Yajue haya majani ni dawa ya vidonda vya tumbo

Yajue haya majani ni dawa ya vidonda vya tumbo

Mint ni kama kiungo kwenye mboga
Hiyo inaitwa Mint leaves,unaweka kidogo kwenye maji Yake uvuguvugu au moto kiasi,unakunywa kama chai.
Screenshot_20220222-050307.jpg
 
Thread ina miaka mitatu lakini hakuna mrejesho sijui waliokunywa wametokomea wapi!
Kama umepona basi Mungu ni mwema.
Mi nilianzia mwanzo kusoma mbona wapo walipsema wamepona!
Halafu hizi thread zipo 2 zinafanana!

Ila mi nitaleta mrejesho
 
Habarini za jioni ya pasaka ndugu wana jamvi.

Si mwandishi sana humu jamvini japo ni msomaji wa muda kidogo. Leo nimependa ku share jambo lilionipa msaada baada ya kuona watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na shida ya vidonda vya tumbo.

Binafsi niliumwa na vidonda vya tumbo kwa miaka mitatu Lakini nilielekezwa na jamaa niliyekutana naye. NILIEKEZWA BURE NAMI NATOA UFAHAMU HUO BURE.

Tafuta majani flani ntaatach hapa ya aina mbili nayo ambayo utayachuma na kuyatwanga yakiwa mabichi na kisha kuandaa maji ya uvuguvugu na kisha kuyachanganya na hiyo rojo na kisha chuja. Kikombe kimoja cha robo lita kwa siku 3. Nawe utapona kama nilivyopona.

Nina mwaka wa 4 sasa toka nipone. So nina hakika na nisemalo. Majina ya hayo majani siyajui kwa majina yake ila picha zake ndio hizo hapo.

Wataalamu wa classification wanaweza saidia kutupa majina ya hayo majani .

Enjoy the remedy.

View attachment 1077606
Mashona nguo au Nyakifwega
 
Back
Top Bottom