Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Pamoja na yote Mzungu ni mtu aliyenyooka sana!
Mzungu kawekeza sana kwenye suala la utawala bora ambapo kupitia utawala bora amejenga Taasisi na mifumo imara sana zinazosimamia mambo na kuhakikisha yanaenda bila shida.
Kunyooka huku kwa Mzungu ndiko kumefanya sasa aanze kupoteza sana Africa. Hii ni kwa sababu Viongozi wa Afrika wanapenda sana Rushwa. Kupenda Rushwa kwa Viongozi wa Afrika ndiko kumefanya kwa sasa bara la Africa kuongoza kwa uwekezaji wa Wachina na Wahindi.
Mchina na Mhindi ni watu wanaoamini kuwa ili jambo lake liende lazima atoe Rushwa. Endapo siku ikitokea ukafanyika uchunguzi huru wa namna kandarasi za Wachina na Wahindi zinavyopatikana hapa Tanzania na Afrika nawaambia wananchi wetu wanaweza choma nyumba zote za Viongozi wetu sio tu Tanzania bali Afrika nzima.
Waendesha Mashtaka wa Marekani kufungua Mashtaka dhidi ya tajiri wa kihindi Adani ni funzo kubwa kwetu kuwekeza kwenye katiba bora inayojenga na inayosimamia mifumo imara. Mifumo isiyotoa nafasi kwa rushwa na kuhakikisha fedha zote za walipakodi zinatumika kwa maendeleo ya wananchi tu na sio kuwanufaisha wachache.
Hapa Tanzania Adani kapewa sehemu ya Bandari yetu. Huwezi sikia hata siku moja PCCB wakifanya uchunguzi. Na kamwe hatutosikia. Hii ni kwa sababu Adani ameingia Tanzania kupitia Ofisi namba moja.
Sio mara ya kwanza kwa mzungu kuonyesha umuhimu wa Mifumo na Taasisi imara kwenye utawala bora. Tanzania tulishawahi rudishiwa chenji yetu ya Rada baada ya Wazungu kugundua kuwa kampuni zao zilitupiga na wakazibana zikarudisha kweli.
Kuna kipindi Bandarini Wazungu waligundua kuna kampuni zao zilitoa Rushwa kupata tenda za kufunga mifumo ya tehama kwenye Bandari yetu. Ila pamoja na Ile kampuni kubanwa nchini mwao hapa kwetu hatujasikia hadi leo wahusika wakifikishwa Mahakamani.
Kusema kweli ili tuendelee tunawahitaji sana Wazungu kuliko hawa wachina na wahindi wanaojenga miradi ya hovyo iliyo chini ya kiwango tena kwa pesa nyingi ambazo zinaenda kutumika kama Rushwa kuwanufaisha wachache.
Najua huu uzi hautapata wachangiaji wengi kwa sababu Watanzania wengi ni mazuzu. Hawaelewi unyeti wa kodi zao na wanawaona wanasiasa kama miungu ambao wanaweza fanya chochote na hela zao bila kuhojiwa au kufanywa chochote.
Ipo siku
Lord denning
Qatar