Yajue maisha ya Mbinguni, yana raha isiyo na kifani

wataofufuliwa siku ya mwisho, sindio wataamka na miili yao ??
Hapana.
Soma: Wafilipi 3:20-21
Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.

Soma pia: 1 Kor 15:51-54
Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu[mwili] uharibikao uvae kutoharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutoharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa katika ushindi.
 
Punguza bangi hakuna kitu kama hicho.
 
Punguza bangi hakuna kitu kama hicho.
Sijazungumzia kitu. Nimezungumzia mambo mazuri yaliyopo mbinguni.

Halafu ukipinga jambo pinga kwa hoja uonyeshe kweli wewe ni great thinker.
 
Sijazungumzia kitu. Nimezungumzia mambo mazuri yaliyopo mbinguni.

Halafu ukipinga jambo pinga kwa hoja uonyeshe kweli wewe ni great thinker.
Sihitaji kutoa ushahidi kwa vile hicho kitabu unachorejea ni hadithi za kawaida zilizotungwa na wakoloni na zikatupumbaza kiasi cha kugeuka mazezeta na mazwazwa. Wangapi waliwahi kufufuliwa, kwenda kule na kurudi na mbona haya yote yanaingia akilini kwa njia ya imani na si kuelewa?
 
Soma uzi wangu huu:
Hapo nimezungumzia habari za C.S. Lewis. Alikuwa mpinzani wa Biblia kuliko wewe, lakini akageuka, akaamini uwepo wa Mungu na habari za mbinguni. C.S. Lewis can be professionally referred to as:
  • Professor C.S. Lewis – He was a professor of Medieval and Renaissance Literature at the University of Cambridge.
  • Scholar C.S. Lewis – He was a distinguished academic in literature and theology.
  • Author C.S. Lewis – He wrote numerous influential books, including Mere Christianity and The Chronicles of Narnia.
  • Literary Critic C.S. Lewis – He analyzed and wrote about literary works extensively.
  • Christian Apologist C.S. Lewis – He defended and explained Christianity through logical arguments.
  • Philosopher C.S. Lewis – He explored deep philosophical and theological questions in his works.
  • Theologian C.S. Lewis – His writings deeply influenced Christian thought.
 
Nasikia kutakuwa na mito ya pombe tamu l/adhatil kwa mujibu wa sheikh
Biblia inasema walevi hawataingia mbinguni.
1 Kor 6:9-10
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."


Mstari huo unaonyesha wazi hakuna pombe mbinguni. Kwanza pombe haina raha yoyote. Kitu kinaathiri utendaji kazi wa ubongo ndio raha gani hiyo.

Mbinguni tutakunywa vitu vitamu kuliko hivi vya duniani
 
Hivi ulikutana na magaidi waliojiua na kuahidiwa mabikra 72 huko, vipi mke wa shetani FaizaFoxy ulikutana naye?
 
Umenukuu maandiko vizuri!
Unasimlia kama umeshawahi kufika huko na kurudi duniani kumbe bado.
 
Kuwa professor siyo kuwa genius. Lewis aliishia kwenye Ukristo kwa sababu ulimshawishi au alikuwa anatafuta kitu kama Paulo wa kwenye biblia aliyeanzisha injili yake ndani ya injili ya Yesu na akawa na influence kuliko hata Yesu mwenyewe. Mie nitakacho ni rahisi. Ukiwaangalia hao waliotuletea hizi ngano sasa. hawazifuati wala kuzimani baada ya kuzitumia kututawala kwa ajili ya kutunyonya milele. Mbinguni eti miili mipya. Kama ni hivyo, iweje mtu akizikwa mnamwambia ni makazi yake ya milele? Kwani, milele ina mwisho?
 
Hapa duniani mi nasikia raha ninapo lala usingizi tu.
Nikiamka mawazo ni mengi kuhusu mchakato wa maisha.
Nadhai kifo kina raha zaidi kwani usingizi wake ni mwingi zaidi.
 
Mimi huwa nina Maswali yangu huwa natatafuta mtu wa kunisaidia sijui kama wewe Setfree, unaweza nisaidia.

Naomba nitoe maelezo kisha swali.
Biblia inasema Shetani alikuwa Malaika wa Mungu mtiifu amabye baadaye ali hasi sijui hili ni kweli au la, lakini baada ya ku kukataa kupokea amri kutoka kwa Mungu, Mungu alimfukuza na akamtupa Duniani.

Adam na Hawa baada ya kuwa wamemkosea Mungu kule Bustanini Eden, nao aliwafukuza, nao wakaletwa au wako Duniani.

Sasa Swali langu, Eden ni Mbinguni au ni Hapa hapa duniani?

Na kama ni hapa hapa duniani iko nchi gani kwa ufahamu wako?

Na kama ni Mbinguni kwanini Shetani alitupwa Duniani na Adam na Hawa nao wakatupwa Duniani. Je Duniani ndio mahala pa Mungu kutupa asivyo-vithamini(Taka).

Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake, Je Shetani anaumbo gani?

Nakumbuka kwamba Shetani alimrubuni Hawa, na Hawa akamshawishi Adam. swali langu hapa ni Je, kati ya Shetani, Adama na Hawa nani alitangulia kufika Dunia hii au ani alifukuzwa kabla ya wenzake?

Mungu kauumba ulimwengu kwa uelewa wako kwanini hakumtupa Shetani sayari nyingine yoyote badala yake akamtupa hapa Duniani, ambaka Sisi wapendwa wake tunaishi? au nini lilikuwa lengo la Mungu kutuweka pamoja na shetani aliyemshindwa yeye?

Ni hayo tu kwasasa?
 
Unaweza kuta yeye ndiye yule mchungaji Zumaridi anayeishi Mwanza.

Anasema yeye Mbinguni huwa anakwenda na kurudi, anaongea na Mungu kwa kiswahili na Kisukuma.
 
Hivi kweli mbakaji Muddy yupo mbinguni kweli firahuni yule?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…