Smartkahn
JF-Expert Member
- Jun 22, 2020
- 594
- 1,061
Nimeiona leo hii thread, nimeipitia nimeona wengi mmechanganya hii mimea, napengine mmeharibu dose na kukosa suluhu ya maradhi yenu.Habarini za jioni ya pasaka ndugu wana jamvi.
Si mwandishi sana humu jamvini japo ni msomaji wa muda kidogo. Leo nimependa ku share jambo lilionipa msaada baada ya kuona watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na shida ya vidonda vya tumbo....
Mimea alioiweka mleta maada ni mimea pori (wild plants), huwa inajiotea tu yenyewe hata kama karibu na makazi ya watu.
Mfano picha ya mmea namba mbili ule mmea ni unaota porini lakini wengi wenu mmeufananisha na maua yanayopandwa majumbani ingawa iko katika familia moja lakini imetofautiana katika species level(spishi tofauti). Hii ya porini ina chemikali yenyenguvu zaidi, hata ukitafuna inakua na harufu pamoja na radha kali iliyochangamka mithili ya peppermint (radha ya pipi kifua zile arafu kuwe na pilipili kwambaali)
Sasa tuone mimea halisi aliyokua ameilenga mleta mada.
Picha ya kwanza na ya pili: Huu unaitwa Blackjack, kitaalamu unaitwa; Bidens pilosa. Kwetu tunaita mavanivani.
Picha ya tatu, nne na ya tano: Huu unaitwa Fever tea, kitaalamu unaitwa Lippia alba/ Lippia javanica. Kwetu tunaita kilienyi.
Hayo majina ya kitaalamu, botanical or scientific names yanatambulika duniani kote(officially).
Kwahiyo mliochangaya mimea (dose) na hamkupona mnaweza kuanza tena kwa usahihi.
Na hizi hapa chini ndio uhalisia wa mmea wenyewe(wild oregona)
kwa huku kwetu na ndio aliotumia mleta maada na akapona.