Ya msanii Mabeste na mkewe hutokea pale mwanamke anapomzidi akili mumewe

Ya msanii Mabeste na mkewe hutokea pale mwanamke anapomzidi akili mumewe

Mkuu inaonekana, umefurahi sana juu ya swala la kuvunjika kwa ndoa yao.Nikiangalia comments zako nyingi nagudua kuwa umekaa kiushabiki sana, sishangai sana kwakua huku ndo dunia ilipofikia.Ningependa ukumbuke kitu kimoja, ya mwenzako yasikie ila omba sana yasikupate.Ilitakiwa utulie na upate cha kujifunza na sio kushabikia unless uwe unalipwa.Be humbled.
Hata nisiposhabikia, kama yangu ni ya kwenda kombo yataenda tu, kwani Mabeste na Mkewe walishabikia ya nani?

Sijafurahi ila nimejifunza kitu katika suala lao na nimeliweka wazi kwenye uzi huu. Sasa sijui unataka kunichagulia cha kujifunza!
 
Hata nisiposhabikia, kama yangu ni ya kwenda kombo yataenda tu, kwani Mabeste na Mkewe walishabikia ya nani?

Sijafurahi ila nimejifunza kitu katika suala lao na nimeliweka wazi kwenye uzi huu. Sasa sijui unataka kunichagulia cha kujifunza!
Nimekuelewa, siwez kukuchagulia cha kujifunza.Ikitokea yakwako yameenda kombo pia, usisahau kufungua uzi, ili na sisi tufurahie kidogo mkuu.
 
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la kuaibishana au kusemana mtandaoni kwa wanandoa ambao wameshafeli kwenye union zao.

Tulishuhudia Mihayo Wilmore na mkewe wakishambuliana mmoja kwenye podcast ya Men Men Men, mwingine akahojiwa na Clouds pamoja na kuvujisha video.

Kisha msanii Stamina akatoa wimbo pamoja na kufanya interview akieleza wazi wazi kuwa kachapiwa na hataki iwe siri ya ndani na akamtaja alommega mkewe kuwa eti ni mchezaji wa Simba.

Wakati bado anga lina vumbi ikaja issue ya Msanii Venance William 'Mabeste' na Mkewe Lisa Karl Fickenscher kuwasuprise fans kuwa wameshatalikiana huku kila mmoja akivuta kamba upande wake kuwa kaonewa.

Niliangalia interview za hawa watu wawili na ninachoweza kusema ni kuwa Mabeste alioa mke asiye level zake especially kiakili.

Sijui yupi ni mkweli kati yao, ila Lisa hata anavyojieleza tu you can tell alimzidi akili Mabeste. Sijasema ana akili saana ila zikiwekwa zake na mabeste kwenye mzani tofauti ni kubwa sana na hapo ndo tatizo lilipoanzia.

Huyu dada anajua kupangilia maneno, ana the right facial expression, hajajichanganya hata kidogo, hajaonesha chuki wala kupiga ngenga, kwa kifupi kamuaibisha Mabeste with class kwa kupitia kwenye weakness zake na kujifanya kama vile hana shida nazo kumbe ndo anatoboa meli.

Mabeste on the other hand, kakimbilia lile lile ambalo wanaume wote hukimbilia, "ooh kaenda kuwa na rafiki yangu, tulikula Christmas kwao". (Kwanza wanaume mtambue tu, ukimuacha mkeo probability ya yeye kuwa na rafiki yako ni kubwa sana hasa akiwa jembe. Kwa sababu wenzio kwani hawana macho? Unadhani hawakuonei wivu unavyofaidi?)

Kisha Lisa kuhusu hilo suala ameclarify, kuwa huyo rafiki alikuwa rafiki yake yeye kwanza na Mabeste ndo akamjua. So Mabeste amebaki hana claim. Alitumia a very weak point.

Mabeste anasema "sijashirikishwa shule anayoenda kusoma mwanangu naambiwa tu kuwa kaenda shule, sijaambiwa natoaje matunzo". Yani amecheza mule mule kwenye story ya Lisa kuwa Mabeste ni Marioo hawajibiki.

Wanaume, tafuta mwanamke unayemmudu kiakili or else utalialia weeh na kusema wamemchukua sababu ya pesa, wamemchukua sababu ya mali kumbe hukutosha kiakili.

Wasalaam




Kuna video anadai kuumwa kwake alilogwa na ndugu... Au sijaelewa vizuri??!!

All in all mwanamke hadi anakuacha huwa anaandaa point za kujitetea mapema sana, kiasi kwamba anaweza neutralize mazuri yote uliyowahi kumfanyia kwa kosa moja tuu... So sishangai kuonekana anapoint nyingi.

Hawezi kupata akili ya kujitetea kwa sasa sababu moja kwa moja kisaikolojia hayupo sawa hata ukimuona anavyoongea...

Na mwanamke wake kwa alichofanya hatokuja kuamini kikimrudia, kama alichofanya ni sahihi tutajua. Kama Ayubu pia mke wake alivyoona anapitia msoto hadi akafikia hatua akamshauri mume wake aache kumtumikia Mungu wake... Lakini alibaki mpaka jamaa alivyo barikiwa tena.

So ni kwaakili ipi aliyo tumia Lisa... What if uamizi wake ungemfanya mzazi mwenzie ajiue??

How come umeolewa ndoa ya kanisani alafu bado unaomba Mungu akule Mwanaume mwingine...

Karma is a bitch who f#ks every body...


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna cha akili wala nini mwanamke kupangalia maneno ndo akili halafu mabeste wala hakutaka kueleza juu ya maisha yao ila alieleza kwanini ndoa yao ilivunjika kwa sababu watu wengi walivutiwa na ndoa yao na pia walitaka kujua nini kiliwasibu, huyo mwanamke kuona kaumbuka kutoka na rafiki wa mabeste ndo anajieleza story za uongo na kweli kwani ni uongo haishi na huyo rafiki wa mabeste au ndio hiyo akili unayoisema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nakubali kuwa Mabeste alizidiwa akili. Kama sio akili basi tupunguze tuseme uwezo wa kujieleza.
 
Kuna wanawake wengi waliozidi akili waume zao lakini hawajachana. Michelle Obama alikuwa law practice teacher wa Barrack na walichanganya akili zao kufika walipofika.
Wale walimu wangu wa primary waliostaafu wakaoa wake wenye umri mdogo na kuwa walevi hawawezi nizidi akili hata kama walinifundisha. Sekondari kuna walimu wawili nina akika hawanifikii popote kwa vitendo wanavyofanya na wanavyoendesha maisha yao.
 
Hamna sababu ya msingi hapo. Tatizo ni kuchokana tu na mmoja akishamchoka mwenzie basi atatafuta sababu au kuanza visa.

Mitandao imefanya wanawake na mabinti wawe exposed sana so hata kama mwanamke kaolewa anakua bado anajiachia sana na jamaa wengine wakimuona wataanza kuingilia ndoa ya watu

Wanawake zamani hata kutoka tu kwao ilikua ni mpaka awe na ruhusa ya mzazi au mme wake, hii ilisaidia kufanya asionekane sana kwa wasiohusika nae lkn siku hz kama usipomuona mtaani basi utamuona fb, insta au kwenye videos pendwa
Nina jaribu Sana kumuweka mama watoto mbali na mitandao ya kijamii na kuto kumfanya awe mtembeaji pasina sababu za msing na kumjengea mazoea ya kuto kuvaa nguo zisizo na staha na ze matamanio

Tunachokosea Ni kwamba wanaume tunataka kuwa sawa na wanawake yaaan Kama mnafanya Kaz Basi 50/50 nyumbani

Hapo lazima utawaliwe tu na akupande na afanye atakavyo wanaume tunakimbia majukumu yetu Yale halisi mke wangu Ni mtumish ila nilishamwambia huna hela ya kulisha familia yangu Wala kusomesha hvyo visent vyako nunua vocha na ukizingua nakupiga chini naweka mwingne fanya upumbavu wako ila nisijue tu nikigundua tu hakuna Cha nn Ni kupiga chin TU

Mpka Leo heshima na adabu na amenyooka tutafute hela wanaume ukileta romantic love kwa mkeo atakusumbua Sana Tena Sana na hich ndio huwaponza vijana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Too bad mimi ni sexist, nikichangia huu uzi nitakuwa biased kinoma noma..
 
Wanaume wa siku hizi mnakosea wapi? Akili huwa mnaziacha wapi wakati wa kuchagua mke?
 
Back
Top Bottom