Yajue maeneo ambayo ni marufuku kupiga picha Dar es Salaam

Zile fremu za lugalo mpaka unafika pale agakhan hospital sijui kwanini hawazitoi Kwa usalama. Wa jeshi.
 
Reactions: ---
Taja eneo restricted uletewe picha zake
 
Mlimani City Mall walikuwa wanakataza hasa kwa nje parking area hawataki upige picha jengo, n.k.
 
Jengo la AU pale Adis Ababa wachina walijenga na wakaweka vifaa vya kusikiza.
China waliingia mkataba na UK kuwauzia bus za mwendokasi Waingereza walivyogundua kuwa yale magari yanapeleka taarifa China wasitisha hiyo Tender wameenda kuchukua bus Holland..
 
Reactions: ---
Taja eneo restricted uletewe picha zake
Sasa picha utakazo leta utakuwa umepiga ww raia?
Picha OFFICIAL hutoa wao.!
Nenda kapige ya simu yako Uletee.
Kapige kwenye maeneo restricted kama yalivyoorodheshwa.
 
Swali langu, mfano hayo majengo ya wizara au vital installations nimepiga picha, naweza nikachukuliwa hatua zipi za kisheria ikiwa umesema hakuna sheria ya Ujumla? Kwa sababu sio sehemu zote ulizozitaja zina maandishi au alama ya kuzuia mtu kupiga picha Bujibuji Simba Nyamaume
 
Huu nao ni upuuzi tu.Wananchi wanaogopa hata kushika bendera ya nchi yao?Sasa wajivunie nini?Au wajivunie nembo mpya za utekaji,utesaji,ufirauni na uuaji?
Unapita sehemu kuna nembo ya usipige picha hapa harafu mbele unamkuta Bujibuji Simba nyanaume na Madmax wanakagua wapiga picha ili wawakamate huwa najiuliza je ni vyakula vimetudumaza uwezo wa kufikiri au nini na sipati majibu..
 
Sasa picha utakazo leta utakuwa umepiga ww raia?
Picha OFFICIAL hutoa wao.!
Nenda kapige ya simu yako Uletee.
Kapige kwenye maeneo restricted kama yalivyoorodheshwa.
Picha kupigwa sio lazima simu mazee mbona hauelewi Dunia imeendelea kiongozi..
 
Asante kwa kututahadharisha! Hata hivyo Dunia imeendelea! Teknolijia iko mbali. MO29 walizima internet lakini kila kilichofanyika dunia nzima ilijua.
Sasa hivi hata kwa Google map unaona location vizuri.
 
Sasa lugalo pale palivyojaa maframe picha si zinapigwa tu sahvi Isanga family RRONDO

Ova
Hizo ni sheria za mwaka 60s. Sasa kama nataka picha ya eneo lolote si natumia Google Earth? Huwezi kuzuia watu kupiga picha zama hizi za smart devices. Unaweza kunionq napita tu nimevaa sun goggles kumbe nachukua video kiulaini. We are still stuck in the 60s!
 
Watawala wetu wana akili mgando
 
Sijawahi elewa umuhimu wa haya makatazo.

Mtu anakataza usipige picha kwenye Panton, kwa lengo la kuficha nini?

Hadi mwendo kasi nazo ziliwekewa hii sheria (sijui kama hadi saizi bado inaendelea)

Mgambo wa Jiji alimfuma jamaa akiwa anapiga picha kwenye kituo cha mwendokasi eti akawa anataka kumnyang'anya simu kisa kupiga picha.

Jamaa akamwambia kama haya mabasi na vituo vyake havipaswi kupigwa picha sasa mbona mimi huwa nayaona mtandaoni tena hadi na video zake?

So ni either nifute picha na kila mtu aendelee na michongo yake ila sio uchukue simu yangu kwasababu ya picha.

Ikabidi jamaa afute picha.
 
Kumbe?🤔 Ni kuwa makini maana hawa wauaji kuua ni kitu kidogo, ni fedheha kuuawa kwa ajili ya kupiga picha tu
 
Usije ukapiga picha ukipanda Feryy kigamboni,walitaka kunitoa roho.
 
Jamaa walinkazia ,wakanioandisha Kule juu kwenye pantoni na nilikuwa Niko vyombo ,walikomaa niliwapa 20k ndo wakaniachia.
 
Yaah sasa hivi sisi tupo bado 90s huko wenzetu wako mbali
 
Inashangaza kwa kweli!mwaka jana nilikuwa kwenye msiba wa kanali mstaafu wa jeshi,basi wakaja kikosi cha JWTZ kwa ajili ya kupiga mizinga.kabla hawajaaza wakatoa taarifa kuwa mtu yeyote asirekodi yale matukio wala kupiga picha na kama kuna ambae amerekodi au kupiga picha afute haraka!sasa mi nikasema ina maana gani?nilipokaa nikazoom nikarekodi yote mpaka mwisho na mpaka leo yapo kwenye simu sijaona lolote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…