Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 35,566
- 104,386
- Thread starter
- #21
😁😁😁Hizi gari naona huku kwetu bado sana. Sisi gari zetu ni multi-purpose, maana kuna muda inakuwa gari ya mkaa, kuna muda inakuwa kikapu cha sokoni kubeba mikungu ya ndizi na gunia za viazi, kuna muda inakuwa daladala maana huwezi kurudi peke yako tegeta wakati kuna raia wanatia huruma kituo cha daladala na wanakuchangia mafuta, kuna muda zinakuwa gari za mizigo hasa wachaga wanabebea mpaka cement na kuna muda linakuwa bus la kuendea Mkoani, maana huwezi kumwambia Kyaruzi, Muganyizi, Rwehumbiza, Mutayoba na Rweyemamu kwamba gari yake haina chaji ya kumfikisha Bukoba wakati anataka akauzie sura kwa wakina Koku kuwa amejipata.
Ndio maana wengi tunakimbilia gari za kazi mfano Rav 4, hizi gari laini laini zitateseka sana.