Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 529
- 1,150
Kumekucha kumekucha
Gambo
Mkuu Gambo kaambiwa maneno machache tuu, ‘Hudhuria kwenye vikao’ almanusura adondoke chini kwa shambulizi la moyo. Nikagundua kumbe alikuwa yupo mbele ya wateja wake a.k.a wapiga kura. Maneno ya RC yamemchoma sana mwanaume huyu; chupa ya chai ya wanawe imepokea mguso na kitisho, lazima apige yowe. Naona anatoa maelezo mengi sana mtu huyu, hakika ni mwanaume wa kweli, chai ya watoto ipo hatarini, yowe lazima lipigwe.
Mbowe
Baada ya Tundu Lissu a.k.a Apostle Mwamposa wa siasa za Tanzania kuanza kukishikashika kichwa cha Mbowe (kwenye paji la uso) na kukiachia kama afanyavyo Mwamposa kwenye maombezi, napo yowe limeanza kusikika.
Msaidizi: Apostle!, unavyogusa na kukiachia kichwa cha mtu huyu tunaona muujiza ukitendeka.
Mwamposa: Muujeza gaaani unatendeka?
Msaidizi: Anapiga yowe huku amekumbatia chupa ya chai
Mwamposa: Yumkini, chupa yake ya chai imepata mguso usojulikana
Msaidizi: Hii ina maana gani Apostle?
Mwamposa: Ne mwanaume wa kweli mtu huyu, chai ya Watoto ekiguswa, lazima apige yowe, mwacheni apige yowe.
Msaidizi: Piga yowe piga yowe mwanaume, onesha uanaume wako kwa kupiga yowe.