Ya Adani na Wachina: Hii ndiyo sababu kuu inayofanya Wanasiasa wetu wawachukie Wazungu

Kusema kweli ili tuendelee tunawahitaji sana Wazungu kuliko hawa wachina na wahindi wanaojenga miradi ya hovyo iliyo chini ya kiwango tena kwa pesa nyingi ambazo zinaenda kutumika kama Rushwa kuwanufaisha wachache.
Tatizo ni nyinyi wenye miradi mnataka 10% Mchina hana tatizo
 
Nakubaliana na wewe isipokuwa kuchoma nyumba hicho kitu sahau watanzania mazuzu.
 
Unakumbuka enzi za Magufuli hadi HISA za Barrick ziliporomoka sana huko duniani baada ya ile report kutoka? Barrick pia wamekua wanalalamikiwa huko huko Ulaya kwa madhambi wanayo yafanya Africa na America kusini. Wazungu wamenyooka, Wahindi na Wachina HAPANA
Wote wale wale tu wazungu wenyewe wanatoa hongo kuoata tenda.
Hukuona ile report ya malipo ya barick yasiyo kuwa na maelezo hapa nchini.
 
Eti "Wanasiasa wanachukia wazungu"

Hebu tuwekee makala yeyote ile au matamshi ikionyesha/yakionyesha Wanasiasa wa Tanzania wakiwa wanawachukia wazungu??


Uzi kama huu huwa una lengo la kuwachonganisha Waafrika na Wahindi na Wachina.

Piganeni wenyewe huko, msituingize Waafrika kwenye vita zenu na fikra za Ubeberu. Rushwa or Not
 
Umezungumza ukweli wa 100%, na hii unayoona viongozi wanaingia kwa chaguzi za wizi, njia zote chafu ni ili kulinda maslahi yao yanayopatikana kwa njia ya rushwa. Na kwenye rushwa hizi wanakula viongozi wa kisiasa na wa vyombo vya dola, ili kulindana katika madaraka.
 
Kwa hiyo wazungu hawatoi rushwa na hawali rushwa?
Hakuna paliposemwa Wazungu hawatoi Rushwa, wanatoa ila kutokana na nchi zao kuwa na mifumo imara ya checks and balance wanaogopa sana kutoa Rushwa na ndo mana Viongozi wa Kitanzania na Afrika kwa ujumla hawawapendi
 
Magulification must go on to root out the scourge of Corruption in the African Continent.

Lead by Big Wazungu, Wahindi na Waarabu Cooperation. And Big Companies.
 
Ndio anapindisha hivyo. Wazungu wamekula Rushwa kutoka kwa Adani, anawasingizia Waafrika.

Wazungu ni watoa Rushwa na wala rushea namba moja Duniani. piga ua
Elewa mada acha kukurupuka.

Mbona imeelezwa kuhusu walivyotupiga kwenye manunuzi ya Rada kipindi cha Mkapa?

Uzi unazungumziq namna walivyokuwa na mifumo thabiti ya cheks and balances kiasi ambacho hata kampuni zao zimekuwa zikiogopa sana kutoa Rushwa.

Mzungu akitoa Rushwa kuna mfumo wa kumchunguza kwenye nchi yake. Na anaweza kubanwa na mpaka kuchukuliwa hatua. Hili limewafanya waogope sana kutoa Rushwa hivi karibuni
 
Umeishia darasa la ngapi?
 
Kwa Viongozi ipo hivi km ulikua haujui kwenye masuala ya Uchaguzi ngoja nikutoe tongotongo mfano chama A kipo madarakani km chama tawala halafu chama B kipo km chama pinzani, sasa ikitokea mgombea wa chama B ana nguvu kuliko mgombea wa chama A yaan wananchi wanamkubari sana mgombea wa chama B ambae yupo upinzani na kwenye sanduku la kura kweli wote wakampigia mgombea wa chama B ambae ni wa chama pinzani, nikuambie kitu kinachofanywa na viongozi wa Afrika ni kwamba Mwananchi hana haki wao viongozi waliopo madarakani ndio wenye haki kwa hio ikitokea wapiga kura wakampigia kura zote mgombea wa chama pinzani wanatumia nguvu ya Dola kumuweka mtu wao wanaemtaka wao kwa kumtumia msimamizI wa kutangaza matokeo ya uchaguzi wanachompa ni security tu kwamba ukitangaza tutakulinda viongozi na Wananchi hawana haki kwa hio wataamua waende wakashtaki wanapopajua maana wakienda mahakamani ndio km unaenda kushtaki kesi ya nyani kwa ngedere
 
Mapovu hayakusaidii chochote, utendaji wetu ni takataka kama wewe umechukulia kuwa wewe ni takataka hayo ni matatizo yako binafsi.

Sisi tunayo matatizo yetu mengi tu, inferiority complex zetu zinatudanganya kwamba kila mtu ni adui ya maendeleo yetu wakati adui wa kwanza ni hulka zetu wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…