Yajue maeneo ambayo ni marufuku kupiga picha Dar es Salaam

Yajue maeneo ambayo ni marufuku kupiga picha Dar es Salaam

Zile fremu za lugalo mpaka unafika pale agakhan hospital sijui kwanini hawazitoi Kwa usalama. Wa jeshi.
 
  • Thanks
Reactions: ---
HYO tecnolojia iliyoongezeka Je kila mtu ana access nayo?
Hyo picha za kiwanda zinazopigwa Kutokea korea ,
Je kila mkorea raia anaweza kupiga?
Ukweli unabaki pale pale maeneo yaliyokatazwa kupiga picha ,nchi yeyote Duniani yapo,hata nchi zilizoendelea na zinazotengeneza hizo tecnolojia baadhi ya maeneo hurusiwi kabisa kupiga picha wala kuendesha ki drone.
Kama unajua ni kupunguza usumbufu na sii sababu zaidi ya usumbufu,basi ufahamu ndo ulipokwamia hapo sio kosa.
Taja eneo restricted uletewe picha zake
 
Mlimani City Mall walikuwa wanakataza hasa kwa nje parking area hawataki upige picha jengo, n.k.
 
Jengo la AU pale Adis Ababa wachina walijenga na wakaweka vifaa vya kusikiza.
China waliingia mkataba na UK kuwauzia bus za mwendokasi Waingereza walivyogundua kuwa yale magari yanapeleka taarifa China wasitisha hiyo Tender wameenda kuchukua bus Holland..
 
  • Thanks
Reactions: ---
Taja eneo restricted uletewe picha zake
Sasa picha utakazo leta utakuwa umepiga ww raia?
Picha OFFICIAL hutoa wao.!
Nenda kapige ya simu yako Uletee.
Kapige kwenye maeneo restricted kama yalivyoorodheshwa.
 
Swali langu, mfano hayo majengo ya wizara au vital installations nimepiga picha, naweza nikachukuliwa hatua zipi za kisheria ikiwa umesema hakuna sheria ya Ujumla? Kwa sababu sio sehemu zote ulizozitaja zina maandishi au alama ya kuzuia mtu kupiga picha Bujibuji Simba Nyamaume
 
Huu nao ni upuuzi tu.Wananchi wanaogopa hata kushika bendera ya nchi yao?Sasa wajivunie nini?Au wajivunie nembo mpya za utekaji,utesaji,ufirauni na uuaji?
Unapita sehemu kuna nembo ya usipige picha hapa harafu mbele unamkuta Bujibuji Simba nyanaume na Madmax wanakagua wapiga picha ili wawakamate huwa najiuliza je ni vyakula vimetudumaza uwezo wa kufikiri au nini na sipati majibu..
 
Sasa picha utakazo leta utakuwa umepiga ww raia?
Picha OFFICIAL hutoa wao.!
Nenda kapige ya simu yako Uletee.
Kapige kwenye maeneo restricted kama yalivyoorodheshwa.
Picha kupigwa sio lazima simu mazee mbona hauelewi Dunia imeendelea kiongozi..
 
Asante kwa kututahadharisha! Hata hivyo Dunia imeendelea! Teknolijia iko mbali. MO29 walizima internet lakini kila kilichofanyika dunia nzima ilijua.
Sasa hivi hata kwa Google map unaona location vizuri.
 
Sasa lugalo pale palivyojaa maframe picha si zinapigwa tu sahvi Isanga family RRONDO

Ova
Hizo ni sheria za mwaka 60s. Sasa kama nataka picha ya eneo lolote si natumia Google Earth? Huwezi kuzuia watu kupiga picha zama hizi za smart devices. Unaweza kunionq napita tu nimevaa sun goggles kumbe nachukua video kiulaini. We are still stuck in the 60s!
 
Hizo ni sheria za mwaka 60s. Sasa kama nataka picha ya eneo lolote si natumia Google Earth? Huwezi kuzuia watu kupiga picha zama hizi za smart devices. Unaweza kunionq napita tu nimevaa sun goggles kumbe nachukua video kiulaini. We are still stuck in the 60s!
Watawala wetu wana akili mgando
 
Sijawahi elewa umuhimu wa haya makatazo.

Mtu anakataza usipige picha kwenye Panton, kwa lengo la kuficha nini?

Hadi mwendo kasi nazo ziliwekewa hii sheria (sijui kama hadi saizi bado inaendelea)

Mgambo wa Jiji alimfuma jamaa akiwa anapiga picha kwenye kituo cha mwendokasi eti akawa anataka kumnyang'anya simu kisa kupiga picha.

Jamaa akamwambia kama haya mabasi na vituo vyake havipaswi kupigwa picha sasa mbona mimi huwa nayaona mtandaoni tena hadi na video zake?

So ni either nifute picha na kila mtu aendelee na michongo yake ila sio uchukue simu yangu kwasababu ya picha.

Ikabidi jamaa afute picha.
 
Kumbe?🤔 Ni kuwa makini maana hawa wauaji kuua ni kitu kidogo, ni fedheha kuuawa kwa ajili ya kupiga picha tu
 
Kabla sijaenda naomba kwanza nisahihishe jambo moja muhimu: si sahihi kusema kwamba kila eneo hapa chini lina sheria ya jumla inayosema “hairuhusiwi kupiga picha.” Baadhi ni maeneo nyeti ambayo hupaswi kupiga picha bila ruhusa, na baadhi yana restrictions maalumu, hasa maeneo ya kijeshi na sehemu za usalama za viwanja vya ndege. Serikali ya Marekani pia inaonya kwamba maeneo ambayo upigaji picha umepigwa marufuku Tanzania si mara zote yana alama.


Kwa Dar es Salaam, orodha ya maeneo 20 ya kuwa mwangalifu ni:


  1. Ikulu / State House, Dar es Salaam — epuka kupiga picha za jengo na mifumo ya ulinzi bila ruhusa.
  2. Kambi na vituo vya JWTZ — upigaji picha wa vituo vya ulinzi unaweza kuzuiwa kisheria.
  3. Makao au vituo vya polisi — hasa kupiga picha za ndani, askari, magari au shughuli za kiusalama.
  4. Julius Nyerere International Airport (JNIA) — hasa maeneo ya security-restricted, runway na miundombinu ya uwanja.
  5. Bandari ya Dar es Salaam — maeneo ya operation/security ya bandari. Hata Feri ya Magogoni kwenda Kivukoni huruhusiwi kabisa kupiga picha, wale askari migambo wakiotea lazima wakusumbue sana.
  6. Magereza ya Dar es Salaam — hasa ndani, mageti na miundombinu ya ulinzi.
  7. Majengo ya Wizara na Serikali — hasa maeneo yenye ulinzi au miundombinu nyeti.
  8. Mahakama na maeneo yenye shughuli za kiusalama — omba ruhusa kabla ya kupiga picha za ndani au za kiusalama.
  9. Ubalozi wa nchi za kigeni — epuka kupiga picha za mageti, walinzi na security installations.
  10. Makazi rasmi ya viongozi wakuu wa Serikali — usilenge nyumba/makazi au ulinzi bila ruhusa.
  11. Vituo vya mawasiliano ya kijeshi/usalama — antena, minara na miundombinu yake.
  12. Miundombinu ya kijeshi kwenye maeneo ya jiji — hata kama iko karibu na barabara ya umma.
  13. Vituo vya kudhibiti ndege/air-traffic facilities — hasa maeneo yasiyoruhusiwa kwa umma.
  14. Runway na maeneo ya aircraft operations JNIA — usipige picha ukiwa kwenye restricted area bila ruhusa.
  15. Vituo vya nishati vya kimkakati — kama vituo muhimu vya umeme na miundombinu inayolindwa.
  16. Miundombinu muhimu ya bandari — cranes, control/security facilities na maeneo yaliyowekewa restriction.
  17. Vituo vya mafuta vya kimkakati — hasa maeneo ya kuhifadhi mafuta yenye ulinzi.
  18. Madaraja au miundombinu ambayo imewekewa restriction ya usalama — usidhani kwamba kwa kuwa uko barabarani basi kila picha inaruhusiwa; watu wamewahi kuzuiliwa kwa kupiga picha za madaraja na maeneo ya viwanda.
  19. Maeneo ya viwanda yenye miundombinu nyeti — hasa kama kuna walinzi au alama za kutoruhusu upigaji picha.
  20. Maeneo yoyote yenye alama “NO PHOTOGRAPHY / PHOTOGRAPHY PROHIBITED” — hili ndilo rahisi zaidi: usiipuuze alama hiyo, hata kama eneo linaonekana kuwa la kawaida.

⚠️ Jambo muhimu kuhusu simu​


Kuwa unapiga picha kwa simu badala ya kamera kubwa hakumaanishi moja kwa moja kwamba inaruhusiwa. Sheria/kanuni zinaweza kulenga kitendo cha kuchukua picha yenyewe. Kwa mfano, kanuni za maeneo ya ulinzi zinaweza kumpa mamlaka anayehusika kuzuia kuchukua, kutengeneza au hata kumiliki picha/sketch/plan ya defence establishment.


🚁 Na kama ni drone?​


Hapo masharti ni makali zaidi. TCAA inasema drone zinahitaji approval/permit, na maeneo yaliyotajwa kama restricted/prohibited ni pamoja na military installations, State House, prisons, airports/airfields, government facilities na crowded public areas bila ruhusa maalumu.


Kwa hiyo, ukiwa Dar es Salaam na unaona eneo la kijeshi, polisi, Ikulu, uwanja wa ndege, gereza, bandari au miundombinu nyeti, kanuni salama ni: usilenge eneo hilo kwa kamera mpaka upate ruhusa.
Usije ukapiga picha ukipanda Feryy kigamboni,walitaka kunitoa roho.
 
Jamaa walinkazia ,wakanioandisha Kule juu kwenye pantoni na nilikuwa Niko vyombo ,walikomaa niliwapa 20k ndo wakaniachia.
 
Sasa hivi technology imeongezeka hayo matangazo ni ya karne ya 18 huko sio sasa hivi wazungu wanaweza kukuonyesha picha ya kiwanda chako wakiwa South Korea..
Meli yetu ya Mv Bukoba ilipoleta tatizo na kuua watu wengi wataalamu walikuja na sababu ilijaza watu wengi ikapinduka Mabeberu wakaja na picha za satellite wakionesha ilipoanzia tatizo mpaka kwenda kugonga mwamba mimi hayo matangazo najua yapo kupunguza usumbufu ila sio ikitakiwa picha mtu atashindwa kuipata sio kweli..
Yaah sasa hivi sisi tupo bado 90s huko wenzetu wako mbali
 
Inashangaza kwa kweli!mwaka jana nilikuwa kwenye msiba wa kanali mstaafu wa jeshi,basi wakaja kikosi cha JWTZ kwa ajili ya kupiga mizinga.kabla hawajaaza wakatoa taarifa kuwa mtu yeyote asirekodi yale matukio wala kupiga picha na kama kuna ambae amerekodi au kupiga picha afute haraka!sasa mi nikasema ina maana gani?nilipokaa nikazoom nikarekodi yote mpaka mwisho na mpaka leo yapo kwenye simu sijaona lolote
 
Back
Top Bottom