Mnajidanganya nyie, wamarekani licha ya kutokuwa na wanyama wengi kama sisi lakini karibia kila jimbo wana ZOO na wanyama ni hawa hawa wetu tunaojivunia, Tembo, Twiga, Nyani, Chui, na wengine wengi. Wamewatunza vizuri na kuwazalisha, sisi tunazo mbuga za asili na wanyama wa asili sio ZOO. Hao WWF wanatusaidia sisi na wanyama wetu, ushauri wao kwetu ni wa kitaalam sisi tuna leta siasa na ujuaji.
Watalii wengi kutoka huko marekani waliisha waona Twiga, Tembo,Chui na wengine huko huko marekani, hukuk wetu, Tanzania, Kenya, Afrika kusini Namibia wakija wanataka kuwaona wanyama hao kwenye natural habitat zao, na hicho ndicho hao WWF wanakitetea, eti sisi tunawasikiliza wanasiasa wasiofahamu chochote kuhusu ecologia na maisha ya wanyama wetu lakini wanahamasisha UTALII waingize pesa.
Ohoo viwanda, hata hawafahamu wanataka viwanda gani vya kutengeneza nini, kwa teknologia ipi na ya nani kutoka wapi?!
Siasa zenu ziishie bungeni acheni wataalamu wawaambie ukweli.