Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
hujaelewa nini hapa?.
P.
- Mradi unaelezwa unakwenda kinyume cha mikataba ya kulinda World Heritage ambayo Tanzania tumesaini, this also is nothing!,
- Tanzania tumesaini mikataba kibao ya kimataifa ya haki za binaadamu na kila siku serikali inakiuka mikataba hiyo,
- kama rais Magufuli, ameikanyaga katiba alioapa kuilinda, what are the chances kuheshimu mikataba ya kimataifa kama itatuzuia kupata manufaa,
- to hell with mikataba ya kimataifa at the expense of development.
Hauwaelewi Wazungu, na wala haujui jinsi capitalistic system inavyo fanya kazi, WWF ipo ni kama NGO tu ili kufuja fedha ktk Ulaya na USA, wanaandika maproposal fake ili watu wapige hela, ni kama UN tu na UNHCR yao, bila ya kuwa na Wakimbizi watu hawana ajira na ndiyo maana Wakimbizi hawaishi Goma, Sudani na kwingineko isitoshe hata Trump anataka kukata funding ya UNHCR!
Hawa Wazungu wanaweza tu kupata fedha ktk Serikali zao kama wakija na projects fake kama hizi za kulinda Mbwa mwitu Selous, lkn siyo faida yetu bali ni yao!
Kingine sidhani kama una ufahamu wowote wa haya mambo ya global warming zaidi ya kusoma kwenye magazeti , kwanza unaelewa chochote kuhusu stiegler gorge na vyanzo vya maji?
Unasema tusiwekeze kwenye umeme wa maji tuangalie vyanzo vingine, ni vipi hivyo ambavyo unafikiri vinaweza kuendena na low level yetu ya sophistication kwa sasa? Unataka twende Nuclear? AK mpaka leo hii wanarumbana na hao hao Wazungu kwa sababu Zuma alitaka kuwekeza kwenye Umeme wa nuclear, sasa unataka tufanye nini?
Kesho tukiongea na Urusi au Mchina aje kujenga Nuclear power plant utaona Wazungu hao hao watapinga, sasa tufanye nini? Embu sema another source of power tunayoweza kuitumia, nitajie moja tu, usilete blah blah tafadhali naomba unitajie moja TU, badala ya hii ya Maji ambayo tutaiweza!
Mwisho elewa kwamba Mzungu hana interest na Afrika yetu iendelee hata siku moja kwani hii ni source of cheap resources, na kwa kukusaidia, kama leo hii Mzungu angetawala TZ ninakuhakikishia angepunguza hizi hifadhi zote na kuwa nazo chache tu nyingine kutumia kwa uzalishaji!
Unafahamu kwamba zaidi ya 35% ya Eneo la JMTZ ni Hifadhi? Sasa nitafutie nchi ya Muzungu ambayo ametenga zaidi ya 30% ya eneo lake kwa ajili ya kufugia wanyama, nitajie moja tu!
Fikiria hili pia!
Unafahamu kwamba USA kulikuwa na Malaria mpka miaka ya 70'? Na wakatumia DDT kuitokomeza, baada ya hapo wakapiga DDT marufuku, na leo hii haturuhusiwi kutumia DDT kuangamiza Malaria wkt Muzungu aliitumia kuangamiza Malaria, sasa ni kwa nini? Taiwani, Eastern Europe na Asians countries waliondoa malaria kwa kutumia DDT lkn Sub saharan Afrika ikapigwa matrufuku na WHO, sasa kwa nini?
Ni kwa sababu Malaria ni business za watu, watu wanauza dawa, hivyo acheni kuwaamini Wazungu hawajawahi kuwatakia mema hata siku moja!