Yajue Maisha yalivyo jela

Yajue Maisha yalivyo jela

Utaratibu wa kutembelea upoje? Maana kuna watu wanapaogopa unaweza ukaenda mule usirudi uraiani ukabakia humo humo kwa hio toa maelezo kila siku unaruhusiwa kwenda kutembelea na kuwaona wafungwa na unapitia taratibu zipi ili mtu aelewe maana panatisha pale Mimi nikipishana na wafungwa wananiangalia kwa huruma sana kuna kitu wanatamani kuniambia ila sijui wanataka kusema nini kwa hio wanapokodoa macho naogopa hata kuwasogelea na pia ungeongeza sio jela zote wanaishi maisha magumu hivyo kuna jela zingine treatment ni nzuri zaidi km upo uraiani tu
Una fika unataja majina yako matatu na kazi yako Kisha una waambia nimekuja kuwa tembelea wafungwa na mahabusu Kama sehemu ya ibaada katika Imani yangu watakuelewa mkuu

Kumbuka huwezi kuingia jera bila fairi la mahakama kwahiyo Hilo halina shida mkuu
 
Samahani,katika kitu kinachopigwa sana vita huko gerezani hasa Tanzania ni ushoga, ikigundulika utajuta, sifahamu ulikuwa gereza gani ,ila litakuwa mkoani.
Kama una nia ya kujenga, litaje hilo gereza ili hatua stahiki zichukuliwe.

Kuna wafungwa wazoefu humu, tupeni uzoefu wenu kuhusu hali ya ushoga huko magerezani coz inawezekana watu wanaangalia magereza ya Dar es salaam na kuhisi yote ni kama ya mikoan
Hali hii ipo magereza yote japo you will never know Kama haupo tayali kuwa mfungwa au mahabusu kwanza

Vueni hizo suti kimkakati

Kisha ingieni gerezani mkaonje ladha ya maisha harisi huko

labda mtaingiwa na ubinadamu kidogo

Labda mtayaona Maovu mengi yaliyomo
 
Hivi naomba kuuliza kwa ulalaji wa jela ukibanwa na haja uinuke uende chooni unafanyaje maana sakafu yote imejaa watu wamelala chini,unakanyagaje hapo down
Kumbu kumbu zitakubeba mkuu kinyume na hapo una weza kumpa taarifa nyampala japo atakuonyesha kwa kuku achia maumivu kidogo
 
Nikitaka kuwatembelea wafungwa na kuwapelekea Zawadi je sitosumbuliwa na hao viongozi wao? Yaani mtu yoyote anaruhusiwa kutembelea wafungwa? Au kuna masharti.
Mkuu fika jera waambie haja yako Kama unataka kuwa saidia wafungwa sabuni watakuuliza kwanini waambie nisehemu ya sadaka yangu
na niKama ibaada yangu kwa mungu wangu

hakuna baya mkuu

Lakini pia Kama Ni swala la mavazi una weza kuwaambia kwamba Nina nguo nyingi Sasa nimeona kuzitupa kwangu Ni dhambi Kama Kuna watu watazihitaji ninazo naomba niwa saidie watakuelewa pia mkuu

Lakini pia gerezani Kama una ndugu au mtu unaye mfahamu unaenda na unawaambia nimekuja kumwona frani Mimi Ni frani kwake

Na watakapo mwita watamuuliza mhusika Kama anakufahamu

Kiukweli Kuna maswali mengi lakini mtu mkweli na mwema huonekana tu

Kingine labda tunge mpata askali magereza Nina Imani yupo humu atupe mwongozo mkuu

Kwani Mimi Nina uzoefu wa ndani Sana lakini sio nje
 
Nilishatembelea gereza la butimba nikiwa na watu wa tume ya haki za binadamu na utawala bora mida ya asubuhi tukakuta baadhi ya wafungwa wanacheza mpira wa miguu.
Tume ya haki za binadamu ikafanya kikao na uongozi wa gereza wakaomba wasaidiwe tv kwani iliyokuwepo ilikuwa imeharibika.
Ila jela siyo nikifikiria tu ile kukosa uhuru.
Duh Mwenyezi Mungu atuepushe na hicho kikombe nilishatembelea pia gererza la keko kuna brother wangu alikuwa rumande .
Huyu brother wetu hatukumtupa tulikuwa na ratiba ya kumpelekea breakfast,lunch na dinner.
Jamaa alikaa tu rumande baadae kesi yake ikafutwa .
 
Mkuu je kuna matukio yoyote ya kikatili wafungwa hufanyiana?

Na vipi kuhusu nyembe za kunyolea huwa hazitumiki kama silaha?
Matukio ya kikatili yapo kwamfano...

Mfungwa awapo shambani huwa wanalima kwa mstali ulio nyooka

Sasa mfungwa awapo shambani kulima hapaswi kulima kwa speed wala slow

Yani akiwaacha nyuma wenzie tafsiri yake nikwamba ana taka kukimbia hivyo atachezea mijeredi ya nyapala

Na wakimtangulia akabaki nyuma ya wenzie tafsiri yake nikwamba anategea hapo pia atachezea mijeredi

Sasa hebu fkilia unajituma kulima lakini huku nyuma nyapala hachoki kukupiga

Huo si ukatili?

Nyapala huyu atasema chuchu maeni huyu atasema simameni nakila anaye kuja huja na adhabu yake

Na kuhusu nyembe wanao ziuza na kunyoa niwatu special walio chaguliwa na nyapala mkuu

Na sjui huwa Wana zingatia Nini kuwa chagua Ila sjawai shuhudia tukio la kuchinjana na nyembe
 
...Yajue jinsi maisha yalivyo jera no 2

Nilipo fika kwenye ule mlango wa cell Ile na kutazama ndani sikuamini na ilikuwa Kama naota..

Kwanza ni mionekano ya watu waliopo ndani ya gereza ilini shangaza Sana

Vichwa vyao vyote vimenyolewa vipara na langizao nikama wote Wana fanana/wamepauka

Mithili ya mtu anaye shinda kwenye mashine za kusaga akajifuta vumbi ya unga lakini Kuna Ile vumbi kwa mbaali inayo bakia

Baada ya kusogea zaidi pale ndani nikaona vipande vya vimagoro vile vyembamba/ulimi wambwa. vipande vyake Sasa

Vime kusanywa sehemu lundo Kama mchanga ulio mwagwa na na tipa kwenye ukuta wa Ile cell yenyewe

Niliona watu wengi wakiwa Katika mwonekano wa kukata tamaa nyuso zao zime poteza matumaini ya kuishi kabisa

Walionekana wamekata tamaa na Hawa ijui kesho hatima yao hakika jera nikuzimu jera sio duniani jera ni upade wa pili wa dunia

Nikiwa nime zubaa alisogea Yule nyampala aliye nipokea pale nje na kuniambia Sasa nataka niku tambulisheni kwa viongozi wa gereza

Akaanza kutu tambulisha mmoja baada ya mwingine kuanzia kierehere mpaka nyampala mkuu

Baada ya kumaliza kutu tambulisha Yule nyampala msaidizi akatu peleka kwa kiingozi mwingine

Ambaye nikiongozi wa nidhamu hapo cell na jukumu lake nikuku uliza ulikuwa una fanya kazi gani huko mtaani/urain

Kwanini umefika pale gerezani na nimshauri pia anaweza kuku shauri jinsi ya kui epuka kesi yako Kama Ina wezekana

Lakini pia huwa na maswali ya kinafiki kwamfano anaweza kuku uliza pale dilishani Kuna nondo ngapi?

Ukijibu hovyo utachezea baraa Mambo ya jera hayo

Basi baada ya kukutanishwa na viongozi wote wa cell ndio tuka pelekwa kwa nyampala mkuu na huyu ndiye mkuu wa gereza kwa upande wa wa fungwa wote na mahabusu

Wale viongozi pamoja na Yule mkuu wao wakatufundisha Sheria zote za gereza na jinsi ya kuishi gerezani sheria a zenyewe nikama ifwatavyo

1)kiongozi yeyote wa gerezani awe mkubwa au mdogo chochote atakacho kuambia imatakiwa uitikie ndiyo bwana mkubwa

kinyume chake ni makofi 15 mazito ya kiatu Cha tairi ya gali/gurubasi ya mgongoni/mbata wao waita hivyo"

2)ukiwa gerezani iwe chooni unajisaidia au popote pale ukiskia filimbi inatakiwa ulale kifudi fudi zingatia popote pale"

kwamaana hiyo Kama nu chooni hata kimba au mkojo wewe lalia

kinyume na hapo kitakacho kukuta ni shida"

3) ukiingia chooni hauruhusiwi kukojoa umesimama Ina takiwa ukojoe umechuchumaa"

na unapo kojoa hautakiwi mkojo usikike kinyume chake ni tatizo"

4)kuna kuwa na ndoo ya maji na vikombe viwili kimoja Cha kuchotea na kingine ni chakunywea ukichukua kikombe Cha kunywea ukachotea kichapo"

Na ukichukua kikombe Cha kuchotea ukanywea kichapo"

Unacho takiwa kufanya nikuchukua kikombe Cha kuchotea unachota maji.

Baada ya kuchota maji kwenye ndoo unaya miminia kwenye kikombe Cha kunywea.

Baada ya kuya mimina una kiweka kikombe juu ya mfuniko wa ndoo/juu ya ndoo kwa kuki funika/juuchini Kisha unakunywa maji

Shariti lingine usichote maji ambayo huwezi Kuya maliza kuyanywa kinyume chake utaisoma namba

5)UKipiga makofi gerezani tafsiri yake nikwamba una neno/au unataka kuzungumza Jambo

Kwahiyo UKipiga makofi watu wote huacha kuzungumza na kuku tazama wewe wakusikilize una semaje?

Hivyo gerezani kuwa makini wakati wa kuuwa mbu aliye tua kwenye ugoko wako yasije yaka kukuta

6) gerezani kuna ushoga na mashoga wapo lakini nikosa kumwita shoga. shoga"

Atakacho kifanya huyo shoga nikwenda kwa nyampala mkuu nakuku shtaki kumtaka kimapenzi ili na wewe uongezewe siku gerezani ili uje uwe ashoga Kama alivyo yeye

so unakuwa unawajua mashoga Ila una kausha kwani hizo ni mboga za nyapara

7)gerezani hauruhusiwi kupiga story mda wa kulala

8)gerezani ukifika mda wa I abada ni lazima uhudhulie hasa ibada ya kabra ya kulala

Haijarishi ni ibada ya kikristo au kiisramu chamsingi usikilize tu

9)unaopo enda chooni ukii kuta ndara ipo mlangoni na zimeangalia ndani/kuelekea chooni usii ngie Ina maanisha Kuna mtu

Kinyume chake ingia hiyo itakuwa Ina maanisha hakuna mtu

10)jera Kama utakuwa na tatizo au shida yoyote hauruhusiwi kwenda kwa askali magereza moja kwa moja

unacho takiwa kufanya nikwenda kwa Nyampala Kisha Nyampala atampa taarifa nyampala mkuu

Kisha Nyampala mkuu ndiye ata Kaye fikisha taarifa kwa Askari wa gereza kinyume na hapo nitatizo

Na hapo ndipo ushoga unapoanzia kwamba mfungwa

anaingiliwa kimwili na mwanaume mwenzie/nyampala

Na ili mfungwa huyo atoe taarifa kwa askali magereza nilazima apitie kwa Nyapala

na nyampala huyo huyo ndiye anaye mla mfungwa

je tuta zuia ushoga jera kweli?

Ndiyo maana wanasema
Kama jera ni shule mpeleke mwanao sio mwana wa mwenzio

Na yafwatayo nimengine ambayo nikama sheria ndani ya jera....

Itaendelea....
Jitahidi kutendea haki herufi R na L.
 
Inchi zilizo endelea huwezi.kumkamata mtu kabla haujapata ushahidi

Lakini huku kwetu police ana kukamata ndipo anaenda kutafuta ushahidi

Haijarishi ata tafuta ushahidi kwa mda gani

nahata asipo upata hawezi.kukulipa kwa kukupotezea mda

Kwajinsi Hali ilivyo na mazingila ya kisheria yalivyo police anauwezo wa kukutupa ndani bila hatia na aka kuolea mkeo vizuli tu
Inasikitisha sana
 
Kwanini mashirika yanayotoa misaada ya kisheria yasiende kuwasaisldia hao waliosingiziwa? Waliokaa mahabusu miaka mitano anaona Bora ningefanya hayo ninayotuhumiwa niwe hapa kihalali. Kuna mashirika, mpk mawakili wa serikali, na legal aids mbalimbali ikiwemo na ya Mhe Rais hebu wawe wakiwakumbuka na hao kama Kijana aliyeokota risasi
Aisee kweli kabisa hebu jamaa atoe detail zote za huyo kijana aliyeokota risasi hapa kuna watu msaada unatokea sana humu
 
Matukio ya kikatili yapo kwamfano...

Mfungwa awapo shambani huwa wanalima kwa mstali ulio nyooka

Sasa mfungwa awapo shambani kulima hapaswi kulima kwa speed wala slow

Yani akiwaacha nyuma wenzie tafsiri yake nikwamba ana taka kukimbia hivyo atachezea mijeredi ya nyapala

Na wakimtangulia akabaki nyuma ya wenzie tafsiri yake nikwamba anategea hapo pia atachezea mijeredi

Sasa hebu fkilia unajituma kulima lakini huku nyuma nyapala hachoki kukupiga

Huo si ukatili?

Nyapala huyu atasema chuchu maeni huyu atasema simameni nakila anaye kuja huja na adhabu yake

Na kuhusu nyembe wanao ziuza na kunyoa niwatu special walio chaguliwa na nyapala mkuu

Na sjui huwa Wana zingatia Nini kuwa chagua Ila sjawai shuhudia tukio la kuchinjana na nyembe
Dah! Jela ni jehanamu kwa kweli. Yaani unalimishwa na mijeledi kama ng’ombe.
 
Dah! Jela ni jehanamu kwa kweli. Yaani unalimishwa na mijeledi kama ng’ombe.
Nakumbuka kwa mda ambao nili kaa pale Nika kutana na skukuu ya Christmas

Nikiwa ndani Sasa akaja mkuu wa mkoa kutembelea pale na aka ahidi kuwa letea mchele wafungwa ili angalau wapate kula wali pale badara ya ugari wa kila siku

Cha ajabu Sasa baada ya kuleta huo mchele

Ulipikwa wali ukiwa hauja wekwa mafuta na pia umechanganywa na unga wa ugali

Hawakuishia hapo nyama haikuungwa Nikama ilichemswa af nimifupa tupu

Sjui walienda kukusanya mifupa butcher haijulikani

Wafungwa walipo hoji wakaambiwa jera nisehemu ya mateso hampaswi kuhoji
 
Stori za vijiweni zina uongo mwingi sana.
Unadhani tupo kijiweni mkuu?

Au tuna fanya stories hapa?

Na Kama nadanganya si useme wapi nime danganya? Ili tuone Nani mwongo Kati yangu Mimi na wewe?

Mwisho. Ushawai ingia jera?

Kama umewai nisahihishe nilipo kosea lakini Kama huja wai usiombee kuingia hakufai huko
 
Back
Top Bottom