Habarini za jioni ya pasaka ndugu wana jamvi.
Si mwandishi sana humu jamvini japo ni msomaji wa muda kidogo. Leo nimependa ku share jambo lilionipa msaada baada ya kuona watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na shida ya vidonda vya tumbo.
Binafsi niliumwa na vidonda vya tumbo kwa miaka mitatu Lakini nilielekezwa na jamaa niliyekutana naye. NILIEKEZWA BURE NAMI NATOA UFAHAMU HUO BURE.
Tafuta majani flani ntaatach hapa ya aina mbili nayo ambayo utayachuma na kuyatwanga yakiwa mabichi na kisha kuandaa maji ya uvuguvugu na kisha kuyachanganya na hiyo rojo na kisha chuja. Kikombe kimoja cha robo lita kwa siku 3. Nawe utapona kama nilivyopona.
Nina mwaka wa 4 sasa toka nipone. So nina hakika na nisemalo. Majina ya hayo majani siyajui kwa majina yake ila picha zake ndio hizo hapo.
Wataalamu wa classification wanaweza saidia kutupa majina ya hayo majani .
Enjoy the remedy.
View attachment 1077606