Maneno yangu sio ya unabii wala mitume ni mawazo binafsi na muelekeo wa kesi tokea huko ulipotokea ,tusidanganyane kuna mawakili mimi huwaita mawakala.
Kesi ya Lisu ni nzito tena nzito sana kuliko mnavyofikiria ,maneno aliyoyatamka Lisu ambazo video zake zimeanza kuondolewa youtube ,ni ushahidi tosha kuwa kazi ipo,tuseme Tundu aliteleza na alipoteleza alikuwa kwenye mtelezo.
Ameongea maneno mazito ya kusisimua na kufikirisha sana na kujiuliza .Je ataweza au wataweza ? Kukinukisha kufanya uasi dhidi ya Serikali. sio kesi rahisi haswa Serikali ikiamka mapemba kabla uasi huo hauja shika kasi na kuichafua nchi.
Sasa hawa mawakala wanaozuka kila shehemu hata kutoka nchi za nje ,hapa napo pana neno ! Ni wazi walikuwa wameshajiandaa ikiwa A tufanye B nayo ndio haya tunayoyaona toka hawa tulionao ambao walikuwa wamejificha sas tunaona. Jambo la mwanzo kufeli ni kufeli kwa viongozi wa dini ambao ndio wamwanzo kuvaa shanga na kulicheza twimbili la Tundu makanisani na kwenye mitandao, sasa hivi wote wamezima.
Ushauri ni kukaa na Serikali mkazungumza nayo (Viongozi waChadema mjipange na muende Ikulu) na kusio kushindana na Kesi inayomkabili Lisu na kujifanya hamjui uhatari wake na zaidi pale mnaowatuma au kujituma kutoa amri ...Serikali imuachie Tundu mara moja.... hilo ni tamko baya sana na ndio linalompoza mwenzenu ,upande wangu kila anaetamka hivyo ndie adui nambari one wa Lisu.
Kwanza kesi za namna hii zinakula tarehe na mwisho wake ni gerezani badala ya kitanzi umevuka kitanzi unaswekwa Jela ,tuseme hakuna ushadi lakini matamko yanamtia mtu gerezani.
Tumieni hekima na busara kumuokoa mwenzenu/mwenzetu WaTanzania tunajuana ,achaneni na wachochezi waliopo nje au ndani wanaojaza mawakala kwa madai ya kumtetea kwa kutumia mahesabu ya probability .