Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 26,021
- 79,710
Serikali inakusudia kufanya marekebisho kadhaa katika Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168. Marekebisho yaliyowasilishwa Bungeni kupitia Mswaada
wa Marekebisho ya Sheria ya makosa ya Barabarani ni pamoja na:-
1. Marekebisho katika Kifungu cha 21, kwa kuweka sharti la lazima kwa mtu yeyote anayetaka kuwa dereva wa pikipiki kusomea udereva katika shule ya udereva iliyosajiliwa kama ilivyo kwa madereva wa magari.
2. Marekebisho ya Kifungu cha 36, ambapo inakusudiwa kuwa dereva aliyefungiwa leseni Kenya na Uganda atahesabika kuwa amefungiwa vilevile kuendesha gari Nchini (Tanzania);
3. Marekebisho ya Kifungu cha 50, ambapo inependekezwa kuongezeka kifungu kidogo cha (29) chenye lengo la kufanya kuwa kosa la kwa dereva kuendesha gari huku akiongea na simu.
Kifungu hiki hakihusiani na kuendesha gari huku dereva akiongea na simu kwa kutumia kifaa maalumu cha kuongelea;
4. Utambulisho wa kifungu kipya cha 39D, ambacho kinaleta kufanya kuwa kosa kwa abiria aliyeko katika gari bila ya kufunga mkanda.
Vilevile kifungu hiki kinafanya kuwa kosa kwa mhusika / wahusika kwa kumweka au kumbeba mtoto aliyeko chini ya umri wa miaka mitano katika kiti cha mbele. n.k.