Ya nini Kununua Range Rover Moja wakati kwa Bei iyo iyo unapata Xiaomi SkyNomad Nne!

Inaweza kuwa wanaepuka gharama, hawakai nazo muda mrefu kama mradi ni wa muda mfupi unanunua gari ya kutumia muda mfupi tu
Muda mfupi ni miezi/miaka mingapi?

CCECC wamepewa ujenzi wa SGR Lot 6 (Tabora-Kigoma),muda wa ujenzi ni miaka mitano nako wameingiza Hillux kama walivyofanya Lot 5 ambako wanaenda mwaka wa sita sasa na hillux.

BTW:Labda wanaangalia yatakayouzika kirahisi mradi ukikamilika au suala LA uimara.
 
Hiyo RR unatumia KM 120,000, unawauzia wamatumbi second hand $ 50,000. Gari bado inatumika na kwa ubora mzuri. Huyo mchina akifika KM 60,000 unapima skrepa. Hiyo betri na mota ya kufika hapo mchina hana 😊

Mchina anakuuzia kitu kwa ubora kulingana na bei, ukitumie ukanunue kingine.
 
Kwa nini wachina wanaokuja kwenye miradi mikubwa bongo huwa hawaji na hizi gari kutoka kwao.

Mitambo yote (bulldozers,excavators, tankers,trucks etc) ni brands zao ila misele ni Toyota hillux.

Nenda yard yeyote ya mradi wa mchina, utakutana na skrepa za hatari. Greda zilikuja mpya, miaka miwili zipo juu ya mawe. Mchina akimaliza mradi huwa ananunua mashine ya kusaga vyuma ili apunguze skrepa/takataka za mamitambo yake, anapiga mnada mamitambo chakavu ndio anasepa. Anakata chuma chakavu ndio anafunga yard.
Anakuja na kila kitu kipya, lakini akija kumaliza mradi anaacha skrepa, watu wa vyuma chakavu wananunua anasepa zake.
 
Nazani taste yake watanganyika hawaku pendezwa nazo maana show room Yao ipo barabara ya Nyerere zime doda tu.
Kama wana yard hapo watakua wanauza tu ni ngumu kujua hawauzi ni gari nzuri mimi mwenyewe navizia moja ya kampuni hapa wakikubali nilipie itakuja home...
Wachina wana gari nzuri sana kwa bei zake sio mbaya mfano huyu mdudu hapa anatembea mno.
 
Nazani taste yake watanganyika hawaku pendezwa nazo maana show room Yao ipo barabara ya Nyerere zime doda tu.
Wabongo hawa hawa wanaonunua Nissan Juke na Harrier tako la nyani ndio unasema hawakuwa na taste na Haval?

Sema kingine ukweli unaujua.
 
duh
ukimuweka dereva wa daladala aendeshe hio anajikojolea maana hajui abonyeze wapi, na gia hazioni
Mara anasikia welcome please enter your password , atawehuka

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
RR ni RR tu, ile ndinga ni konyo, niliwahi sukuma siku 1, aloooh.
Hatarii sanaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…