Yaandaliwe Mapokezi makubwa kwa Rais Samia tokea Marekani

Yaandaliwe Mapokezi makubwa kwa Rais Samia tokea Marekani

Wengine hata kusoma bado kuchanganya madawa
Ndio nasema basi shida ipo kwa kuwa si Mara ya kwanza kuwa na makosa ya aina hiyo. Ni mara nyingi inatokea, ni ngumu sana kukuta hotuba haina makosa ya hivyo.
Kama shida ni msomaji basi tatizo ni kubwa sana, mm hofu yangu ni hao anaokua anawahutubia wanamuonaje? Bahati mbaya sana ukikosea huwa huambiwi umekosea, utapigiwa makofi. Huu ndio utamaduni wetu
 
Kuna mwingine naye aliwahi kusemekana anaandikiwa sahihi. Ila akija kwenye hotuba anajifanya hasomi. Hapo sasa.

Tatizo kubwa ni namna wanavyochujwa hatimaye kutokea kuwa kinara. Kumbuka uelewa na hata ufahamu wa mambo si kigezo.
 
Haipo siri kuwa safari ya mama Samia Marekani imekuwa ya mafanikio makubwa.

Hakuna shaka kuwa mazungumzo ya ana kwa ana (one to one) ya awaye yote (mwenye nia njema) na mama Samia huwa ni ya mafanikio makubwa.

View attachment 2189466

Kwa hakika mama Samia si wale wengine. Huyu ni msikivu na mwenye mawazo huru (open minded). Mungu atupe nini?

Bila shaka kutokea sasa tutegemee misimamo mipya kuhusiana:

1. Katiba mpya.
2. Haki zetu zikiwamo za mikutano ya kisiasa.
3. Vita vya Ukraine na Urusi.
4. Nyimbo mpya kutoka kwa chawa wale wale.

Safari yenye fursa ya kulileta taifa pamoja, kwa hakika ni bora kuliko zozote zile.

Mungu ibariki Tanzania
Kwakweli naunga mkono.
 
Yaani hapo maza anaongea na camala jicho kwa jicho,magu asingeweza,ndiyo maana alikua hatoki..nikikumbuka kule Uganda waandishi wanamuuliza swali,ye anaandika kwanza,Hadi musevenk akawa anaokoa jahazi,pale tulipigwa
Hii mijitu ya Afrika ninayoona kuongea na mzungu ni Bora kuliko kuongea na mwafrika mweenzake sijui itaacha lini fikra za kitumwa
 
Hii mijitu ya Afrika ninayoona kuongea na mzungu ni Bora kuliko kuongea na mwafrika mweenzake sijui itaacha lini fikra za kitumwa

Kinachokufanya uwe na chuki ya kibaguzi baina ya watu ni ugonjwa unaotibika. Wahi hospitali wala hujarogwa mkuu.
 
Nasikia Makamu wa Rais wa Marekani alijua kwamba mwaka 2015/2020 nchi haikuwa na Rais, ilimchukua mama Samia saa nzima kumuelezea hali ilivyokuwa, hakuamini, ikabidi amuonyeshe picha na video.

Yeye alikuwa anajua JPM ni Waziri wa ujenzi,
😄
 
Kinachokufanya uwe na chuki ya kibaguzi baina ya watu ni ugonjwa unaotibika. Wahi hospitali wala hujarogwa mkuu.
Kati ya mtu anayeona mzungu ni sawa na mwafrika na yule anayeona mzungu ni Bora kuliko mwafrika yupi ana chuki ya kibaguzi
 
Suala si misaada mkuu. Kubadilishana mawazo na kuiona dunia kwa mapana zaidi ndiyo ubinadamu huo.
Kama ishu ni kubadilishana mawazo kwanini yeye kila mara anaenda nje kuliko wa nje kuja huku bongo
 
Kati ya mtu anayeona mzungu ni sawa na mwafrika na yule anayeona mzungu ni Bora kuliko mwafrika yupi ana chuki ya kibaguzi

Si options hizo tu zilizopo lakini.

Vipi umemwangazia anayezingatia kukutana na mzungu, mwafrika, mwarabu, mchina nk kama ni kukutana na binadamu tu?

Hukuwahi kusikia wengine wakiamini binadamu wote ni sawa?
 
Kama ishu ni kubadilishana mawazo kwanini yeye kila mara anaenda nje kuliko wa nje kuja huku bongo

Kupanga si ni kuchagua mkuu?

Kumbuka kuna mambo sisi tunayataka jana mfano demokrasia. Akiupata muarobaini wake leo kutokea kokote kwa mashauriano, si bora kuliko kusubiria kesho?

Si walisema wapambanaji, aliyeko juu mpandie huko huko?
 
Kuna mwingine naye aliwahi kusemekana anaandikiwa sahihi. Ila akija kwenye hotuba anajifanya hasomi. Hapo sasa.

Tatizo kubwa ni namna wanavyochujwa hatimaye kutokea kuwa kinara. Kumbuka uelewa na hata ufahamu wa mambo si kigezo.
Ni kweli.
Ila pia kuandikiwa na kusoma au kukariri sio shida Kama utavyosema ni sahihi.
 
Suala si misaada mkuu. Kubadilishana mawazo na kuiona dunia kwa mapana zaidi ndiyo ubinadamu huo.
Mkuu kwenye ulimwengu wa kibepari neno ubinadamu halina uhalisia. Ubinadamu utakuwepo endapo utanufaika
Ili utoboe kwenye ulimwengu wa kibepari basi weka kando kitu kinaitwa ubinadamu. Ni ukweli huu
Kuua, kupora, kudhulumu ndio nguzo pekee kwenye ulimwengu wa kibepari.
 
Si kila siku na kwa kila kitu mkuu.

Kumbuka tuliambiwa chanjo ni upigaji sijui kama inafahamika hadi leo tumepigwa ngapi.

Waliyaona haya waswahili. Asili ya usemi huu:

"Mchagua nazi hupata koroma."
 
Back
Top Bottom