WWF waponda na kupinga mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge

WWF waponda na kupinga mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge

Tunazo mbuga za kutosha sana ikiwepo Ruaha ambayo ni first or second largest national park in Africa. Eneo litakalomegwa kutoka Selous ni dogo sana kulinganisha na litakalokuwa covered na Dam. Wanyama hasa tembo hawatadhurika.
Mwaka 1993 China walianza ujenzi wa bwawa la umeme (Three Gorges Dam) kwa ajili ya kuzalisha umeme MW 22,500 mradi ambao ulibuniwa mwaka 1919. Wakati wa ujenzi mamia ya watu walifariki, watu zaidi ya milioni 1.3 walihamishwa (sisi tunalalamikia wanyama). China bado wanazalisha umeme wa Nuklia pamoja na makaa ya mawe. China wameendeleza viwanda na kuuza bidhaa zao kwa bei nafuu kutokana na kuwa na umeme mwingi na wanaendelea kujenga Dams nyingine. Tunahitaji umeme wa bei nafuu unaozalishwa kwa maji. Hao WWF wapotelee kwa mbali.
Hahaha ndugu wachina wanateknologia ya viwanda nyingi ilitoka marekani. Sisi hatuna teknologia tunaimba viwanda. Hata wakiua wanyama wote labda hatutaathirika mbona kuna nchi hazina hata zoo lakini zina maendeleo?! Mimi sikatai wasijenge, wao wajenge tu ila pia wasikilize ushauri wa kitaalam.
Hiyo strigler gorge siyo na haitakuwa solution ya umeme Tanzania, na haitaleta wala kurudisha viwanda Tanzania, wanasiasa kuimba ni kawaida na wananchi kuitikia imekua kawaida.
China siyo Tanzania na Tanzania haitakuwa china.
 
Maajabu ya uchuni wa Magufuli pia yapo kwenye kuishadadia sana hii SGR, kama tumekuwa na reli mbili ya meter gauge ya Kati na Tazara, zote zina under perform, tumeanzisha bandari kavu ya Isaka ili ipokee mizigo ya Rwanda, Burundi na DRC, lakini haifunction na reli ya kati ipo, tena hadi eneo la ICD ya Rwanda watu wanalima tuu mahindi!, hii SGR italeta miujiza gani?.
2035 nitarudi kufukua hizi Hoja zako
 
Kwanza hao WWF hawajakataza wameshauri, mkiona ushauri haufai fanyeni kama kawaida yetu, athari tutajijua huko baadaye, isitoshe mawanyama ya nini sisi tunataka umeme wa viwanda, ingawa sijui ni viwanda gani hahaha nchi hii kiboko.
 
Hahaha Tanzania na wadanganyika mnavituko kweli. Mbona huwa mnapanga budget hewa Dodoma, hawa wazungu wana kaa huko Washington DC kujadili mpewe kiasi gani na kwanini ili mkidhi malengo ya budget yenu na huwa hamkatai. Leo hao hao wanawakosoa kwa kuwaonyesha tatizo la mradi wenu mnawaona wajinga.
Mradi wenyewe mnategemea pesa kutoka kwao teknologia mtoe kwao, eti watanzania tunadanganywa na wanasiasa nasi tunajiona wajanja. Hivi ecologia ya asili mkiiharibu mnadani mtaweza kuirudisha nyie. Stigler's Gorge sio mbaya lakini sikilizeni wanaofahamu.
Hahaha mnatumia mbinu na ubabe wa Iran na NK mpewe pesa mbadala ?! Wale wananyuklia nyie mna bonde tu hamtapata pesa hizo, wao wanashauri kwa mazuri yetu ili tusiharibu ecologia ya asili sisi tunajitia vichwa ngumu.
Kila siku tunadanganyana eti umeme wa viwanda, viwanda gani?! Viko wapi?! Vinatengeneza nini?!
Ohoo Trump, kawafanya nini kama sio kujizushia tu, akisema nyie ni shitholes mnakuwa shitholes kweli?! Mara ohoo WWF wako Nairobi, so what?! Mbona maamuzi ya Jerusalem mlipigia kura New york mnajidai mnamisimamo wakati ujinga tu. Sikilizeni wanaofahamu sisi hatufahamu huo ndio ukweli mtaharibu tu.
mbona huwa wanashangilia rais anaposema unaodaiwa ni ukweli hata Kama hakuzingatia utu leo iweje wakasirikie Maneno ya Trump?
 
mbona huwa wanashangilia rais anaposema unaodaiwa ni ukweli hata Kama hakuzingatia utu leo iweje wakasirikie Maneno ya Trump?
Hahaha wadanganyika hawajiamini mpaka wapendwe na Trump. Lakini utawasikia eti tuliwafukuza wakoloni na wanasheherekea uhuru. Sasa Trump hawapendi sijui wanakosa nini?! Na huyo Trump akiwapenda sijui ndio watajiona ni binadamu?! Ninavyohisi siku Trump akisema anaipenda afrika anakuja kuitawala, miafrika italipuka kwa furaha, inapenda kupendwa na wazungu balaa hahaha
 
Sikubaliani na WWF wala serikari katika kuangalia mahitaji ya umeme na maslahi mapana ya taifa.

Nishati ndio nguzo ya stability kwenye kujenga uchumi na maendeleo ya jamii nchi yoyote makini katika sera muhimu za taifa energy security ndio top of the agenda hiyo ainaga mjadala ata serikari zinapobadilika.

Matiafa yote yaliyopiga hatua kubwa za maendeleo ukipekuwa utakuta wanazalisha kutumia the most pollutant source ambayo ni makaa ya mawe kati ya 60%-80% ya total energy output. To put into perspective USA and UK respectively 70% ya chanzo cha umeme wao ni makaa ya mawe one US household uses 10 times of their counterparts moreover the Washington subway system alone uses enough energy to power the whole city of Geneva.

Na hao watu wala hawana mpango wa kuachana na hivyo vyanzo hivi karibuni ndio kwanza Trump kajitoa kwenye Paris agreement, wachina ndio uwaambi lolote kwenye makaa ya mawe na UK badala ya kupunguza ndio wanaongeza kimya kimya. Kwanini makaa ya mawe ni cheap source to run, more reliable than any other source (an important factor in stability of supply) katika mataifa yaliyoweka kipaumbele uchumi wao and over the long term it the best investment in terms of value for money.

Nimejaribu kutafuta energy security policy yetu online sijaona something which came close to it is "POWER SYSTEM MASTER PLAN 2012 UPDATE" ambayo inazungumzia pretty much aspects za energy policy za Tanzania mpaka 2036 humo ndani utaona kuna prediction za population growth za sehmu mbali mbali na technical aspects za energy policy ambazo kwakweli zinaridhisha na makaa ya mawe yamepewa sehemu kubwa ya uzalishaji kufikia capacity planned.

Leo hii watu walioandaa huo mkakati kama Eliakim C. Maswi, James Andilile, Eng. Innocent Luoga and na timu yao ya ufundi kutoka TANESCO sidhani kama wanaimpact tena japo kwenye ushauri wa policy yao. Inaonekana waliokuja wamekuja na agenda nyingine na mkakati mwingine.

Tayari tunazalisha umeme wa maporoko Pangani na Mtera na tumeshaona sio reliable source ni kwasababu hizi hizi ndio maana nchi zilizoendelea awaupi kipaumbele China Yangtze river unaweza ufananisha na Nile tu kwa ukubwa na wanamito mitatu kama hiyo umeme wamaporoko kama reliable kwanini wasiongeze na wana means and resources au USA wana great river ngapi ya kufanya miradi ya umeme wa maji.

Sisi waafrika ni watu wenye matatizo sana kutaka kukimbia ata kutembea vizuri atujaweza Stiegler's Gorge' ni bad investment na sio kitu tunachoitaji kwa sasa, what we need are more reliable sources na vyanzo vyake tunavyo vya kutosha. Alieturoga kesha kufa
nimekuelewa sana boss!
 
Sina ushabiki mkuu, nionyeshe hiyo link. Over
Hakuna link hapo....watu wakurupuka tu kujadili mada pasi na kusoma kwanza rejea zilizowekwa. Hii yaonesha namna watu wengi walivyo wavivu ktk usomaji. Na muanzisha mada mwenyewe akiombwa link awa mkaliiii na akunasibisha na CCM!
 
Hawa WWF wakafie mbali!, kwa sababu uamuzi kuhusu Mradi huu, umeishafikiwa, hivyo uhamasishaji wa mjadala huu ni too little too late!.

Hoja za msingi za WWF ni hizi

  1. Mradi huu utaathiri Selous Game Reserve ambayo ni moja ya World Heritage Sites hivyo ujenzi katika eneo hili utaathiri ecology ya Selous kwa kuathiri mazingira, yatakayoathiri uchumi na maisha ya watu, hoja hii inakuwa defeated na manufaa ya Mradi huo ukilinganisha na athari za Mradi huo, manufaa ni makubwa mara 1000 kuliko athari!.
  2. Eneo litakalotumika ni kilomita za mraba 1,200km2, hivyo kulifanya kuwa bwawa kubwa kuliko yote eneo la Afrika Mashariki, hivyo litakausha maziwa madogo madogo yote ya jirani, litaathiri utalii, na kukomba fertility yote ya Ardhi ya eneo hilo hadi kwenye Delta ya Rufiji Delta, hivyo kuua samaki, na kuathiri uvuvi wa Kamba samaki na kamba koche unaotegemewa ka watu 200,000 wa eneo hili, pia hoja hii inapigwa chini kwa hoja kuwa Tanzania tuna maeneo mengi ambayo ni waste land, what is km za mraba 1,200?. Hao watu 200,000 watakaothiriwa na Mradi huo ni nini ukilinganisha na Wamasai wanaishi ndani ya eneo la hifadhi ya Loliondo ambao hawaruhusiwi kulima, bali wanalishwa bure?. Kwa vile faida za Mradi ni kubwa, serikali inaweza kuwaambia watu hao 200,000 wasilime na badala yake watalishwa bure maisha yao yote, hivyo Mradi uendelee!.
  3. Mradi unaelezwa unakwenda kinyume cha mikataba ya kulinda World Heritage ambayo Tanzania tumesaini, this also is nothing!, Tanzania tumesaini mikataba kibao ya kimataifa ya haki za binaadamu na kila siku serikali inakiuka mikataba hiyo, kama rais Magufuli, ameikanyaga katiba alioapa kuilinda, what are the chances kuheshimu mikataba ya kimataifa kama itatuzuia kupata manufaa, to hell with mikataba ya kimataifa at the expense of development.
  4. Mradi huo utaazuia tani milioni 16.6 za virutubisho vya Ardhi kwa mwaka, hivyo kusababisha mmomonyoko wa Ardhi kwenye Delta ya Rufiji, hii pia sio hoja, kwa ukubwa wa ardhi ya Tanzania, shughuli za kibinaadamu kama uchimbaji wa madini, unaleta athari kubwa zaidi za kimazingira na kusababisha sio tuu mmomonyoko Mkubwa wa Ardhi, bali kutuachia mahandaki mengi na makubwa Zaidi kuliko hizo tani milioni 16.6 kwa mwaka, hivyo Mradi utaendelea!.
  5. Hoja kuwa Mradi huo utaathiri sio tuu Mbuga ya Selous, bali pia Delta ya Rufiji na Bonde la Mto Kilombero, hapa tena tunaangalia faida za Mradi na kulinganisha na athari za kimazingira, then faida za Mradi ni kubwa kuliko athari!, Mradi utaendelea!.
  6. Hawa wazungu na wana mazingira ni watu wa ajabu sana, nakumbuka walivyotucheleweshea Mradi wa Kihasi kwa ajili tuu ya vyura wa Kihansi hadi Marekani walipokubali kuwahamisha vyura hao hao kuwahifadhi nchini Marekani, kisha kuwarudisha ndipo Mradi ukapitishwa!, yaani vyura walikwamisha mradi muhimu, ujinga huu walimfanyia Nyerere na Mwinyi, lakini kwa Magufuli, watagonga mwamba!.
  7. Hata Mradi wa Kamba Samaki kwenye Delta ya Rufiji, ulikwamishwa na wanamazingira kwa hoja kuwa Mradi huo utaathiri hifadhi ya miyombo!, what is miyombo compared to manufaa ya kiuchumi?.
  8. They can just go to hell, kama katiba ya Tanzania imekanywagwa for the expense ya maendeleo, rais Magufuli aliruhusu tuachane na na hizi EIA katika kupushi Tanzania ya Viwanda, hivyo sasa hapa ni kazi tuu, hakuna cha mazingira, world heritage wala cha nini, Tanzania tunataka Umeme wa kutosha kuendeshea Tanzania ya viwanda!
Hoja zote hizo ni katika kulinda kitu kinachoitwa the sovereignty of our nationalism kwamba Tanzania ni ya Watanzania, tuna uhuru wa kupanga mambo yetu kwa manufaa yetu bila kuingiliwa na mtu mwingine yoyote, hivyo hawa WWF, wasituingilie!.

Lakini on the other hand, kiukweli kabisa japo mimi sio mchumi, lakini sera za uchumi za serikali ya Magufuli ni sera za ajabu sana!.
  1. Huu Mradi wa Umeme wa Stglers Gorge ulizungumzwa tangu Enzi za Nyerere na haukutekelezwa kutokana na hixo hizo environmental concerns na mpango wa Tanzania Power System Master Plan (2016 update), umeonyesha Mradi huu ndio the last option kama miradi mingine mikubwa itashindikana, Mradi wa priority ni Umeme wa kutumia gesi, lakini sasa Magufuli kaingia, mara ghafla hatuzungumzii tena Mradi wa Umeme wa gesi, sasa Mradi huu ndio kipaumbele!, kipaumbele for what?.
  2. Japo ni kweli, the cheapest power generation projects ni hydropower projects, lakini Tanzania hatujifunzi tuu, kutokana na global warming na mabadiliko ya tabia nchi, kuendelea kutegemea Umeme wa maji ni very unpredictable, Richmond ilisababishwa na hii over dependency on hydropower, hivyo kulipotokea ukame, kilichotukuta sote tunakijua!, sasa gesi tunayo tena ya kutosha, na Umeme wa gesi, japo ni expensive kuliko hydro ni cheap kuliko diesel generation, kwa nini tusijikite kwenye gesi yenye uhakika, tunataka kuzamisha matrilioni ya Fedha kwenye pata potea nyingine ya kutegemea mvua?.
  3. Maajabu ya uchuni wa Magufuli pia yapo kwenye kuishadadia sana hii SGR, kama tumekuwa na reli mbili ya meter gauge ya Kati na Tazara, zote zina under perform, tumeanzisha bandari kavu ya Isaka ili ipokee mizigo ya Rwanda, Burundi na DRC, lakini haifunction na reli ya kati ipo, tena hadi eneo la ICD ya Rwanda watu wanalima tuu mahindi!, hii SGR italeta miujiza gani?.
  4. Uchumi wa Tanzania unategemea kilimo, hivyo Tanzania ya kweli ya viwanda, ni Tanzania ya agro processing industries, tunahubiri Tanzania ya viwanda, bila kuinua sekta ya kilimo, hivyo viwanda ni malighafi gani ya kuendesha Tanzania ya viwanda kama sekta ya kilimo ni totally neglected, Magufuli yuko bize kununua ndege na kujenga miundombinu, what has ndege, barabara za juu kwa juu, uwanja wa ndege wa Chato, na hii SGR has to do with sekta ya kilimo?.
Mimi bado nasisititiza, Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!.

Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed Deposit na Faida ya Fedha Kukaa tu BoT

Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136!

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa kiuchumi?

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi?.

P
Kwa hiyo Paskali kwako wewe mazingira si lolote si chochote, ila uchumi tu?
Hujali athari zozote za mazingira. Unadhani Tanzania inao uwezo wa kukabiliana na athari hizo?
Nchi zilizoendelea kwa sasa zinaachana na matumizi ya vyanzo vya nishati vinavuoharibu mazingira, kwa mfano nchi za Ujerumani na Ufaransa zinaachana na nuclear energy na kuingia kwenye solar.
Hata mkaa wa mawe sasa haaatumii tena.
Halafu unapongeza uvunjifu wa katiba na mikataba ya kkmataifa ya haki za binadamu? Tulisaini ya nini sasa?
Hapo ndipo ninapotilia shaka uwezo wako wa kufikiri
 
Hawa WWF wakafie mbali!, kwa sababu uamuzi kuhusu Mradi huu, umeishafikiwa, hivyo uhamasishaji wa mjadala huu ni too little too late!.

Hoja za msingi za WWF ni hizi ........

3. Mradi unaelezwa unakwenda kinyume cha mikataba ya kulinda World Heritage ambayo Tanzania tumesaini, this also is nothing!, Tanzania tumesaini mikataba kibao ya kimataifa ya haki za binaadamu na kila siku serikali inakiuka mikataba hiyo, kama rais Magufuli, ameikanyaga katiba alioapa kuilinda, what are the chances kuheshimu mikataba ya kimataifa kama itatuzuia kupata manufaa, to hell with mikataba ya kimataifa at the expense of development.​


P
Hapo namba tatu sijakuelewa
 
Tatizo ni kwamba athari za kimazingira huwa tunazidharau sana hasa kwa nchi changa kama yetu.

Sitaki kuamini kwamba huu umeme ndio mkombozi wa viwanda ikiwa bonde la rufiji liko hayaoni kupotea. Sijui kilimo kitafanyikaje, sijui wanyama wataishi wapi huku tukiwa tunasubiria utalii.

Mabadiliko ya tabia ya nchi athari zake zipo wazi, kwan wahanga ni sisi wa nchi maskini afu Leo tinatengeneza matatizo makubwa zaidi kwa kuua mabonge yetu.
 
Honestly naona umetoa maelezo mazuri lakini sijaona kama umetoa maelezo nikaridhika kutokana na mahitaji yangu. Yaani ni kama nimetaka kujua habari za Tanga, lakini ukaniletea habari za Morogoro kwa ufasaha. Anyway ngoja niridhike na maelezo yako, lakini bado hujakidhi haja yangu kama nilivyotarajia.
Yawezekana nilikuweka higher wakati ulihitaji maelezo ya chini chini. Kwa ufupi energy kwa nchi inatakiwa iwe diversified ili ujihakikishie usalama. Kwa TZ tuna gesi na hydro. Hata kama gesi inakidhi na kuzidi mahitaji yako, bado tafuta njia nyingine ili ujikinge. TZ bado tuko chini ya mahitaji yetu na siyo busara kukubaliana na WWF eti kuna njia mbadala, ipi? Gesi ipo na hata ikitosha bado tunahitaji hydro.
 
Tatizo ni kwamba athari za kimazingira huwa tunazidharau sana hasa kwa nchi changa kama yetu.

Sitaki kuamini kwamba huu umeme ndio mkombozi wa viwanda ikiwa bonde la rufiji liko hayaoni kupotea. Sijui kilimo kitafanyikaje, sijui wanyama wataishi wapi huku tukiwa tunasubiria utalii.

Mabadiliko ya tabia ya nchi athari zake zipo wazi, kwan wahanga ni sisi wa nchi maskini afu Leo tinatengeneza matatizo makubwa zaidi kwa kuua mabonge yetu.
Hiyo inaeleweka Duniani, kwamba ukiwa nyuma kimaendeleo suala la mazingira huwa siyo muhimu. Ukiendelea hapo ndo madhala ya mazingira huanza kuonekana na unachukuwa hatua.

Wana JF tunapoandika taarifa za mambo muhimu kama haya na kujadiliana tuseme kwa viwango. Unaposema matatizo ya ya mabadiliko ya tabia nchi athari zake zipo wazi. athari hizo ni zipi? Angalia WWF walivyoshindwa kuonyesha uhusiano wa Madaliko ya Tabia nchi na mradi wanaoupinga. Ni bhla-bhla tu, wanataja hili na lile. Nawe unataja kwamba ziko wazi, wapi? hapa TZ? Duniani? au wapi? Zinahusu nini kwenye mradi?
 
Tunazo mbuga za kutosha sana ikiwepo Ruaha ambayo ni first or second largest national park in Africa. Eneo litakalomegwa kutoka Selous ni dogo sana kulinganisha na litakalokuwa covered na Dam. Wanyama hasa tembo hawatadhurika.
Mwaka 1993 China walianza ujenzi wa bwawa la umeme (Three Gorges Dam) kwa ajili ya kuzalisha umeme MW 22,500 mradi ambao ulibuniwa mwaka 1919. Wakati wa ujenzi mamia ya watu walifariki, watu zaidi ya milioni 1.3 walihamishwa (sisi tunalalamikia wanyama). China bado wanazalisha umeme wa Nuklia pamoja na makaa ya mawe. China wameendeleza viwanda na kuuza bidhaa zao kwa bei nafuu kutokana na kuwa na umeme mwingi na wanaendelea kujenga Dams nyingine. Tunahitaji umeme wa bei nafuu unaozalishwa kwa maji. Hao WWF wapotelee kwa mbali.
Nadhani yabidi tuwaulize misitu yao na mbuga zao za wanyama walipeleka wapi? Wanataka Afrika iendelee kuwa 'shithole' wawe wanakuja kutuona na kutulinganisha na nyani wa msituni kwa ufukara wetu. NO! NO!
 
Mnajidanganya nyie, wamarekani licha ya kutokuwa na wanyama wengi kama sisi lakini karibia kila jimbo wana ZOO na wanyama ni hawa hawa wetu tunaojivunia, Tembo, Twiga, Nyani, Chui, na wengine wengi. Wamewatunza vizuri na kuwazalisha, sisi tunazo mbuga za asili na wanyama wa asili sio ZOO. Hao WWF wanatusaidia sisi na wanyama wetu, ushauri wao kwetu ni wa kitaalam sisi tuna leta siasa na ujuaji.
Watalii wengi kutoka huko marekani waliisha waona Twiga, Tembo,Chui na wengine huko huko marekani, hukuk wetu, Tanzania, Kenya, Afrika kusini Namibia wakija wanataka kuwaona wanyama hao kwenye natural habitat zao, na hicho ndicho hao WWF wanakitetea, eti sisi tunawasikiliza wanasiasa wasiofahamu chochote kuhusu ecologia na maisha ya wanyama wetu lakini wanahamasisha UTALII waingize pesa.
Ohoo viwanda, hata hawafahamu wanataka viwanda gani vya kutengeneza nini, kwa teknologia ipi na ya nani kutoka wapi?!
Siasa zenu ziishie bungeni acheni wataalamu wawaambie ukweli.
Mambo ya Wamarekani na zoo hayatuhusu jamani! Au unatuonyesha unaifahamu Marekani? Taarifa ya WWF ina utalaamu gani? Hakuna lolote ni Bhla-bhla tu! Athali gani waliyoionesha na hiyo itatokea kwa njia gani? Ukiwa mtaalamu, lete taarifa ya kitaalamu.
 
Tunawabishia ili hali ndio hao hao wanatuuzia na kutufundisha kutumia vifaa ili TMA watuambie kuwa kesho mvua itanyesha juu/chini ya wastani, bahari itachafuka n.k.

Wanatuambia tutaharibu ecolojia tunang'aka as if tunazo mbinu mbadala.

Hata sijui nikae upande gani, zaidi ya kungoja tu siku zangu ziishe nikaangangalie hayo makazi mapya.
 
Mwacheni dereva aendeshe gari anajua kona na mashimo ya barabara
 
Hapo namba tatu sijakuelewa
hujaelewa nini hapa?.
  1. Mradi unaelezwa unakwenda kinyume cha mikataba ya kulinda World Heritage ambayo Tanzania tumesaini, this also is nothing!,
  2. Tanzania tumesaini mikataba kibao ya kimataifa ya haki za binaadamu na kila siku serikali inakiuka mikataba hiyo,
  3. kama rais Magufuli, ameikanyaga katiba alioapa kuilinda, what are the chances kuheshimu mikataba ya kimataifa kama itatuzuia kupata manufaa,
  4. to hell with mikataba ya kimataifa at the expense of development.
P.
 
Kwa hiyo Paskali kwako wewe mazingira si lolote si chochote, ila uchumi tu?
Hujali athari zozote za mazingira. Unadhani Tanzania inao uwezo wa kukabiliana na athari hizo?
Halafu unapongeza uvunjifu wa katiba na mikataba ya kkmataifa ya haki za binadamu? Tulisaini ya nini sasa?
Hapo ndipo ninapotilia shaka uwezo wako wa kufikiri
Mkuu Kidamva, umekuwa too subjective kuwa kwangu mazingira si lolote, si chochote na kuwa sijali athari zozote za mazingira!, kisha ninapongeza uvunjifu wa katiba na mikataba ya kimataifa ya haki za binaadamu...
Hapa ni suala la uelewa tuu. kitu nilichofanya nimekuwekea jinsi hoja za WWF zitakavyopanguliwa, na hoja zangu nimeziweka pande mbili, on government perspective na my take.
Ruksa kabisa kutia shaka uwezo wangu wa kufikiri, kwa watu wote ambao uwezo wao wa kuelewa unatia shaka!.

P.
 
Hahahahah nimewastukia wazungu wanataka tuendelee kuwategemea kila kitu
 
Back
Top Bottom