfanya mwandishi wa maandishi haya kutiliwa shaka sana yawezekana akwa ni mtu mwingine mwenye malengo ya kuitumia bibilia kupitisha hoja zake.

Na mengine mengi.
Hizi hoja zako zote hazina ukweli,kama nilivyokuambia hapo juu tafuta kitabu halisi cha Enoch na usome,hizi hoja ni chaka baya kabisa....
Naomba turudi kwenye mada, Tumia maarifa yako hayo kurespond kwenye mada maana huku unaibua maswali ambayo yanazidi kupoteza kabisa mwelekeo wa kinachojadiliwa. Unaweza kutumia elimu yako hjiyo kueleza inauhusiano Gani na kile kilichoandikwa na nini msimamo au mawazo yako juu ya mada husika
Suala la hoja zangu ambazo zilikuja kusababisha kutaja kitabu hiki zinahusiana na mada yako.Harakati za malaika waovu ndiyo zilizaa vita ambazo umeweka mada kuzihusu hivyo niko kwenye mada bado.....

Labda utake ijadiliwe na watu wengine wenye mtazamo kama wako.....
 
Wajinga huhitaji kujifunza na kuelewa
Bali wapumbav huona tayari wana maarifa kumbe la..!
Maana kama ufahamu wako una upumbav
Basi ni dhahiri hutotaka kusikia jambo na kulichanganua
Dunia haijawahi kuendelea kwa utabiri.

Ni ujinga tu umewaita. Sisi huwa tunayasoma sana hayo na mwishowe tunaelewa kuwa huu ni upuuzi.

Kwa ajili ya kukujuza tu kuwa huo ni ujinga, tuchukulie huo ni ukweli, ingawa siyo. Jee, unakusaidia / utakusaidia nini? Au wengine unawasaidia nini?

Ukijibu hayo honestly, utajielewa kuwa kufata hayo ni ujinga tu.

Hakika wajinga ndiyo waliwao.
 
Sawa nitaeleza lakini acha nijibu hizi hja zako hapa chili ili kuweka ulinganifu na sio niache kujibu halafu niende kwenye ukitakacho...

Pamoja na hayo,post yangu ya kwanza iliyomtaja Plato imeelezea link baina ya hiki nilichokisema na mada yako labda uwe hujaielewa....

Binafsi sioni kama kuna ambacho kipo zaidi ya Biblia,huo ndiyo msimamo wangu kwenye hili....

Mgoja niangalie kama unayodai naamini ndiyo hayo au kuna shida mahali.....

Sijui unamaanisha nini unaposema "Wakristo wengi" lakini kama unamaanisha wingi wa kuwa na kundi kubwa ukweli ni kwamba siyo kweli biblia ya vitabu 66 inakubaliwa na Wakristo wengi kwasababu wakatoliki ni wengi kuliko Wakristo wengine wa Madhehebu yote ya Kikristo hivyo dhana yako haiko sahihi

Sababu za Wakatoliki kukubali vitabu zaidi ya vile ambavyo Waprotestant wanavikubali ni jambo ambalo linashangaza kidogo,kwakuwa hii siyo mada acha niliache kwa sasa.....

Naona unaendelea kutumia wingi kama kigezo cha kutaka watu waamini kwamba hiyo ni sababu ya biblia yenye vitabu 66 kuwa sahihi kitu ambacho siyo kweli kabisa...

nijuavyo mimi ni kwamba kama ni kuna ukweli kwenye ukisemacho basi ukweli huo hufanywi kuwepo na wingi wa wanaoikubali bali kilichomo kwenye vitabu hivyo...

Pamoja na hilo,siyo kweli kuwa biblia yenye vitabu 66 inakubaliwa na wengi na ndiyo inayotumika duniani kama biblia ramsi,hili haliko sahihi kabisa na nimekuambia hapo juu....

Mkuu ngoja niachane na mengine yote kwenye kauli yako hii maana tutaenda mbele sana,nikuulize swali moja tu....

Kati yako wewe na wanafunzi wa Yesu ni nani ambaye anajua uhalali wa kitabu hiki?

Hapana,siyo source pekee bali kuna Biblia pia....

Hebu tuone hayo mapungufu mkuu....

Hicho ulichotaja cha mwsho ni toleo jingine la kitabu hiki.Usichokijua ni kwamba kitabu hiki kimetolewa matoleo mengi na mengine ni fake na nadhani haya umeyatoa kwa wapinzani wa kitabu hiki ambao wengi wamepotosha tu kwa sababu zao wenyewe na wengine ni miongoni mwa hawa ninaowataja hapa ili watu wasikitafute kitabu hiki....

Kuna toleo la kitabu hiki ambalo ni la zamani sana hata kabla ya Musa....

Hili nimekueleza hapo juu kuwa kuna udanganyifu,inawezekana unazungumzia toleo jingine kabisa ambalo lina shida fulani.

Usichokijua ni kwamba kuna vitabu huwezi kuvipata kiurahisi nyakati hizi hivyo unapaswa kujua unachokitafuta na siyo kwenda tu kwenye net na kujichukulia....

Hahahahaaaa.....

Mkuu umenichekesha sana,kwa kuanzia ni wapi yesu ameitwa "sons of God"?

Anyway,kuna haja ya kuandaa mada kwaajili ya hili...

Hata hili nalo lina ukakasi sana tu.Acha niliache lakini suala la umbo la dunia unaposema Biblia imesema ni umbo la tufe kama wanasayansi wanavyoongea sidhani kama ni kweli.Biblia imezungumzia "duara ya dunia" duara hii haijasemwa kuwa ni ya tife maana duara inaweza kuwa yoyote maana hata CD nayo ni duara.....

Kutokana na haya maelezo yako yalivyo nachelea kusema kwamba hujakisoma hiki kitabu,hebu tumia muda kutafuta ukwli kwenye hili na nakushauri hii hoja achana nayo na ifute kabisa kwenye kichwa chako halafu ujifunze kwanza kisha urudi hapa,kama kuna kitabu umesoma basi siyo kitabu cha Enoch....

Kitabu ninachokisema hakina makosa unayosema.Kwasababu hii basi nakushauri hizi hoja zako achana nazo kabisa maana naona umesoma kitabu tofauti....

Hizi hoja zako zote hazina ukweli,kama nilivyokuambia hapo juu tafuta kitabu halisi cha Enoch na usome,hizi hoja ni chaka baya kabisa....

Suala la hoja zangu ambazo zilikuja kusababisha kutaja kitabu hiki zinahusiana na mada yako.Harakati za malaika waovu ndiyo zilizaa vita ambazo umeweka mada kuzihusu hivyo niko kwenye mada bado.....

Labda utake ijadiliwe na watu wengine wenye mtazamo kama wako.....
Hiyo ianzishie mada yake maana kama unakana quotation kutoka kwenye reliable source Bila kuonyesha QUOTE sahihi ili tufanye comparison inatia Shaka kama hata vyanzo halisi umewahi kuvipitia. Ulipaswa kusema book of Enoch hasa verse uliyopewa kuwa sio sahihi kwa kutoa verse unayodhani ni sahihi.
Tunaelewana na kupishana kwenye angle kuu moja. Mungu aliumba free being hakuna chotara wa kishetani mwenye Uwezo mkubwa sana ambaye yuko nyuma ya mipango miovu ya dunia hii Bali ni hawahawa wanadamu huru sio chotara ndio wako nyuma ya kinachoendelea duniani.
Ila kwa sababu unasema ulichoelewa ni punje ya mchanga katika bahari yawezekana research yako ikakurudisha kwenye uhalisia kwamba hakuna chotara wa kishetani ambaye yuko nyuma ya uovu wa dunia Bali ni mwanadamu mwenye akili huru aliyeamua kufanya hayo kwa ushirikiano na separate Shetani. Hiki ndicho utakielewa siku ukitupa hicho occultic book na kubaki believer wa pure Bible.
Kwa hoja zako hata jamaa wa juzi itv aliyekuwa mrefu na mkubwa kuliko watanzania wengine unasema ni nephil au hybrid. Goliath kwa evidence ipi alikuwa nephil? Spy waliotumwa na kutisha watu kuwa wao ni kama panzi exaggeration Mungu aliwaua wote maana ulikuwa uongo na chumvi ili jamaa warudi misri. Yoshua na karebu walipo pambana na wakaanani hakukuwa na hicho kitu. Ila uko huru kuchagua chochote kile.
 
Wakuu EIYER na MSEZA MKULU,binafsi naona nyote mna hoja tena zina mashiko mazuri ila inaonekana sources zenu ndio zinatofautiana na hapo kupelekea ninyi kubishana. Napendekeza kila mtu amwage madini kulingana na anavyojua ili sisi tupate mwanga pia. Kuna mengi ya kujifunza hapa na lengo la wote ni kutuelimisha
 
Back
Top Bottom